Mchezaji Sankara Karamoko aamua kuachana na Yanga na kwenda kucheza Ulaya

Imeloa

JF-Expert Member
Jan 28, 2013
12,917
15,347
Mshambuliaji nyota wa klabu ya Asec Mimosa ya Cote D'Ivoire Sankara Karamoko, ameamua kwenda kucheza mpira wa kulipwa nchini Austria na kuachana na timu ya Young Africans ya Tanzania.

====

Mshambuliaji aliyekuwa akiwindwa na Yanga, Sankara Karamoko amekamilisha uhamisho wa kutua katika Klabu ya Wolfsberger AC ya Austria baada ya kudumu ndani ya Asec Mimosas kwa miaka mitano.

Karamoko (20), ambaye alijiunga na Asec mwaka 2019 akianzia timu ya vijana amekamilisha uhamisho huo baada ya timu hiyo kukubaliana na Wolfsberger AC inayoshiriki Ligi Kuu Astria maarufu kama Ausrian Bundesliga.

Katika msimu huu akiwa na Asec, Karamoko amefanikiwa kuwa kinara wa mabao kwa timu kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika akikofunga mabao manne.

Wolfsberger AC iko katika nafasi ya saba kwenye msimamo wa ligi nchini humo ambapo Asec imeeleza kwamba mshambuliaji huyo ameuzwa kwa dau lisiloweza kuwekwa wazi.

Karamoko anakwenda kuungana na mshambuliaji mwenzake wa zamani wa Asec, Karim Konate ambaye naye aliuzwa msimu uliopita kwa klabu ya Redbull Salzburg.

Tayari mshambuliaji huyo ameondoka nchini Ivory Coast akielekea Ausrtia kukamilisha dili hilo ambapo endapo atafuzu vipimo vya afya atasaini mkataba utakaomfanya aishi huo hadi 2027.

Yanga iliweka mitego yake ili kumnasa mchezaji huyo wakati wa dirisha dogo la usajili lililofungwa Januari 15, lakini ilishindikana katika ishu ya makubaliano kwa kilichodaiwa kwamba timu yake ilikuwa na mpango wa kumuuza Ulaya.

Mwanaspoti
 
Mshambuliaji nyota wa klabu ya Asec Mimosa ya Cote D'Ivoire Sankara Karamoko, ameamua kwenda kucheza mpira wa kulipwa nchini Austria na kuachana na timu ya Young Africans ya Tanzania.

Ulitaka awe kama Chasambi!!
 
Japo nipo nje ya mada Mimi naamini kabisa viwango vya wachezaji wa africa magharibi vinafanana tu na sisi huku ila wenzetu wametuzidi connection tu ndio maana akicheza kidogo tu africa huyo unasikia tu yupo ulaya...fikiria mchezaji kama feisali,ibrahim baka,aishi manula,kibu denis,Dickson job,kapombe,mzamiru,kuna dogo mmoja akiitwa rashidi juma nk hawa ni wachezaji ambao wamekosa connection tu tangu wapo vijana ila laiti wangekuwa wamezaliwa africa magharibi japo sio wote niliowataja ila nadhani nusu yao wangekuwa ulaya
 
mtoe mzamiru hapo . pia wachezaji wetu hawana muendelezo mzuri
 
Japo nipo nje ya mada Mimi naamini kabisa viwango vya wachezaji wa africa magharibi vinafanana tu na sisi huku ila wenzetu wametuzidi connection tu ndio maana akicheza kidogo tu africa huyo unasikia tu yupo ulaya...fikiria mchezaji kama feisali,ibrahim baka,aishi manula,kibu denis,Dickson job,kapombe,mzamiru,kuna dogo mmoja akiitwa rashidi juma nk hawa ni wachezaji ambao wamekosa connection tu tangu wapo vijana ila laiti wangekuwa wamezaliwa africa magharibi japo sio wote niliowataja ila nadhani nusu yao wangekuwa ulaya
Mtoe Kibu hapo
 
Naunga mkono hoja
 
Sio suala la connection tu hao wachezaji hata wakipata hizo fursa huwa hawataki kwenda na hata wa akienda hachukui round lazima warudi bongo! Coz hawana moyo wa upambanaji

Rejea farid musa, shiza kichuya, yahya zaid, shabani chilunda adam adam

Hata zamani wakina edibily walipata fursa za kwenda kucheza nje wakazichezea

Kwa kifupi wabongo roho ya upambanaji hatuna na tunaridhika na vitu vidogo sana.

