Ni bidhaa gani naweza kuziuza nikiwa na gari au Bajaji, Gari Duka

Hyrax

JF-Expert Member
May 20, 2023
620
1,581
Wanakijiji wa JamiiForums mimi nipo Dar saivi ninafikiria jambo fulani la kujikwamua kiuchumi ila hii kidogo naipigia mahesabu kitofauti nataka ninunue ka-ist au bajaji then ukiachilia mbali sijui kusafirisha watu sijui uber au bolt nataka hicho chombo nitakachonunua kiwe ndio duka lenyewe sitaki nikodi fremu.

Nataka niwe naenda chimbo nachukua bidhaa mtakazonishauri hapa then napambana huko mtandaoni kutangaza bidhaa au nabeba furushi langu naingia mitaa iliyochangamka nauza mzigo niliubeba kwenye ka-ist changu au Bajaji nikiona wateja wamepungua nahamia mtaa mwingine mpaka mzigo unaisha narudi home kulala je ni bidhaa gani naweza anza nazo zinakanisaidia kupambana na maisha hapa mjini Dar.

Ushauri wenu nitauzingatia kwa unyenyekevu, asanteni
 
Sambaza bidhaa za ngano (bites) kama mikate,Andazi, Cake, madukani au vibanda vinavohitaji huduma hii, ingawa ni vyema hizo bidhaa ukawa ni sehemu ya uwekezaji wako mwenyw.
 
Chukua kirikuu, halafu kila asubuhi nenda Mabibo chukua gunia tano za njegere mbichi za Morogoro halafu ingia kwenye njia panda wanapopita watu wengi, pima kisado kwa elfu mbili mbili na kimbo kwa buku.

Baada ya mwezi niite tukapate bia.

Aquila non capit muscas!
 
Gari Duka kuna jamaa mmoja yy anauza Asali n kalanga kazipaki vzr. Zinavutia mnooo. Hata mm hua namuungisha.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom