Mwana wa Mungu
JF-Expert Member
- Aug 14, 2008
- 1,003
- 83
Nguvu iliyotumika kumkamata mchungaji wa DECI majuzi, iliniumiza sana, mtumishi wa Mungu, mtu anayesimamia makanisa vile, halafu akafungwa pingu wakati hajaleta upinzani wowote, wala hajatoa dalili ya kupingwa kukamatwa, ilikuwa ni ya kupindukia.
Mimi sio polisi, ninaweza nikasema kuwa, kama polisi waliona ni bora kufanya vile, basi sawa, lakini basi nguvu ileile iliyotumika pale, itumike hivyohivyo na kwa mafisadi wengine kama kina mramba na mawaziri wengine wakubwa. hao mawaaziri wengine walikamatwa kwa kusindikizwa, lakini yule mchungaji alikamatwa kwa kupigwa pingu hadharani kama jambazi.
Mchungaji yule alikuwa pale akiwapa watu mbegu zao, akawa anawatangazia matangazo. polisi wanasema alikuwa anahamasisha fujo, hivi ni fujo gani wana deci wanaweza kuileta? mimi kama mkristo, na wakristo wengine wengi tu mtaani huku, tumechukizwa sana na kitendo kile cha kumdharirisha mchungaji wetu, hata kama mimi sisali kwake, lakini kuna waumini wake wengi wameumizwa na kitendo kile. kama hakukataa kupelekwa polisi, kwanini nguvu ya ziada kama ile itumike? lini tulishasikia hata Shehe mmoja tu amepigwa pingu? mbona kuna fujo nyingi tu zinafanyika misikitini, tena kali, nyingine ni hiyo ya arusha juzi kumzuia mtu wa bakwata. na nyingine nyingi. hivi kulikuwa na umuhimu wa kumfunga pingu mchungaji wa kikristo vile? ni mioyo mingapi ya wakristo imeumia? hatutaki jambo hili lijirudie, mapolisi wawe makini, wasilete hasira zzo binafsi kumaliza machungu yao. kama walikuwa na hasira na wale wachungaji au walikuwa na hasira na wakristo, ni maadui wa wakristo nina maana, wangejiweka wazi ili tujue. ile kitendo kile, hata kama watu hawatasema hadharani kwasababu wakristo ni waoga kuandamana, selikali ijue kuwa, liko linafukuta mioyoni mwa watu. na kuna siku watawajibika, either kwa kupitia kura au kitu kingine chochote ambacho sio violent. asante.