Hivi kumbe hata kwenye kuzoa taka kuna utapeli, ndio maana jiji uchafu unaongezeka badala ya kupungua. Kwa utaalam wangu wa Operations Management kazi ya kuzoa taka kwa jiji kama Dar hailipi kabisa kwa kuwa utatakiwa kuinvest sana kwenye magari ya kuzolea taka due to foleni. Gari moja linaweza kishia trip mbili tu kwa siku na pia watz hatuna utamaduni wa usafi tunatupa taka hovyo
Kama hailipi unafikiri wakubwa, wazito hawa wanafanya hizi kazi kwa nini? kufurahisha wahisani au wanamazingira? hii inaweza kua inalipiwa na serikali kuu moja kwa moja kama katika harakati za kutunza mazingira huku kukiwa na mchakato wa wahisani...kuna mambo mengi sana ndugu yangu, hivi unajua uwa kuna hela zinatolewa na wahisani kupunguza umaskini jijini Dar? sasa zinaenda wapi jiuzlize