Ni dakika 55 zimepita sasa nikisubiri basi la Mwendo Kasi Kituoni Gerezani

mgonjwa

JF-Expert Member
Dec 2, 2013
514
223
Ni saa moja kasoro dakika 5 nipo hapa Gerezani nasubiri mwendo kasi kwenda Morocco. Kuna tatizo gani kwani tuliahidiwa kila baada ya dakika tano bus itakua inaondoka kituoni. Huu mradi kwa kweli ni jipu.

Mkimalizana na UKUTA Sept 1 mtupie jicho na huku, imekua kero sasa!
 
Hawa jamaa siyo wabunifu hata kidogo. Nilishaandika humu kuhusu kuboresha route ya Morocco, huenda hawakunielewa au wanabanwa na taratibu za sumatra.
 
Haya mabasi ikifika saa tano asubuhi yanatoweka;
yanaonekana tena saa kumi na moja jioni;
sijui ndo yanaenda kupumzika.
 
Nadhani kuna tatizo la kiutawala katika mradi huu wa mabasi. Siku za mwanzo mradi ulipozinduliwa kulikuwa na mabasi mengi ya kutosha. Kadiri siku zinavyoenda ndiyo yanazidi kupungua. Hii inadhihirika kwa mabasi hayo kujaza watu kupita kiasi hasa nyakati za asubuhi na jioni. Kuna baadhi ya vituo kupata nafasi kwenye mabasi haya ni tatizo kubwa. Mfano, basi likitoka Gerezani au Kivukoni linakuwa limejaza kupita kiasi hivyo kusababisha mabasi haya kupita vituoni bila kuchukua abiria. Abiria wa kituo kama Ubungo kwenda Kimara nyakati za jioni hupata shida sana. Nashauri kuwe na route ya kuanzia Ubungo kwenda Kimara kuanzia
 
halafu pia waangalie utaratibu wa ule mlango wa kutokea pale gerezani.. watu wanabanana mno, wezi nao wanatumia hiyo nafasi kuiba.. niliponea chupuchupu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom