Ni bora wananchi tuchangie gharama za ufanisi wa Bandari zetu, ila si kuwapa DP word kwa mkataba sawa na bule!

Trable

JF-Expert Member
Jan 3, 2023
1,783
3,281
Ukweli ni kwamba, nchi yetu ina watu masikini kiasi ambacho wengine ni huruma ukiwaona!

Wapo ambao, kula yao inategemea Jirani yake ama wapita njia, Mungu amewapa furaha ya aina gani siku hiyo ili tu kuwapa chochote kitu

Baadhi ya wabunge, wanatoka kwenye maeneo ambayo watu wake ni masikini kiasi cha huruma na kusikitisha,

Licha ya hivyo, wabunge hao wamekuwa ni watu ambao hawawezi kuwasemea watu wao badala yake wamekuwa ni watu wa kwenda Bungeni kupitisha miswada ya hovyo ambayo haina uhusiano wowoye wa kuwapunguzia umasikini wananchi wao, na badala yake, wao ndiyo wamekuwa ndiyo watu wa kuwasababishia umasikini zaidi!

Mkataba wa DP kwa nini wananchi wanapiga kelele?

Sababu za kwa nini wapewe Bandari zetu bado hazina mashiko hata kidogo!

Mkataba ambao unawapa DP world Bandari zetu zote bila kuwepo ukomo wa mkataba, unatufanya wananchi kuanza kuhoji uwepo wa wabunge Bungeni tuliowatuma kwenda kutetea masilahi ya nchi na wananchi!

Ni kweli kabisa sisi watanzania hatuwezi kuendesha Bandari zetu?

Je? Ni ufisadi au uzembe wa watu wetu ndio unaifanya serikali ione ni bora Bandari hizi wapewe warabu tena bila ukomo?

kama ni uzembe, uzembe hauwezi kuwa wa watanzania wote, kuna msemo usemao, Jinsi alivyo mchungaji, na kondoo wake ndivyo walivyo, kwa hiyo hilo la uzembe na ufisadi linategemea mchungaji . Kwenye hili, ccm hamuwezi kukwepa!

Unajiuliza, Je? Ni fedha za kununua mitambo ya kuifanya bandari yetu iwe ya kisasa ndiyo hatuna? Iweje kwenye bajeti ya kununua mashangingi ya serikali tunafanya tena kwa asilimia 100%?

Hata hivyo, kampuni ya DPW, kwa asilimia kubwa ya wananchi wameikataa,

Mimi kisamv kama mtanzania mzalendo na mpenda nchi yangu, niko tayari kuchangia Miamoja elfu huku nikiwaomba watanzania kwa mamilioni yetu kuuunga mkono ili tuiwezesha serikali yetu inunue mitambo ambayo DPW wanaturingishia kwamba hatuna huo uwezo wa kuinunua

Na wakati huo huo, tutamuomba Mh Rais wetu awe mkali tu ili kuwadhibiti hawa ambao tumedhani ili kuwadhibiti, dawa yao ni kubinafisisha Bandari zetu!

Tanzania bila DPW, tunaweza!
 
Ndiyo mana hata viongozi wa dini wameamua kupiga kelele hata baadhi ya wananchi mtu mmoja mmoja kumbuka bunge hili siyo chaguo la wanchi haliwezi kuwawawakilisha wananchi walio wengi
 
Back
Top Bottom