Ndachuwa
JF-Expert Member
- Mar 8, 2006
- 6,269
- 4,569
Hivi karibuni wimbi la wananchi kuandamana ili kishinikiza viongozi wao waondoke madarakani hasa nchi zinazozungumza kiarabu limekuwa kubwa sana. Ikumbukwe nchi hizi kila baada ya muda fulani hufanya uchaguzi unaoitwa wa haki na huru.
Nisichoelewa ni kuwa wanaopiga kura ni kina nani na wanaoandamana ni kina nani? Maana kama wananchi wanapewa fursa ya kupiga kura kwani nini wasitumie sanduku la kura kuondosha utawala wasioutaka na badala yake wanatumia nguvu ya uma?
Mojawapo ya mambo ambayo yanagharimu pesa nyingi nchi zinazoendea ni gharama za kuitisha chaguzi. Sasa kama uchaguzi unaitishwa viongozi wanapatikana lakini raia wanaandamana kuukataa uongozi, ni kina nani waliopiga kura? Jee wanaosimamia chaguzi hizi wanahesabu kura za wananchi au wanakuwa na majibu yao wanayotaka?
Kama uchaguzi hauwezi kutoa viongozi bora, ni wakati muafaka kwa nchi zinazoendelea kubuni njia mbadala ya kupata viongozi badala ya kutumia pesa nyingi kuendesha chaguzi ambazo matokeo yake hayatawakilisha utashi wa wapiga kura.