Ni dua gani ya kumuombea mtu aliokudhulumu ili apate mikosi?

Amini nakwambia,kama kweli ulitendewa hivo na ile pesa au nguvu yako hukumzulumu mtu,basi hakika malipo yatafanyika kwake kwa njia yoyote ile na mara nyingi Mungu umlipa mtu kiasi asijue kama yale ni malipo kwa aliyemfanyia mwanzo na hata wewe uliyetendwa waweza usijue kama yule "adui" yako yale anayopitia ndio malipo yake kwa ubaya alioutenda kwako.
 
Hakuna kitu kama Iko, ,acha kuchafua uislamu, ,hakuna haya katika msahafu za kufanya uchawi kafiri wewe
Nauchafua kwani uisilamu msafi? wewe hujui uisilamu kabisa. Unajua mtume mohd alikuwa anabaka katoto ka miaka nane?
 
Embu acha masiala ,,unashindwa nini kumpeleka mahakamani ???/acha uoga . peleka mahakan ,ikishindikana ndo umwachie Mungu .


Hapa duniani hamnaga haki kwaiyo nilazima upambane na hali yako !!.Siulipeleke mahakaman !!!.
 
Dua ya aliyedhulumiwa ni moja kati ya dua ambazo huwa hazirudi patupu (pia dua ya mzazi kwa mtoto na mtoto mwema wa mzazi).
Kusononeka pee yake dhidi ya aliyekudhulumu ni dua kubwa kulio hata kuvunja nazi na chungu, ni vile tu mkuu una haraka kuona mambo yakitokea fasta, jaribu kuvuta subira(mungu yupo na wenye kusubiri) wala huna haja ya kuingia kwenye ushirikina, wakati ukifika utashuhudia (wakati ukifika hakuna wa kumkinga na kama wakati bado ataendelea kusalimika ingawa ni kwa muda), muachie mungu,mtesi wako atalipia dhulma( mungu ni mkali wa kuadhibu) aloifanya nawe utapata kikubwa zaidi ya ulichodhulumiwa kwani mungu ni mwenye fadhila kubwa.
 
Pole sana. Mi kuna jamaa nimemuweka kiporo kwa miaka miwili kabla sijarevenge namuacha ajisahau tu. Ubaya ubaya...
Sure mkuu ,,, hapa duniani hamna haki ...kuna mtu anakupa pigo ambalo mpaka unakufa linazidi kukuathiri tuuuu...

Yaan kiukweli huwa napataga hasira namijitu inayofanyia wenzao ubaya ,, yaaaan kuna wakati unataman place risasi ktk kichwa cha mtu !!..

Kuna mtu aliwahi mtapel (--) 24 M Kwa awamu mbili ,, Mara yakwanza 10M Mara yapili 14 M,, tulikuaga wadogo I was in kidato chakwanza ,,alafu hilo libaba ltulikaa nalo hom miezi miwili ,,,Popote lilipo ,, ananyoa kipala kichwan mwake anakama mistari mistar yaan km mabonde ivi ya mistar,, ni muislam anajiita Sheikh, nimrefu mnene mweusi !! Ila kichwan ndo rahisi kumjua na anamacho yaujanja ujanja !!


kuna wakat matatizo huzaa matatizo. huyu jamaa nimoja yamtu ambaye Sitokaa nimsamehe popote alipo..
 
Umeomba ushauri au kujua dua lenye ufanisi lakini hukuenda mbali zaidi kuelezea kiini cha kuzulumiwa.Bila kujua kisa kizima kilichopelekea wewe kuzulumiwa na mtu wako wa karibu si rahisi kupata ushauri mzuri. Kwa mtazamo wangu kiasi ulichokitaja unaweza kukipata kwa kufungua kesi mahakamani kama kesi ya madai. Kuomba dua ili mtuhumiwa adhurike?.., Binafsi sina uhakika kama inafanya kazi ingawa mimi pia kuna wakati niliwahi kumlaani yule aliyeniibia.

Kisa changu kilitokea mwaka 1977 pale Mwenge secondary school tukiwa kwenye mashindano ya UMISETA kanda ya kati. Nilikuwa na daruga zilizokuwa zinajulikana wakati huo kama ''Six meno'' ziliyotengenezwa mahususi kwa ajili ya Franz Backenbau na ilikuwa na picha yake kwenye ulimi wa daruga kwa wale wanaofahamu mambo ya kambumbu. Ilikuwa ni buti ya nguvu kwa wakati huo.

