N'golo Kante: Toka kuzoa taka mitaani hadi kuwa mchezaji bora anayetegemewa

anonymousafrica

JF-Expert Member
Aug 24, 2016
611
639
jpeg.jpg

Ng'olo Kante, alitamani kombe la dunia lichezwe nchini Ufaransa kila mwaka, kwasababu mwaka 1998, alifanikiwa kuzoa taka nyingi kuliko miaka yake yooote ya kuzoa taka mitaani.

Kante alizaliwa Machi 29, 1991, huko mjini Paris nchiniUfaransa. Wazazi wake walikuwa wahamiaji kutoka nchini Mali barani Africa. Kutokana na ugumu wa maisha nvhini humo, waliona ni bora wavuke maji waendezao Ulaya (sasa we kimbilia ulaya na kingereza hujui, Utaongea nini na wazungu wenzako?)

Walifuata nafuu ya maisha huko ulaya miaka ya 1980. Na kuishi kwenye kighorofa kidogohuko Rueil Malmaison, Eneo hili linajulikana kama mahali pa wafanyikazi wa kola ya blue ( wazee wa shurbashurba, kazi za ngungwa).

Baba alifariki na kumuacha mtoto Kante akiwa na umri mdogo, kijana ambaye alirithi kazi ya kuokota makopo na uchafu ambao unaweza kutumika au kuuzwa kwenye viwanda kwaajili ya matumizi mapya (Recycling) watu wamehustle bwana.

Kante akawa baba wa familia akiwa kijana mdogo. Ndoto yake ni kufanya kazi kwa bidii ili kuikomboa familia yake kutoka kwenye njaa.
Maisha ya familia masikini yalimfanya Kante awe tayari kufanya kazi zaidi ya kutazama mpira , japo aliupenda. Alipata bahati ya kuangalia mpira sehemu zenye baa au mgahawa pale akiwa kwenye shughuli zake za kuokota uchafu (scavenger)

Wenzetu wana academy za kufundisha mpira (kwa watoto/vijana) ye wakati huo alikua busy kutafta hela.

Ningekua naandikia story masela basi ningetukana kidogo tusi letu maarufu lile, ila tuendelee.

Alianza kuupenda zaidi mpira wakati wa kombe la dunia mwaka 1998, alishangazwa na kikosi cha ufaransa kikiwa na wahamiaji wa kutosha kama Zinedine Zidane, Lilian Thuram, Patric Vieira, na Nicolas Anelka. Kupitia ushiriki wao, Ufaransa iliweza kushinda taji la Bingwa wa Dunia.

Kwenye kombe la dunia Kumbuka wakati wao wanajenga historia ya ushindi, mwaka huo Kante alijenga historia ya kuzoa taka nyingi na kuokota mabaki kutoka kwa wageni waliokwenda ufaransa kwaajili ya kombe hilo.

Alijiunga na JS Suresnes huko magharibi mwa Paris. Baada ya kuingia kwenye chuo hicho, Kante alikua mchezaji maarufu katika timu. Lakini wengi walitilia shaka uwezo wake kwasababu ya umbo na kimo. Walijiuliza hivi haka kajamaa kataweza kumaliza dakika 90?.
Alionyesha maajabu na wakasema alaaah kijana yupo vizuri.

Akiwa academy alitumia muda wake pia kuwafundisha mpira wachezaji wadogo na kujipatia fedha kidogo na kwa msaada wa Pierre Ville ambaye alikuwa msimamizi wakati huo alikua mtu muhimu kumfanya Kante kuwa mchezaji mzuri.
kuanzia hapo, Kante alianza kupata pesa.

Kante alijiunga na Boulogne. Alifanikiwa kumshangaza kocha wa Boulogne, Durand. Akapita hapa na pale mpaka alipoajiunga na moja ya timu za England, Leicester City mnamo 2015.

Kama ilivyo ndoto ya wachezaji wengi kutamani kucheza Uingereza, Leicester City ikawa moja ya ndoto zilizofanikiwa za N'Golo Kante. Alionyesha kiwango na kuipatia Leicester City taji nayeye kutajwa kama mchezaji bora kwenye ligi kuu.

Leicester City ikampeleka Kante Stamford Bridge. Na mungu akamuinua na kuwa kiungo anayejulikana zaidi.

Licha ya mshahara wake mzuri baada ya kujiunga na Chelsea, Kante hajawahi kubadili tabia yake ya upole na unyenyekevu.

Dunia ikamtambua na watu wakaona shughuli yake.kwenye kombe la dunia, Walipeleka kombe ufaransa dhidi ya Croatia.

Alikua mchezaji wa mwisho kupiga picture na kombe, walipomwambia em njoo upige picha.

KASEMA. MHH NAONA AIBU AISEE HILI KOMBE LINANG’AA SANA ALAFU LITAKUA ZITO

hi-res-d46f06d287222dcb1cab83bdd7af6cc1_crop_north.jpg
 
umesahau hajawahi kubadirisha gari alilopewa kama zawadi aina ya min cooper na shabak mmoja , na bado analitumia kama kumbukumbu ya wema aliofanyiwa na shabiki ...

alinishawishi sana kuipenda min cooper ,
kakaaa hadi hilo niandike?
siwezi kuandika vyote.. na suala hilo limezungumzwa sana
najitahidi kuandika vitu hadim

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hiyo kuwa mchehzaji bora anaetegemewa sijaona maelezo yake.
Acheni ku overrate mambo wabongo
 
Back
Top Bottom