Ni adhabu ipi iwe mbadala wa viboko kwa wanafunzi watukutu mashuleni?

Kipindi nasoma seminari, sikuwahi kushuhudia kabisa uchapaji wa viboko, lakini tulikuwa na discipline ya hali ya juu kabisa.

Watovu wa nidhamu walipewa adhabu ya kupalilia mashamba, kusafisha mabanda ya nguruwe, kufukuzwa shule na kupewa suspensions.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ingekuwa shule za seminari na nyinyi mnaletewa wanafunzi na serikali, hiyo unayoiita discipline ya hali ya juu ungeisikia kwenye redio tu. Na ndio maana huko seminari wanachuja sana kwenye ile mitihani yao ya kujiunga na shule yao, washajua mtoto mwenye akili za ununda hawezi kufikisha wastani wa 90%, na ndio huo wanaweka mwanawani, nunda hata akijikakamua vipi anaishia wastani wa 35% hahahahaaaa chaliii anarudi kwenye shule yake ya kata aliyochaguliwa.
 
Viboko avina maana yeyote watoto waliolelewa kwa viboko kichwani wanakuwaga zero na maisha uwashinda kabisa ...Mfano mwanafunzi unamwambia afike shulen saamoja kamili kuwa akichelewa zaidi ya hapo apigwe bakora uwo niujinga wakiwango cha PhD

Viboko niujinga mtupu.
Mwanao akichelewa shule unataka aambiwe aende library

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kabla hajaadhibiwa juu ya utukutu wake lazima ijulikane nini kimesababisha awe mtukutu, tatizo lianzwe hapo....

Sent from Jamii Forums using siemens kidole juu.
 
Wazazi au walezi wa mwanafunzi ndio wawe wanachapwa. Mwanafunzi akifanya kosa shuleni mzazi/mlezi anapigiwa simu akifika anachapwa fimbo 4 za ukweli anarudi zake kwenye majukumu yake! Watoto watakuwa na nidhamu tu hakuna namna.
 
Ingekuwa shule za seminari na nyinyi mnaletewa wanafunzi na serikali, hiyo unayoiita discipline ya hali ya juu ungeisikia kwenye redio tu. Na ndio maana huko seminari wanachuja sana kwenye ile mitihani yao ya kujiunga na shule yao, washajua mtoto mwenye akili za ununda hawezi kufikisha wastani wa 90%, na ndio huo wanaweka mwanawani, nunda hata akijikakamua vipi anaishia wastani wa 35% hahahahaaaa chaliii anarudi kwenye shule yake ya kata aliyochaguliwa.
Sio kweli.

Hata hivyo, pamoja na hayo yote, wanafunzi watovu wa nidhamu wanaweza kupewa adhabu kali za mikono, kufukuzwa shule, au kusimamishwa masomo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sio kweli.

Hata hivyo, pamoja na hayo yote, wanafunzi watovu wa nidhamu wanaweza kupewa adhabu kali za mikono, kufukuzwa shule, au kusimamishwa masomo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kikubwa hapa ni kuwasihi walimu wetu kucontrol jazba zao. Fikiria mwanafunzi unampa adhabu za mkono hafanyi au analipua lipua. Unamhoji kwann hakulima au alime alivyolima vile hovyo hovyo, anakujibu majibu yanayokuacha wa mnyama. Aaaaa bora sio mwalimu aisee, maana lazima achezee za mbavu.
 
Asimamishwe masomo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
TATIZO LA SIKU HIZI WALIMU WENGI NI WAHUNI.

HUWEZI KUONA MWALIMU ANATOA MAONYO WALA MAELEKEZO YA KUMJENGA MWANAFUNZI.

VIJANA WANAHITAJI MIONGOZO, MAKARIPIO, NA USHAURI.

SIAMINI KABISA KATIKA "UNUNDA".

BINADAMU YOYOTE ANAWEZA KUELEKEZEKA NA KUFUNDISHIKA.

HII FALSAFA YA VIBOKO NI FALSAFA YA KING'OMBE NG'OMBE TU, HAINA UHALISIA WOWOTE.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shule za dini zinafaulisha na watoto wanakuwa na maadili mema sababu,hawacheki na kima,mtoto akijifanya kaenda kukua hapo shule anarudishwa nyumbani akamfate mzazi wake,aje afokewe badala yake.akirudia tena kosa nao wanamkataa mtoto wako,tena kwa unoko na ada unarudishiwa.

Jaman wazazi/walezi wangu walikuwa wanoko,sijawahi kuchekewa mimi kwenye maslahi mapana ya ustawi wa tabia yangu.nashukulu leo hii mimi si kijana wa ajabu ajabu,ili kuunga mkono juhudi za wazazi wangu namimi nitakuwa mnoko kwa kizazi changu chote.

Sent using Jamii Forums mobile app
Unoko ndio adhabu gani? Majibu yako hayako clear.
Shule za dini wanapiga? Wazazi wako walikupiga?
 
maoni yangu ni kuwa kama walimu hawawezi ku control stress zao waache tu kutupigia watoto...watawaua...
Hata mzazi hupaswi kupiga mtoto kwa hasira...unaweza kumuua sababu kavunja kikombe tu...
Viboko ni short cut ambayo haiko effective kihivyo....unatakiwa uwajue wanafunzi wako na kuwajenga kimaadili kwa kuwashauri na kuwaonyesha mifano mizuri...(role models).

Mimi japo nimetandikwa na wazazi (si saana) lakini siwezi ku attribute tabia na mafanikio yangu kwa viboko...
Ni ukaribu wa wazazi wangu hasa baba (ambaye hakuwa mpigaji kabisa).

Kama viboko vinalipa kabila fudenge lisingekuwa linaongoza kwa tabia mbaya....

Simaanishi kuwa sipigi wanangu...lakini inaniuma sana baada tu ya kumpiga...
Nadhani katabia ka kupiga hakapotei maana kanarithishwa....I wish nisingewagusa ila ningejikita kwenye kuwaelekeza bila kuchoka.... Ila mpaka nipige mtoto ni kazi sana,
 
Asimamishwe masomo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kabla hamjafika huko kwenye kumsimamisha masomo, lazima kuna mahali mlianzana na huyo mwanafunzi. Fikiria umemkuta mwanafunzi na kosa linalostahili achapwe viboko, unamwambia nyoosha mkono nikuchape, anakwambia mwalimu mi hunichapi. Unaona isiwe tabu, unamwambia tangulia ofisini, ukidhani labda kule kwa kuwa mpo walimu wengi ataogopa na utamchapa kirahisi, nako ukifika anakudishia vilevile. Mwalimu anapanic, na kuanza kumchapa dogo randomly, dogo anakamata fimbo na kuivunja. Sasa hapo ndio ile mitama , mateke na mangumi unayoiona kwenye video za kurekodiwa inapoanzaga. Mwalimu tayari anajazba, dogo nae ni nunda by nature, hahahahahaa yajayo lazima mfumbe macho kwakweli.
 
Na unajua kuna umri fulani hata mzazi unaona aibu kumpiga mwanao...
Sasa hawa walimu wanataka eti kumchapa mtoto ambaye ana nguvu zaid yao...
Wajiongeze...
Mtoto anapozidi kukua anahitaji kuheshimiwa na wazazi, walimu na jamii
 
Back
Top Bottom