Nguvu ya Punyeto na kujichua katika Ulimwengu wa Roho

Sijakubishia brother sema nawaza kwa sauti Hapa " Unawakataza watu nyeto ili wafanye Zinaa ama?
Wape njia mbadala Basi itakayo walinda wao kimwili, kijinsia, na kiroho as you said...."

Imagine una Mwanao ambae Yuko kwenye foolish age, ametawaliwa na vichocheo vya Mwili na Anabadirisha wenzi kila siku, ukiuliza why anakujibu loudly and clear Kwamba hamu ya Mwili ndo inafanya afanye hivyo, utamuombea? Utamtafutia Mchumba aolewe au aoe na umri Bado? Sio kila kitu mpaka muwe mnakaririshwa.. siajabu unajifanya mlokole Hapa Ila in real life Ni mchafu kuzidi hata mm.. Magonjwa yameshakuwa mengi, kujizuia sio Jambo la rahisi kwa ulimwengu huu unaoenda Kasi.. tunapoteza Vijana wengi Mapema kwa sababu ya watu kama nyie.. Wape Vijana njia mbadala yakujiridhisha kuliko kuwafanya wajione wenye hatia kwa kufanya kitu Cha kawaida tu Kama kujikuna au kujisaidia haja

Anajiita jina la mkuu ..ila kichwani kwake ni tope achana nae
 
Kweli Punyeto ni laana na si dhambi tu
Reference to me..
Kila nikamaliza najutia na kujiona Mtu nisiefaa kwa lolote yaan Mtupu pure mtupuu kabisa
Lakini pia kila nikifanya punyeto nikimaliza najiona kabisa nimeondosha nguvu zangu yaan nakua kama zombie zombie tu sijielewi, majuto mengi sana moyoni na hata ukiwa mbele ya watu unajihisi kama u mtupu hata kama huna aibu ila internally you feel as you are naked.
Ila ukiacha kujichua hata mwezi, kwanza kwa sisi waumini hata ukiomba kwa Mungu unaona Moyo wako una Amani na Sala yako imefika kabisa ila sasa jichue alafu uombe yaan unajiona kama unatimiza tu wajibu bila matokeo yeyote
Ukiacha kwa Mda unaona mwili unarudi safi kabisa na nguvu za mwili na rohoni unakua nazo yaan full Amani. Kujichua huwezi kua na Afya bora Daima.
Mwisho Mtu anaejichua yeyote hata mwili wake hauna Nuru,uwe na hela uwe huna hela, ule mboga saba au moja huwezi kua na nuru. Ni mtupu rohoni na mwilini hata kama utajiona una kila kitu na kweli baraka za Mungu haziwezi kua juu yako hata kama utapata kama unavyohisi ni baraka bado huwezi kudum na vikidum huwezi kua na furaha navyo yaan lazima misukosuko ikuandame.
Shukrani kaka.

We bado lena😁😁 sisi hatujutiii tukimaliza tunafurahi
 
Ushuhuda unaendelea...

Niseme wazi Mwenyezi Mungu amenipa uwezo mkubwa sana darasani. Ni kwamba katika maisha yangu masomoni, mwalimu afundishapo, anapofika mwisho wa kipindi basi nami nimemaliza, nasubiri mtihani tu!! Sisahau neno hata kidogo, hivyo katika maisha yangu ya masomo sikuwahi kusoma tuition.

Neema hii iliendelea hata kazini pia, nikiwa napendwa sana na watu wote viongozi na wafanyakazi wenzangu. Sasa kumbuka kujichua kulianza nikiwa kazini. Kadri siku zilivyozidi kusonga, nikawa napoteza mvuto kwa wenzangu, halafu moyo wa kufanya kazi ukawa unapotwa. Ghafla nikajikuta natamani tu kujichua japo mara moja kila siku, halafu baada ya hapo huishiwa nguvu za kimwili na kiroho. Mabaki kulala tu siku nzima, siwazi lolote kuhusu maisha.

Hali iliendelea hivyo hata nikiwa sisikii hamu ya kuwa na mwanamke zaidi ya kujichua. Ndipo nikaingia kwenye kutazama picha za ngono na pia kutembelea beach kila siku kutafuta wanawake wanaoongelea ili nijichue. Hayo yakawa maisha yangu rasmi.

Mungu anitokea kwa mara ya kwanza maishani

Kuna kipindi nilipata pesa nyingi tu kazini, nikaamua nianze uwekezaji ili niache kazi. Nilikuwa sipendi tena kazi yeyote maana ilininyima uhuru wa kujichua nitakapo. Ni kwamba nilisafiri kwenda nje ya nchi kikazi, nikiwa huko pamoja na mwenzangu mmoja aitwaye Maulid (jina halisi kabisa kama ni member humu atakumbuja) tukaamua siku moja kuanza kuichunguza Biblia kama yanayofundishwa ni kweli. Kisa chote ilikuwa kutaka kujua kwa nini kuna madhehebu mengi ya Kikristo wakati Biblia ni moja tu. Basi ikawa kila siku jioni husoma sura kadhaa huku tulijadiliana kulinganisha na mafundisho ya sunday schools na mainstream churches kama RC, KKKT nk. Ninayo mafundisho tele (audio) ya askofu Zachary Kakobe. Naomba kukiri wazi, hiki ni kipindi pekee maishani mwangu ambacho sitokisahau kamwe. Kwa mara ya kwanza Mingu alizungumza nami wazi wazi.

Ilikuwa katika kusoma neno, basi kila eneo ambalo huonekana lina utata hata kuwa na mitazamo tofauti, mimi hupokea mafunuo hapo hapo na kuelewa maana pasipo kuuliza mtu. Tena nikimshirikisha yeyote, hakuna aliyeweza kupinga. Mbali na hapo, ikawa usiku kila nilalapo, basi roho yangu husafiri sehemu mbalimbali na kushuhudia mambo yafanywayo na WATU NINAOWAFAHAMU KABISA. (Wakati wa usiku tulikuwa na desturi ya kusali pamoja kwenye ukumbi, pamoja na Wakristo wengine kila mtu kwa lugha yake. Wakuu, siku moja nilishangaa nanena kwa lugha, just from no where. Sikuwekewa mikono wala sikuwahi kuomba lugha mpya, hapana. Kuanzia siku hiyo, sikuwahi kupata hamu ya kujichua, ama kutoka na mwanamke tena. Hapo ndipo haswa safari zangu katika ulimwengu wa roho zilianza.

(Labda niseme tu, nimetoka katika familia ya KIKATOLIKI, fundamentalists. Baba ni former seminarian, alikwenda mpaka daraja ya ushemasi, mama alikuwa mpostulant akifukuzia usista. Mimi pia nimesoma shule ya seminari kisha Kanisa walinioenda sana wakataka niwe padre. Namkumbuka Padre Julius Tengi pale Tabora alivyokazania niende major seminari, nikasema kabisa).

Mfano siku moja nikiwa nimejilaza kitandani niko macho kabisa saa nne usiku, Roho alinichukua mpaka kwenye kikao cha wachawi, tena wawili kati yao ni wafanyakazi wenzangu (hawa tulisafiri nao kikazi kama timu moja. Mmoja tulikuwa tukilala chumba kimoja na mwingine chumba tofauti). Basi mimi nilisimama kando nikitazama kinachofanyika lakini wao hawanioni. Walikuwa wachawi wengi sana lakini nikiwatambua wazi wazi hao wawili tu. Niliamka kwa mshituko mkubwa majira ya saa kumi alfajiri, nikastuka zaidi nilipomkuta huyo jirani yangu ndio kwanza anafuta miguu apande kitandani kulala, ni kama ametoka sehemu fulani. Hata hivyo yeye alihisi kuna kitu nimeona, akaniuliza nimeona nini? Mimi nilikataa katakata keamba ni ndoto tu ambayo siikumbuki, alinishurutisha sana nikakataa. Basi niliamua kutoka nje kama nakwenda chooni, huko ndio nikaogopa zaidi kwa nilichokiona. Yule mfanyakazi mwingine alikuwa akichota maji kwenda kuoga, amevaa VILEVILE nilivyomwona kwenye kikao cha wachawi!! Haraka nilirudi ndani nikalala.

Asubuhi huyu jirani yangu alinifuata akaanza kulalamika kwamba kuna wachawi wengi hivyo hatulali vizuri. Mimi nilimwambia sijaona tatizo na ninapata usingizi vema tu. Aliendelea kunifuatilia kama siku tatu hivi, mwishowe aliniambia wazi, KUNA KITU UMEKIONA USIKU, ILA UNANIFICHA, BASI TUTAONA!!

Basi katika kipindi hicho chote, hamu ya kujichua iliisha kabisa, nikawa namtafakari Mungu tu muda wote. Hiki ni kipindi pekee nilipokuwa na amani kubwa maishani. Mungu aliweza kunionyesha matatizo mbalimbali ya wafanyakazi wenzangu, ikawa nawapigia simu kuwaeleza. Mfano, "mkeo ni mgonjwa, usimpeleke hospitali, omba tu kesho atakuwa mzima!" Na kweli ilikuwa hivyo, kilichowashangaza wengi ni mimi kujua matatizo yao binafsi na kuwaeleza hali nikiwa nje ya nchi. Ndugu zangu, Mungu amewahi kunitumia katika viwango hivyo, tena nikiwa mchanga tu katika neno.

Anguko langu

Nikiwa huko nje, kila Jumapili tulikuwa tunakusanyika Watanzania kufanya ibada ya pamoja. Basi nilishangaa aliyekuwa mchungaji wetu siku moja kuniambia kwamba Jumapili ijayo mimi ndio nitahubiri. Sikuwahi maishani mwangu kuhubiri, lakini alisisitiza sana. Basi nilijiandaa huku nikiwa na wasiwasi na hofu kubwa mno. Jumapili ikafika, nami nikadima kwenye madhabahu hali nikiwa na hofu. Kilichofuatia Mungu mwenyewe ndio anajua, kwani nilihubiri kwa zaidi ya saa moja katika uweza wa Roho Mtakatifu. Nilijikuta natiririka tu, hata mwisho wa mahubiri nusu ya Kanisa walikuwa, wakilia machozi. Baada ya ibada, walinifuata watu, kila mmoja akisema hayo mahubiri nilimkusudia yeye na anajuta sana moyoni mwake. Mimi nilibaki kushangaa tu nisijue nini kinaendelea.

Basi ghafla roho ya mchungaji ilibadilika, akanichukia sana na kuniambia wazi, sitoruhusiwa tena kusimama madhabahuni. Nami kuanzia siku hiyo nikaacha kujihudhurisha kanisani, nikawa mzito hata kudoma neno kwani nilishajawa kiburi. Kilichofuata no anguko kuu. Usiku nikiwa nimelala, siku moja niliota ndoto nikiwa natembea njiani huku mbea akinifuata kila niendako. Tena siku mbili baadaye niliota nokiwa njiani nayembea mbwa akawa ananifuata, nikijaribu kumwacha namwona nyuma yangu. Kuanzia hapo nilishikwa na hamu ya kupiga punyeto, nikajikuta nimerejea tena. Maono yangu yakazimija ghafla. Mwezi mmoja baadaye saa 10 alfajiri nikiwa usingizini ilizungumza sauti wazi wazi ikisema, "SI UMENIKATAA MIMI, BASI SAWA." Niliamka kwa mshituko mkubwa huku moyo ukienda mbio, nikaanza kulia nikisema, hapana sijakukataa Baba. Lakini huo ndio ulikuwa mwisho wa maono yangu. Hii ni kweli kabisa wakuu. Learn from me.

Umaskini na punyeto

Niliporudi Tz nikiwa na pesa za kutosha (zaidi ya m80) nilianza uwekezaji. Kwanza nilifungua mradi wa nguruwe, kisha nikanunua Isuzu Journey mbili nikazifanya daladala (Gongolamboto- Temeke), nikanunua eneo (20 acres Tundwi Songatini), nikanunua 12 acres Morogoro Masika, ekari mbili Kisarawe, nikaanza biashara ya kununua dhahabu huku nadoma masters. Wakuu, nonavyoongea nanyi hivi leo, hakuna hata kimoja kiliendelea. Mbaya zaidi, nilikaa na mkurugenzi wa Oryx Tz kuhusu kuanzisha kituo cha mafuta akanipa support kubwa mno, mimi nilitakiwa kufanya sehemu ndogo tu, haikuwezekana!! Nilikutanishwa na marketing manager wa Vodacom niwe wakala mkuu wa mpesa Tanga na Morogoro, lakini nilipotoka ofisini nikaona ni upuuzi!?

Nikisema hakuna kilichoendelea ni kwamba, kilakukicha asubuhi, naacha kwenda kwenye appointment, badala yake nafunga safari kwenda coco beach kujichua. Nitakaa huko hadi waje wanawake kuogelea ndipo nijichue. Nikawa nachukia miradi yote niliyoianzisha. Nikawa nachukia masomo, nikaamua sihitaji yote hayo. Ilikuwa usiku nikilala, ifikapo alfajiri basi napatwa na ashki ya hatari sana, hapo sina tena control ya mwili, ratiba zote zinakufa, naenda kujichua.

Basi nguruwe walizaana wakawa wengi mno, zaidi ya arobaini, lakini siku moja nilichukua uamuzi nikaenda NIKAWAGAWA BURE kwa wafugaji wengine. Nikagawa na mabanda. Daladala moja niliiuza, nyingine ilikuwa ikibadilisgwa seat cover maeneo ya mzambarauni. Basiniliiacga huko bila kuifuatilia MWAKA MZIMA. Nilipokwenda siku moja, nikaluta niliyemkabidhi alikuwa sana, akawa anauza spare ili kujitibu mpaka basi lote likaisha! Yeye pia hakupona akawa amefariki. Kwenye dhahabu ilikuwa vituko, nanunua gram 300,nikifika sokoni zinakuwa gram 200. Nilikuwa hasara kubwa nisijue imetoka wapi.

Maisha yangu yakawa ya ajabu tu, kazini wakawa wanaishi nami kwa kunivumilia tu kutokana na rekodi zangu za mwanzo. Pepo lililovaa sura yangu halikutaka maendeleo yangu, katika ulimwengu wa roho lilisimama kupinga kila jambo. Mfano nikitaka elimu, lenyewe linakwenda mbele yangu (kwa sababu ndilo mimi mwenyewe katika ulimwengu wa roho), linasema hatuhitaji elimu sisi. Nikitaka fedha, linapinga katika ulimwengu wa roho kwamba hatuhitaji fedha nyingi. Zonatosha zilizopo. Nikitaka ndoa linakataa, najikuta sina hamu ya mwanamke, hata wa kusini naye tu, yaani sisimamishi kwa mwanamke, labda kama najichua. PUNYETO NI KIFUNGO CHA UMASKINI, hata ukiona mafanikio, iko siku yatapukutika yote usijue nini kimetokea. nakusihi ndugu, ACHA KABISA KUWSIKILIZA HAWA WANAOJIGAMBA KWAMBA WANAPIGA PUNYETO NA HAKUNA MADHARA. NI MAWAKALA WA NGUVU ZA GIZA HAWA, KWELI HAIMO NDANI YAO. PUNYETO NI KUKABIDHI NAFSI YAKO IENDESHWE NA NGUVU ZA GIZA, NI AGANO LITAKALOUA MAISHA YAKO NA VIZAZI VYAKO!!

Kama mnafikiri nadangaya, tafuteni thread za wauza madini, uanzishaji vituo vya mafuta nk. Mtaona michango yangu humo, sio utani!!

Morg, Khantwe, yuzazifu, Sic March, Mgonga Like, Ismoo, extra life, wiz hov, SHIMBA YA BUYENZE

Sasa wewe ni tahira acha kufananisha punyeto na ujinga wako....sisi wengine tukijilipua ndo tunapata hamasa ya kazi
 
Sasa wewe ni tahira acha kufananisha punyeto na ujinga wako....sisi wengine tukijilipua ndo tunapata hamasa ya kazi
Kumbe unatafuta nini hapa? Huoni hiyo ni dalili mojawapo kwamba umeathiriwa kisaikolojia!!? Umeona kabisa hapa ni dampo, afu umekomaa kubaki hapo ukipinga kwaninj tuwe na dampo. Hakuna aliyekushika, isipokuwa hizo SPIRITS nilizozisemq ndio zimekupiga PINI KALI SANA. Unatumika kama kinywa cha roho wachafu ili kulinda mpango wao. Kifupi tayari umepigwa pini, tena wewe ni mfano mzuri sana
 
Mi naamini punyeto inaachika kwa maamuzi.. mimi mwenyewe naeza kaa mwezi sijafany hivyo alafu kunq siku naeza amua tu kufanya na sio kwamba sijui.. i know what am doing na nafanya.. So ni maamuz tu
Inawezakana ukapumzishwa kwa mda ( punyeto ni dhambi * Act and Intetion * ) kama ni dhambi nyuma yake kuna roho inayo influence mtu ufanye ( ina influence your mind ili kufurahisha nafsi yako huku roho yako ikihuzunika - consience ). Bandu bandu humaliza gogo, kila upigapo mpunyeto mpigo mmoja una athari kubwa sana na kuzidi kufungua mlango wa athari katika nafsi yako ja kuwa nyepesi kupata mashambulizi ( inaweza ikawa katika ndoa ( mainly ), uchumi, maisha ya kiroho binafsi ( kukwama kukua kiroho * spirit capacity * ). But kuna njia ya kuacha permanent, na kupitia Kristo Yesu ( kupitia damu yake ) urejesho na uponyaji wa nafsi yako ukafanyika na kuwa normal. Unaeza ukawa na elfu 20,000 lakini kama ungekuwa hupigi nyeto a.k.a ka mkono huenda ungekuwa na 80,000 😃😃😃.. Nilitwanga sana ka mkono enzi nipo chuo na kipindi nagombana na manzi wangu.. asila zote nilikuwa namalizia kwa ka mkono..
 
Kumbe unatafuta nini hapa? Huoni hiyo ni dalili mojawapo kwamba umeathiriwa kisaikolojia!!? Umeona kabisa hapa ni dampo, afu umekomaa kubaki hapo ukipinga kwaninj tuwe na dampo. Hakuna aliyekushika, isipokuwa hizo SPIRITS nilizozisemq ndio zimekupiga PINI KALI SANA. Unatumika kama kinywa cha roho wachafu ili kulinda mpango wao. Kifupi tayari umepigwa pini, tena wewe ni mfano mzuri sana

Kafirisiwe we huna kitu...
 
Amani kwenu wakuu. Leo tutaongelea hatari inayomkabili mpiga punyeto kiroho. Ni ukweli usiopingika kwamba asilimia kubwa ya vijana na wazazi wa kileo wamejiingiza kwa nguvu kwenye utamaduni huu mchafu na hatari. Kwa nini nasema ni hatari?

Punyeto na kujichua ni tendo la kiroho

Wengi hutazama tendo la ngono kama furaha ya kimwili, lakini tumeshaona ni tendo la kiroho linalohusisha sehemu tatu za mwanadamu:

Roho
Mwili
Nafsi


Roho ndio inayoamua kama iungane na roho nyingine ili kukamilisha uumbaji, ikikubaliana na mwenzake nafsi huungana kuwa kitu kimoja kisha mwili huungana na mwili mwingine kukamilisha tendo hilo kwa nje. Baadaye nitarlezea kwa kina kipengele hiki muhimu ili kujua uhusiano wa roho mwili na nafsi katika nguvu ya mapenzi.

Kwa hiyo tendo la ngono huamshwa rohoni, kisha KUKAMILIKA kwa Muungano wa nafsi, ndipo watu wanaona ushuhuda wa mwili kuwa watu fulani wanapendana. Mungu aliumba mtu mke na mtu mume, hao ndio wanaokamilishana. Kwamba aliumbwa mwanamume kwanza kisha akagawanywa kupata mwanamke, kwa hiyo ili huyu mtu awe kamili, ni lazima awe na opposite sex wa kumkamilisha. Nimekupa hint ujue mwanamume kumtamani mwanamume mwenzake ni tatizo la kiroho, kadhalika mwanamke pia. Nitafafanua vizuri mbeleni..

Punyeto kama Ilivyo kwa ngono haiwezi kamwe kukamilika bila kuwa na mwenza. Tendo hili linahusisha kuamsha hamu kwa kuvuta hisia (meditative stimulation) mpaka kufikia sexual experience. Ni rahisi mtu kujidhani yu peke yake, lakini ukweli ni kuwa kuna mshirika wa pili anayefanya uwezekano wa kumaliza (ejaculation/climax). Hakuna mtu anayeamua tu, ngoja nipige punyeto. Huanza kwanza hamu ambayo huuteka ufahamu na ghafla mtu hujisikia hawezi tena kuvumilia. Sasa hiyo hamu ni NGUVU YA KIROHO inayoingia mwilini, ni ulimwengu wa roho, ni pepo wachafu. Pepo hawa wabaya ndio sex partners wa wapiga punyeto!! Wao wanashughulika na nafsi ya mtu kwa kuanza na kuiteka roho, kisha wakaungana na mtu huyu katika nafsi kuwa mwili mmoja, ndipo anaanza kujichua kwa kutumia hisia tu mpaka akakojoa.

Ni kwamba, viumbe vyote vya kiroho havina nguvu ya kutenda kwenye huu ulimwengu wetu. Upo ulimwengu unaoonekana kwa macho ya nyama, ndio huu tuliopo, umeumbwa kwa ajili yetu sisi viumbe wenye mwili. Pia upo ulimwengu usioonekana kwa macho ya nyama, uliumbwa kwa ajili ya roho. Sasa ili hao viumbe wa kiroho waweze kutenda kwenye huu ulimwengu ni lazima wawe na nguvu ya miili yetu. Nje ya hapo ni bure kwao! Hapo mwanzo walikuwa wakitumia miili ya wanyama (kisa cha Hawa bustanini), lakini sasa wanatumia nguvu za wanadamu wenyewe. Namna mojawapo yenye kutoa NGUVU KUBWA ZAIDI ni kupiga punyeto na kujichua.

Nguvu ya uumbaji imo katika ngono

Zile baraka walizopewa Adam na Hawa "zaeni mkaongezeke, mkaijaze nchi, mkatawale... " ziliwekwa ndani ya nguvu ya ngono. Kwa lugha nyingine kitendo cha sex kinaachilia nguvu ya uumbaji wa kila kitu duniani. Wazungu wanasema, sexual intercourse opens portals to other dimensions. Ndio maana mke na mume wakiwa na makubaliano katika Roho, watafanya mambo makubwa katika maisha.

Sasa mpiga punyeto naye huachilia nguvu hiyo ya uumbaji, isipokuwa yeye huitoa kwa mapepo. Kumbuka nguvu hii ni sura yake yeye mwenyewe, nafsi yake halisi akawagawia mapepo. Hii ndio nguvu waitakayo ili kuweza kutekeleza mambo yao hapa duniani. Ni nguvu hii wanaitumia kama mlango wa kushuka hapa duniani na kuwavuruga wanadamu. Jiulize, katika roho hakuna pepo jije wala dume. Mapepo ni roho wachafu tu, hawazai wala kuzaliana, imekuwaje leo tunapata JINI MAHABA JIKE NA DUME? Mwanamume anapopiga punyeto, huachia nguvu ambayo ni yeye mwanamume, hivyo pepo lililopo huichukua na kuivaa nguvu hiyo hata kuwa na hali ya kiume. Ndipo huanza kuwaingilia wanawake kwa kutumia nguvu hiyo, huku likimwrka mateka mpiga punyeto huyu aendelee kulizalishia nguvu hiyo. Mwanamke anayejichua hutoa nguvu ya kike na hivyo kuligeuza pepo kuwa jike.

Gereza la kiroho

Pepo huichukua na kuiweka gerezani roho ya mtu huyu na hapo huitiisha nafsi. Kwa hiyo hakuna jambo atafanya linafanikiwa maishani mwake isipokuwa mpaka mpenzi wake huyu wa kiroho akubali. Ndipo huja hadithi za majini yanayoharibu mafanikio.

Kuhani wa Kanisa la shetani, Antonio Lavey, aliwahi kusema, kafara kubwa kabisa ya siri, wakati wa ibada ya matambiko, ni kumwaga shahawa, ni zaidi ya kumchinja mtu na kumwaga damu yake.!! Kumbe kupiga punyeto ni kujitoa kama kafara kwa mapepo na hivyo kuyapa nguvu zako!!

Ndio maana baada ya punyeto, mtu hawezi kufikiri vizuri, akili huwa kama ina ukungu, nguvu hupungua sana mwilini. Nguvu zote za kiroho huondoka, mtu anakuwa mweupe kabisa kiroho, emotional energy inatoweka, ndipo hamu ya kuwa na opposite sex inaanza kufifia.

Shahawa sio mkojo, ni DNA yako mwenyewe. Nguvu za kumiliki zimo ndani yake, sex energy, nguvu ya kuzalisha mali nk. Hizi huitwa dominion power. Ni nguvu hizi zinazochukuliwa na mapepo.

Next time tutakwenda deep... [/B]

Morg, Nature,
Maya Angelou, Africa Tanzania, dumbi, LOGARITHM, Sergei Lavrov, LOVE U JF, korino, Mshuza2, park don, Surya, big-diamond, Mwanamena, Tajiri wa Magomeni, dudupori, Bubolwa Chura, Patra31, Depal, alumn, Ed Kawiche, Sexless, The 13, Avriel, Styles
yna2, ngebo, iMind, HoneyBee, Will jr, gbmm, True Believer, Saint Anne[/i][/B][/B]
dah asante sana mkuu
 
Back
Top Bottom