Wananchi wana Imani na sanduku la Kura. Maneno ya Lissu ni 'blaablaa' na hofu ya kushindwa anatafuta 'exit plan' tu

Tafakari yetu

JF-Expert Member
Apr 19, 2021
1,502
4,408
Namsikia sikia aliyekuwa mgombea Urais 2020 kupitia CHADEMA Tundu Lissu akijisulubu nafsi yake kwa dhana ya kufikirika tu kwamba hakuna hata kiongozi hata mmoja aliyeshinda.

Anayesema haya atambue kwamba:

Siku ya kupiga kura 2020 niliona misululu mirefu sana ya watu wakisubiri zamu zao kupiga kura wakawapigie wagombea wao. Hakuna aliyesimama kwenye foleni hizo ndefu akiwa na uso uliosawajika kwa huzuni wala hofu ya kura kuibiwa. Wananchi walijawa na tumaini kubwa sana kwa zoezi zima la upigaji kura.

Hata kama Kura ni Siri ya mtu lakini Siri hiyo ni kama inajulikana mapema kwa wapigakura kuliko wapigiwa Kura.

Madai ya Lissu yangekuwa yana ukweli wa walau asilimia 1 basi leo tungekuwa na historia ya kukumbuka maumivu ya chaguzi kuu au mathalani uchaguzi mkuu wa 2020 maana fujo zingetokea.

Kitendo Cha Wananchi kujitokeza kwa wingi, kupiga kura ,kurudi makwao na kusubiri matokeo na kukubaliana na matokeo kina maana kubwa kwa wapigakura na hakijakipa nafasi 'blaablaa ' za Lissu kushinda ukweli.

Hata kama watanzania hawana asili ya migomo na maandamano lakini penye dhuluma na kutotendewa haki hawawezi kukaa kimya. Hivyo hiki pia ni kielelezo cha kuonesha Lissu anasumbuliwa na hofu ya kushindwa , kama kungekuwa na ukweli basi angepiganiwa lakini ni Nani wa kumpigania huku ukweli ukijieleza kuwa hakushinda?

Mwisho wa yote, hofu ya kushindwa na kutokukubalika ikikutawala inaleta athari za muda mrefu sana kwenye ubongo na nafikiri tayari Lissu ameanza kuathiriwa na Jambo hilo au pengine anatumia hiyo kama 'exit plan' ya kushindana na Jambo hilo.

Nitamuelewa na kukubaliana na Lissu kwa baadhi ya mambo lakini yote yanayohusu chama chake kukishinda Chama Cha Mapinduzi kwenye nafasi zote za ugombea nitapingana nayo kwa sababu mengi yameegemea kwenye dhana zisizoweza kuthibitika.

Ni muda sasa wa Lissu kupunguza uzito nafsini mwake juu ya ushindi wa kufikirika na ajielekeze kwenye ukweli bila hivyo atakutana na ukweli huu kila mahali na kumsulubu zaidi.

Imeandaliwa na kutayarishwa na
Mzalendo wa Taifa,
Mwanamapinduzi
 
Tanzania hakuna uchaguzi, bali kuna maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura. Sasa ushindi unatokea wapi hapo?
 
Tatizo mnapima kina cha maji na miili yenu ,CCM ni sawa na kina cha maji.
 
Ccm hakina uwezo tena wa kushinda uchaguzi wowote wa halali. Na sio tu kwamba hakiwezi kushinda katika uchaguzi halali, wala hakitakaa tena kiweze kushinda kihalali. Haya matumizi ya vyombo vya dola, na tume isiyo huru ya uchaguzi sio kwa bahati mbaya, bali chama kimefikia katika hatua ambayo hakiwezi kushinda tena kuhalali.

Kina cha maji ilikuwa ni kabla ya uchaguzi wa mwaka 2005, lakini kuanzia hapo kizazi cha CCM kikawa kimeondoka. Mmeishia kunajisi chaguzi za nchi hii kwa kulazimisha kukaa madarakani kwa shuruti. Wakati ukuta boss, CCM sio chama cha kizazi hiki.
 
Namsikia sikia aliyekuwa mgombea Urais 2020 kupitia CHADEMA Tundu Lissu akijisulubu nafsi yake kwa dhana ya kufikirika tu kwamba hakuna hata kiongozi hata mmoja aliyeshinda.

Anayesema haya atambue kwamba:

Siku ya kupiga kura 2020 niliona misululu mirefu sana ya watu wakisubiri zamu zao kupiga kura wakawapigie wagombea wao. Hakuna aliyesimama kwenye foleni hizo ndefu akiwa na uso uliosawajika kwa huzuni wala hofu ya kura kuibiwa. Wananchi walijawa na tumaini kubwa sana kwa zoezi zima la upigaji kura.

Hata kama Kura ni Siri ya mtu lakini Siri hiyo ni kama inajulikana mapema kwa wapigakura kuliko wapigiwa Kura.

Madai ya Lissu yangekuwa yana ukweli wa walau asilimia 1 basi leo tungekuwa na historia ya kukumbuka maumivu ya chaguzi kuu au mathalani uchaguzi mkuu wa 2020 maana fujo zingetokea.

Kitendo Cha Wananchi kujitokeza kwa wingi, kupiga kura ,kurudi makwao na kusubiri matokeo na kukubaliana na matokeo kina maana kubwa kwa wapigakura na hakijakipa nafasi 'blaablaa ' za Lissu kushinda ukweli.

Hata kama watanzania hawana asili ya migomo na maandamano lakini penye dhuluma na kutotendewa haki hawawezi kukaa kimya. Hivyo hiki pia ni kielelezo cha kuonesha Lissu anasumbuliwa na hofu ya kushindwa , kama kungekuwa na ukweli basi angepiganiwa lakini ni Nani wa kumpigania huku ukweli ukijieleza kuwa hakushinda?

Mwisho wa yote, hofu ya kushindwa na kutokukubalika ikikutawala inaleta athari za muda mrefu sana kwenye ubongo na nafikiri tayari Lissu ameanza kuathiriwa na Jambo hilo au pengine anatumia hiyo kama 'exit plan' ya kushindana na Jambo hilo.

Nitamuelewa na kukubaliana na Lissu kwa baadhi ya mambo lakini yote yanayohusu chama chake kukishinda Chama Cha Mapinduzi kwenye nafasi zote za ugombea nitapingana nayo kwa sababu mengi yameegemea kwenye dhana zisizoweza kuthibitika.

Ni muda sasa wa Lissu kupunguza uzito nafsini mwake juu ya ushindi wa kufikirika na ajielekeze kwenye ukweli bila hivyo atakutana na ukweli huu kila mahali na kumsulubu zaidi.

Imeandaliwa na kutayarishwa na
Mzalendo wa Taifa,
Mwanamapinduzi
Hii kauli Ulifanya jamaa Akawa mungu mtu sasa ameshachimbiwa ardhi huko cattle.
 
Back
Top Bottom