Nashukuru sana kupata nafasi hii ya pekee mimi nami kuweza kujikaribisha humu kwani kabla sikuelewa nikaingia kabla ya kupiga hodi.Jamani ndugu zangu kwanza nisameheni kisha mnikaribishe .Naamin nami nitajifunza mengi kutoka humu na zaidi sana kupata kuchangia mengine ambayo naamin ni ya kujenga.Basi kwa pamoja hebu tufanye bidii na kama hiyo haitoshi tusimame kidete kuhakikisha Tanzania inatoka katika kuitwa kichwa cha mwendawazimu na kuwa Baraka kwetu sisi na wale wote wenye kuitakia mema nchi yetu nzuri tuliyobarikiwa na Mungu wetu.