Kwa kuwa ilikuwa kitu adimu ukilinganisha na zile daruga zetu za Bora shoes wakati huo, wajanja wakazipangia mkakati wa kuziiba na siku moja wakafanikiwa kuziiba mimi nikiwa mesini kwenye uji saa wa nne, kosa langu ni kusahau kuzifungia kwenye locker langu zikawa zimeondoka jumla. Nilipagawa siku hiyo mpaka jioni yake nikaenda stendi kupanda gari niende Iguguno kwa mganga mashuhuri ambaye alisifika sana kurekebisha tabia za watu wabaya kama wezi na walaghai. Kweli nilifika kwa mganga lakini sikuonana nae kwa kuwa hadi saa sita usiku alikuwa hajatokea hivyo asubuhi saa 12:00 ikabidi nirudi shuleni mikono mitupu. Hadi siku ya leo sijui kama dua langu la kuku lilimpata mtu.

Jipange upya, fanya kazi kwa bidii, utapata zaidi ya hizo kilo mbili na zaidi ya nusu.
 
Wakuu kwanza samahanini kwa kuwasumbua, Pili. Lengo la uzi huu ni kuomba ushauri wenu kwa kilichonipata. Nitaenda kuwahadithia kwa kifupi sana
.
Mimi ni kijana wa kiislamu, naishi Dar, mwezi mmoja uliopita au mwezi na nusu nilidhulumiwa pesa tsh 2.7M ( million 2 na laki 7 ) sikwambii maumivu nilionayo moyoni, yaani naumia sana halafu alionidhulumu ni mtu wangu wa karibu sana.

Mtu niliemuamini kwa kila kitu, nimekuwa nikiomba Mungu, Mungu naomba unilipie, mpe mabalaa na mikosi ya kila aina, huwezi amini hata saivi ninavyoandika uzi huu nimetoka kuomba, lakini naona bado Mungu hajanilipia.

Je nifanyaje, kuna dua gani ya kumuomba Mungu ampe mikosi? Yaani kiasi kwamba ajute kula jasho langu, mimi ndio kwanza mwaka huu nimefungua kibiashara changu nimeanza kutafuta maisha alafu ananidhulumu.

Nifanyaje? Ndugu zangu naumia mno.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama unaamini watumishi tafuta mtumishi wa Mungu akuombee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sure mkuu ,,, hapa duniani hamna haki ...kuna mtu anakupa pigo ambalo mpaka unakufa linazidi kukuathiri tuuuu...

Yaan kiukweli huwa napataga hasira namijitu inayofanyia wenzao ubaya ,, yaaaan kuna wakati unataman place risasi ktk kichwa cha mtu !!..

Kuna mtu aliwahi mtapel (--) 24 M Kwa awamu mbili ,, Mara yakwanza 10M Mara yapili 14 M,, tulikuaga wadogo I was in kidato chakwanza ,,alafu hilo libaba ltulikaa nalo hom miezi miwili ,,,Popote lilipo ,, ananyoa kipala kichwan mwake anakama mistari mistar yaan km mabonde ivi ya mistar,, ni muislam anajiita Sheikh, nimrefu mnene mweusi !! Ila kichwan ndo rahisi kumjua na anamacho yaujanja ujanja !!


kuna wakat matatizo huzaa matatizo. huyu jamaa nimoja yamtu ambaye Sitokaa nimsamehe popote alipo..
Hata mimi hilo jamaa limefuga midevu na ile alama ya siasa kali linayo ***** hata yanavyoshughulikiwa huko misi.kitini acha yakione...
 
Nauchafua kwani uisilamu msafi? wewe hujui uisilamu kabisa. Unajua mtume mohd alikuwa anabaka katoto ka miaka nane?
Haya matusi katika imani za watu hapa sio mahala pake.
Tafadhali sana

You get what you work for not What you wish for
 
Unauhakika? kuna aya kwenye msahafu unasoma baada ya hapo ulomsomea mambo inavurugika kinoma. Je wajua unaweza kutumia msahafu kufanya uchawi wa aina nyingi tu?
Kitabu chochote cha Mungu wa mbinguni hakiwezi kutumika kufanya uchawi, bali kupambana na uchawi. Huo msahafu kama unatumika hata kwenye uchawi na visasi basi una walakini... Elewa hizo ni kazi za Ibilisi...

Sent from my Nokia-tochi using JamiiForums mobile app
 
Sali sana ili M/Mungu akuondolee uchungu ulio nao moyoni ,akujaalie mafanikio ili mdhurumaji ayaone na ayajutie aliyokutendea maana yamemkosesha Mengine mengi mazuri ya kuwa karibu na wewe,Mwambie M/Mungu kama ulinipa zile kihalali basi naamini utanipa nyingine nyingi,kamwe usitamke neno la chuki maana M/Mungu huwa hazihesabu chuki zako kama moja ya mahitaji yako ila huzihesabu kheri zako


Sent using Jamii Forums mobile app
Well said...

Sent from my Nokia-tochi using JamiiForums mobile app
 
Hata mimi jilo jamaa limefuga midevu na ile alama ta siasa kali linayo ***** hata yanavyoshughulikiwa huko misi.kitini acha yakione...
Hahahah! Umekinukisha mkuu, ngoja waje

Sent from my Nokia-tochi using JamiiForums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom