Ni dhana potofu kusema Mwanaume hasifiwi Uzuri

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,900
NI DHANA POTOFU KUSEMA MWANAUME HASIFIWI UZURI. NI AKILI NA KAMPENI ZA KISHETANI.

Anaandika, Robert Heriel
Kuhani.

Soma Kwa Utulivu. Hizi ni falsafa za Watibeli, Kutoka Nyota yenye mbawa Mbili. Isomwe Kwa hekima Kwa walio na hekima wapate ufahamu.

Zipo kasumba nyingi Mbaya katika jamii zetu. Moja ya kasumba hizo Mbaya ni Hii isemayo; MWANAUME HASIFIWI UZURI. Nafikiri hata wewe umewahi kuisikia au pengine hata kuitaja na au uliwahi kuitumia. Hapa tutajadili Kwa Hoja, wala sio mihemko.

Uliwahi kujiuliza ni Kwa nini Mwanaume HASIFIWI UZURI? Je muanzilishi WA kasumba au dhana hii alikusudia nini achilia mbali kutaka kumjua alikuwa Nani. Je, ni kosa au vibaya Kwa mwanaume kusifiwa UZURI? Ni nini ajenda ya dhana hiyo?

Je, dhana hiyo ililenga kumfanya mwanaume asijisikie na kuwa na Kiburi na majivuno? Au dhana hiyo ililenga kuhifadhi thamani ya mwanamke na ajisikie fahari kuwa uzuri ni Mali yake? Au dhana hiyo ilitungwa kuchochea fikra na Falsafa ya mwanaume ili ajikite zaidi katika uzalishaji Mali na ulinzi WA jamii na dunia Kwa ujumla?

Au dhana hiyo ilitungwa ili kumfanya mwanaume ajisalimishe na kuwa mnyenyekevu Mbele ya mwanamke angalau Kwa kipengele hicho kimoja?

JE, NI KWELI MWANAUME SIO MZURI HIVYO HAHITAJI KUSIFIWA NA KUTUKUZWA?
Ni Kwa nini Mwanaume akijisifia ni Mzuri Wanawake wanachukia? Unaweza kufanya utafiti katika Jambo hilo.
Ukweli na uhalisia ni upi? Sisi Watibeli, tunayaangaliaga mambo katika uhalisia wake, yaani uhalisia unatangulia ndipo mitizamo na Maoni yetu yafuate.

Kidini, waamini wa Biblia na Quran watakubaliana nami kuwa walikuwepo Wanaume wazuri wa Sura, maumbile na kitabia. Nitataja wachache ambao ni maarufu, Nabii Yusufu bin Yakobo, Nabii Musa Mlawi, Nabii Yoshua mwana wa Nuni, Mfalme Sauli, Mfalme Daudi mwana wa Yese, Absalom mwana wa Daudi, Suleiman mwana wa Daudi, na Daniel. Hao ni Kwa uchache. Na wote hao tunajua shughuli yao ikoje, hawakuwa Watu wa mchezo Mchezo.

Kasumba hiyo haikuishia kwenye uzuri WA maumbile, imepenyezwa mpaka kwenye uzuri wa kitabia.
Imekuwa ni kasumba kuwa Tabia zote mbayambaya kama ukatili, ushenzi, uuaji, na matabia mengine niya mwanaume Jambo ambalo sio KWELI. Uchunguzi wangu unaonyesha kuwa matukio mengi mabaya ukiangalia Kwa jicho la tatu mzizi wake umetoka Kwa Mwanamke. Ingawaje wengi huona shida kulisema Jambo hili. Labda Kwa kuogopa kuonekana wataonekanaje lakini ukweli umekaa hivyo.

Ili mtu akuchafue ni lazima aanzie nje. Yaani ili uonekane Mbaya Mbele ya jamii ni lazima Watu waanze kukupaka Matope ili uwe mchafu. Uonekane Mbaya. Kisha wakupe jina Baya. Ukishamchafua MTU Kwa nje ambapo wengi ndio humuona basi watamtambua MTU huyo kama MTU Mbaya hata kama ni mzuri.
Ni hakika kuwa Sisi wanaume ni Watu wazuri, iwe wazuri wa Sura au maumbile na hata wazuri wa kitabia. Hilo linathibitika kiimani/kidini, kimila na Kisayansi.

MTU anayekuambia usijisifie uzuri ni MTU hatari Sana. Yaani anaona wivu au anaumia unapojisifia au kusifiwa UZURI ni dalili anataka kukuchafua na ili uonekane Mbaya. Bado hujamuelewa Taikon, Subiri utanielewa tuu.

Side effects ya Jambo hili utaliona katika level ya Chini kabisa ya Familia. Hakuna mtu wala kiumbe Duniani kisichopenda kitu Kizuri. Watoto hupenda vitu vizuri na watu wazuri. Mara nyingi Ila sio zote, Wamama hufanya kila jitihada kuharibu Uzuri wa Baba ndani ya nyumba iwe Kwa kuwalisha sumu Watoto kuhusu ubaya wa Baba Yao.

Pili, huwapa Stress Wababa na kuwatumikisha na kuhakikisha Baba anapoteza nuru yote, na kunyong'onyea, unakuta Baba anashindwa hata kuzihudumia ndevu zake, shavu limekakamaa na kapoteza Nuru na utukufu wa mwanaume. Huku akiambiwa mwanaume HASIFIWI UZURI, Ila Kazi. Mimi nasema, mwanaume anasifiwa Akili, uzuri, nguvu, kazi n.k.

Kula Kwa jasho haimaanishi upoteze uzuri wako kama Mwanaume. Haimaanishi usijipende, haimaanishi usijijali.
Jukumu la Kwanza la mwanaume au MTU yeyote ni Kujipenda mwenyewe, hiyo ni amri katika dini, amri kisayansi, na amri Kiasili. Jukumu la pili la mwanaume ni Kumpenda Mungu (Hii Ipo kiimani), jukumu la tatu ni kumpenda Mkeo na familia yako.

Kasumba na dhana ya mwaanume HASIFIWI UZURI, imetungwa Makusudi ili kumfanya mwanaume asijipende, yaani avunje amri ya Kwanza ya kujipenda mwenyewe. Hiyo ndio inawafanya wanaume wengi waonekane ni wachafu wachafu, wasijijali wenyewe, na Matokeo ya kutokujijali yanajulikana, usipojipenda na kujijali hakuna atakayekujali.

Sio ajabu mpaka Watoto wetu tuliowazaa wenyewe hawatupendi Baba zao Kwa sababu Sisi hatukujipenda na kujijali.

Nimeishi na ukoo wenye Mababu wenye umri mkubwa, na wengi wao ni mabrazameni, wanajipenda, wanapenda wake zao na familia zao. Sio ajabu mpaka sasa licha ya kuwa na umri mkubwa usiopungua miaka 80 lakini Watoto na wajukuu zao wanawapenda, wake zao wanawaheshimu kama waume Bora.

Wazee wangu wanaamini katika mtazamo kuwa, mwanaume ni Mzuri, na walishanipa mafunzo hayo. Ndio maana nimeamua leo Hii ku-share nanyi hiki Kidogo.

Angalia nature, muangalie Jogoo, muangalie Simba dume, muangalie Ng'ombe dume, muangalie Tausi dume, muangalie Njiwa dume, muangalie beberu, Angalia wanyama, ndege na Samaki na hata hizo hadithi za Malaika wote hao ni madume.

Jipende, hiyo ndio namna ya Kwanza ya kuwa mwanaume wa kweli. Kadiri unavyouathiri uzuri wako Kwa kutojipenda na kujijali ndivyo unavyojitengenezea Maisha magumu Kwa sasa na baadaye. Usijesema ooh! Sijui nafanya Hivi Kwa sababu ya Mke au Watoto. Fanya Kwanza waajili yako, then wengine wafuate. Hiyo ndio namna ya kuilinda kesho yako.

Zingatia, unapojipenda usisahau kuipenda familia YAKO.

1. Kula vizuri
2. Vaa vizuri
3. Paka Mafuta mazuri.
4. Fanya mazoezi ya Mwili
5. Mara mojamoja fanya starehe kama kwenda Club, tembelea nchi zingine au kama kipato ni Kidogo tembelea hata wilaya au mikoa mingine, nenda kucheza mziki.
6. Pumzika vyakutosha
7. Usinywe pombe au vilevi kupita kiasi.
8. Mtafute Mungu wako Kwa bidii
9. Cheza na furahia na familia. Kamwe isikuendeshe
10. Usimdhulumu mtu.

Ni Yule kuhani, Kutoka Nyota ya Tibeli

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Zingatia, unapojipenda usisahau kuipenda familia YAKO.

1. Kula vizuri
2. Vaa vizuri
3. Paka Mafuta mazuri.
4. Fanya mazoezi ya Mwili
5. Mara mojamoja fanya starehe kama kwenda Club, tembelea nchi zingine au kama kipato ni Kidogo tembelea hata wilaya au mikoa mingine, nenda kucheza mziki.
6. Pumzika vyakutosha
7. Usinywe pombe au vilevi kupita kiasi.
8. Mtafute Mungu wako Kwa bidii
9. Cheza na furahia na familia. Kamwe isikuendeshe
10. Usimdhulumu mtu.
 
Mkuu tafuta pesa, ukimuangalia diamond na nyimbo yake ya kwetu mbagala na sasa ni vitu viwili tofauti, pia ray kigosi, kunywa maji mengi pia bila kuchoka

Hapo kwenye kutafuta Pesa, ongezea tafuta Pesa kwaajili yako, kisha wale watakaokupenda watafaidi sehemu ya hizo Pesa.

Vijana wengi wanatafuta Pesa Kwa nguvu lakini sio kwaajili Yao.
Wanatafuta Pesa kwaajili ya Wanawake, mwishowe wanakosea vyote Wanawake na Pesa.

Ila ukitafuta Pesa kwaajili yako, utapata vyote
 
Sema kiukweli wanume wamechoka Sana mtu anafanya Kazi ngumu akipata pesa anampa Mwanamke na Kunywa pombe
 
Mkuu tafuta pesa, ukimuangalia diamond na nyimbo yake ya kwetu mbagala na sasa ni vitu viwili tofauti, pia ray kigosi, kunywa maji mengi pia bila kuchoka
Ingekuwa vizuri ungeanza kuzitafuta wewe na umuonyeshe una earn kiasi gani kwa mwezi. Pia ungeweka wazi kuwa we' ni mtumishi mdaka tonge mwisho wa mwezi au la!
 
Back
Top Bottom