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Mshambuliaji aliyekuwa akiwindwa na Yanga, Sankara Karamoko amekamilisha uhamisho wa kutua katika Klabu ya Wolfsberger AC ya Austria

Heading yako ilipaswa kua hivi
 
Sio suala la connection tu hao wachezaji hata wakipata hizo fursa huwa hawataki kwenda na hata wa akienda hachukui round lazima warudi bongo! Coz hawana moyo wa upambanaji

Rejea farid musa, shiza kichuya, yahya zaid, shabani chilunda adam adam

Hata zamani wakina edibily walipata fursa za kwenda kucheza nje wakazichezea

Kwa kifupi wabongo roho ya upambanaji hatuna na tunaridhika na vitu vidogo sana.

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
Mkuu umemaliza.
 
Rejea farid musa, shiza kichuya, yahya zaid, shabani chilunda adam adam
Ushawahi kukutana na issue ya ubaguzi? Katika wote hao atleast Farid Musa alikazakaza ila naye alikua anabaguliwa sana. Anakwambia mazoezi anafanya vizuri tu na anasifiwa ila kwenye mechi hapangwi.

Ofcourse hatuwei kataa hata wa mataifa mengine pua wanakutana na ubaguzi ila imagine katika group la watu 50+ wewe peke yako unazungumza kiswahili na Kiingereza hujui. Wachezaji wa west nao lugha inawabeba hasa English & French
 
Ndyo maana nikwakwambia wachezaji wetu hawana moyo wa upambanaji yaani kubaguliwa kidogo tu unataka urudi home

Kuna mchezaji mmoja wa ghana anaitwa kingstone huyu jamaa alipata timu urusi kipindi hicho urusi inasifika kwa ubaguzi kwa ubaguzi jamaa anakwambia akiwa anacheza uwanjani alikuwa anazomewa na mashabiki wa timu pinzani na mashabiki wa timu yake lakini alikomaa nao mwisho wa siku mpaka mashabiki wa timu yake akawa kipenzi chao mpaka wakawa wanapigana na mashabiki wa timu pinzani wakimbagua.

Na hii ndio definition ya moyo wa upambanaji waliyonayo wenzetu wa afrika magharibi ndio maana wakipata fursa huwa hawaleti visingizio

Wewe hujakutana na ubaguzi bado. Ni bora huyo Kingstone anabaguliwa na mashabiki. Sasa yeye Farid ndani ya timu kumejaa ubaguzi hapo unatokaje? Though kiukweli siwezi nikakupinga waliowengi hawana moyo wa kupambana
 
Ndyo maana nikwakwambia wachezaji wetu hawana moyo wa upambanaji yaani kubaguliwa kidogo tu unataka urudi home

Kuna mchezaji mmoja wa ghana anaitwa kingstone huyu jamaa alipata timu urusi kipindi hicho urusi inasifika kwa ubaguzi kwa ubaguzi jamaa anakwambia akiwa anacheza uwanjani alikuwa anazomewa na mashabiki wa timu pinzani na mashabiki wa timu yake lakini alikomaa nao mwisho wa siku mpaka mashabiki wa timu yake akawa kipenzi chao mpaka wakawa wanapigana na mashabiki wa timu pinzani wakimbagua.

Na hii ndio definition ya moyo wa upambanaji waliyonayo wenzetu wa afrika magharibi ndio maana wakipata fursa huwa hawaleti visingizio

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
wa west wale ni watu wengine kabisa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom