Ni ipi hatua nzuri ya kuchukua baada ya kumfumania mkeo/ mumeo kwa mara ya kwanza?

GAZETI

JF-Expert Member
Feb 24, 2011
5,277
6,673
Habari zenu wana JF, Naomba kuwaulizeni, iwapo umemfumania mkeo/ mumeo na ni mara ya kwanza ni hatua gani nzuri unatakiwa kuichukua. Ni kupokea fidia kutoka kwa MGONI kisha maisha yaende kama kawaida, kuwasamehe wote wawili, kuvunja uhusiano? Au hatua ipi unaona inafaa?

Binafsi upande wangu ndoa inakuwa imefia hapo. Nawasilisha!
 
Huwezi kupata jibu sahihi mpaka yakukute ndo utaona majibu yake unafirkiri unaweza toa hapa la hasha sababu nasema kuwa maana reaction utayokuwa nayo ndo itakuongoza kutoa uamuzi

Mkuu hiyo kitu haina kanuni unaweza ukajiandaa ikiwa ni pamoja na kumpa kibano mgoni na kumbe wewe ndio ukapewa kibano lol!
 
Huwezi kupata jibu sahihi mpaka yakukute ndo utaona majibu yake unafirkiri unaweza toa hapa la hasha sababu nasema kuwa maana reaction utayokuwa nayo ndo itakuongoza kutoa uamuzi
umesema kweli ndugu yangu,kawaida majibu unayapata palepale kwenye tukio
 
Kama inawezekana, sijahiti usiende kumfimania mke/mume wako! Ukimkuta live, HUTAMSAMEHE!

WAZEE wa zamani waliyajua hayo. Ndio maana wakati wanarudi nyumbani wakati wa usiku walikuwa wanaimba kuanzia mbali, ili mkewe asikie, na kama kuna kitu, atoe....

Siku hizi tunawasaka wagoni wetu...the world is going around
 
Muulize kwa nini kaamua kukusaliti, then mengine yatafuata kama ni kumsamehe au vip?
Ila asilimia kubwa ya wanawake wakiwafumania waume zao huwasemehe ila kwa wanaume huwa ni vigumu sana kuwasamehe wake zao
 
umesema kweli ndugu yangu,kawaida majibu unayapata palepale kwenye tukio

Well said huwezi kupanga cha kufanya kwenye kufumania unaweza kupanga utampa talaka then ukapandisha mori ngumi mkononi mambo magumu haya bana
 
Ya kwanza kabisa ni ya kumuomba Mungu akuondolee hasira na maamuzi ya kisasi.
Ya pili ni kuwaweka wote wawili chini na kuwaonya.
Ya tatu ni kuwasamehe.
Fidia itasababisha mkeo aendelee kumegwa kwani tayari utakuwa umepokea mahari kutoka kwa mume mwenzio
 
chanzo cha kumegwa mmeo/mkeo inaweza ikawa imesababishwa na wewe mhusika ,hivyo haitakiwi papara kwenye kuchukua maamuzi!
 
Kama inawezekana, sijahiti usiende kumfimania mke/mume wako! Ukimkuta live, HUTAMSAMEHE!

WAZEE wa zamani waliyajua hayo. Ndio maana wakati wanarudi nyumbani wakati wa usiku walikuwa wanaimba kuanzia mbali, ili mkewe asikie, na kama kuna kitu, atoe....

Siku hizi tunawasaka wagoni wetu...the world is going around

Dah okada leo umenipa kitu kipya ambacho sikuwahi kukifikiria kabla. Nilikuwa nawaona sana baadhi ya babu zangu wanaporudi kama sio kuimba basi atakuwa anapiga aina fulani ya filimbi ambazo siku hizi hazipo tena au atafanya kitu ambacho kinatujulisha mapema kuwa anakuja. Sikujua kumbe ndio maana yake, lakini ah...... Bora kufumania kuliko kumkurupusha mwizi wako.
 
Habari zenu wana JF, Naomba kuwaulizeni, iwapo umemfumania mkeo/ mumeo na ni mara ya kwanza ni hatua gani nzuri unatakiwa kuichukua. Ni kupokea fidia kutoka kwa MGONI kisha maisha yaende kama kawaida, kuwasamehe wote wawili, kuvunja uhusiano? Au hatua ipi unaona inafaa?

Binafsi upande wangu ndoa inakuwa imefia hapo. Nawasilisha!

Tatizo issue nyingine hazina formula kama 1+1=2
 
Ya kwanza kabisa ni ya kumuomba Mungu akuondolee hasira na maamuzi ya kisasi.
Ya pili ni kuwaweka wote wawili chini na kuwaonya.
Ya tatu ni kuwasamehe.
Fidia itasababisha mkeo aendelee kumegwa kwani tayari utakuwa umepokea mahari kutoka kwa mume mwenzio

Kwenye nye nyekundu nakubaliana nawe, Kwenye blue nahitaji kutafakari mara kumi hapo kwenye kijani nakuunga mkono 100% ingawa kwa maisha ya sasa wengi wanakimbilia hapo kwa macho yangu nimeshuhudia mambo mawili yakifanyika
1. Kudhalilishwa yule mwanaume kwa kufanyiwa vibaya (I hate this way)
2. Nimeshuhudia mtu akichajiwa 4 mil.(milioni nne) baada ya kufumaniwa.
 
habari zenu wana jf, naomba kuwaulizeni, iwapo umemfumania mkeo/ mumeo na ni mara ya kwanza ni hatua gani nzuri unatakiwa kuichukua. Ni kupokea fidia kutoka kwa mgoni kisha maisha yaende kama kawaida, kuwasamehe wote wawili, kuvunja uhusiano? Au hatua ipi unaona inafaa?binafsi upande wangu ndoa inakuwa imefia hapo. Nawasilisha!
pole mkuu kama umefumania
 
pole mkuu kama umefumania
Ha ha ha haaaa! siku nyingi na nilishamwacha yule mwanamke, wakuu wananishangaza hapa jamvini eti hakuna kanuni wakati wengi nawaona wakichukua Fidia
 
Fumanizi alina maandalizi. Waweza kujiandaa kutoa kichapo ukafika eneo la tukio ukaangua kilio badala ya kutembeza kipigo. Kwa hiyo subiri ya kupate solution utaipata on the sport.
 
kama mwenzio alisha ku chosha ni rahisi mno..
unatoa tu talaka basi,na kuwatangazia wote why umemuacha..

but kama unampenda kweli,ni tatizo kubwa
 
Back
Top Bottom