NgomaNzito
JF-Expert Member
- Jan 10, 2008
- 559
- 26
du huku mtaani kwetu vijibweni umeme ni mwingi tena wa ziada tunao lakini umekatika toka asubuhi hahaa ndio maana ngeleja nakupenda
Mkuu mnafiki sio tusi, ni mtu anayezungumza asiyotarenda au asiyoyaamini, na ni kweli tumeyaona sana kwa baadhi ya wanasiasa wetu hasa wa upinzani. Mnyika anataka kutumia hali kukatika kwa umeme kama chance ya kurejesha imani aliyoipoteza pale UBUNGO.
We choko kweli!upeo wakufikiri umeishia apo?Nyie Waandishi, tumeshawaomba muache kuandika taarabu, tumechoshwa na habari za kishenzi kila siku na si habari za kuleta maendeleo. Sasa hii ni maana gani ya kutuletea malumbano ya Ngeleja na Mnyika hapa?? Hapa ni JF hatutaki umbeaumbea na habari ndefuuuuuu lakini ukimaliza kuisoma inaishia hapohapo. Porojo tupu Tanzania. Mnatuchosha hembu badilikeni na wapuuzeni hao, wakiona hawaandikwi wataacha wenyewe kuropoka na kuanza kufanya kazi.
Umeme unaozalishwa kwa sasa ni zaidi ya 1200 MW mahitaji ni 850 MW, tuna ziada ya umeme kwa sasa.
Hongera JMK.
Ngeleja usituone sisi watoto,wewe ndio wakupuzwa.mkigoma kujiuzulu tuta taka r-o-o zenu siku moja,kama naibu wako ana smg na bastola,wewe siunayo rpg na ak47,na iyo yote niuogatu mjua fika kua wavuja jasho wamechoka.
Nimekuwa nikimfuatilia Mheshimiwa Mnyika ktk hotuba,taarifa namaelezo yake hata siku moja sijawahi kumsikia akitumia maneno mabovu,lugha chafu,kwanini Ninyi viongozi wa CCM Mnapenda kutumia Maneno machafu nimemsikia Mkapa,Wassira,na Juzi kupitia Mtandao nimemsikia Lusinde akitukana Hadharani na kutishia Kumuua Dr Slaa akikutana nae wapi mnakotupeleka huko Jazba zinatoka wapi mnawafundisha nini vijana na watoto ambao ni taifa la kesho.Mheshimiwa J.Kikwete. ni kweli siasa ni Matusi Majukwaani ?, tunajenga taifa la namna gani,leo Waziri,Mbunge huyu anamwita mwenzie Mjinga mnajua dhamana mlionayo mbele ya jamii.hivi kweli viongozi kama Lusinde.hawa ndio Kioo cha Jamii namkumbuka hata Tambwe Hiza alikuwa mlopokaji lakini hakufikia hapa ambapo Lusinde amefikia.Chama cha Mapinduzi ni chama chenye Historia Ndefu pana,iliyotukuka si Tanzania tu bali Afrika ,ni chama kilichopigania harakati za Uhuru wa nchi nyingi,kinaheshima zake basi chagueni watu wanaolingana na heshima hiyo.MUNGU IBARIKI TANZANIAUmeme umekatika sasa hivi! Na haukuwapo toka jana! Umewaka nusu saa tu! Shkamoo ngeleja!
Haya wadau upande mwingine wa shilingi!
WAZIRI wa Nishati na Madini, William Ngeleja amemtaka Mbunge wa Ubungo, John Mnyika (Chadema), asitumie kigezo cha kukatikakatika kwa umeme katika baadhi ya maeneo ya Jiji la Dar es Salaam kunakosababishwa na hitilafu za kiufundi, kuwapotosha wananchi.
Amesema huo ni unafiki na kuwataka wananchi wampuuze Mbunge huyo kwa sababu utekelezaji wa miradi ya umeme unafahamika na tayari mipango hiyo imezaa matunda kwa kuwepo kwa umeme wa ziada nchini.
Ngeleja ametoa kauli hiyo ofisini kwake Mtaa wa Samora, Dar es Salaam leo ambako pamoja na mambo mengine, amezungumzia kauli aliyoitoa Mnyika jana akisema umefika wakati wa kufanya mabadiliko makubwa ya kimuundo na kiuongozi katika Wizara hiyo kwa kushindwa kuhimili mahitaji ya sasa.
Nashangazwa na ukimya wa Serikali kuhusu utekelezaji wa mpango wa dharura wa umeme na maendeleo ya sekta ya nishati ambayo hivi sasa inakabiliwa na changamoto nyingi, Mnyika alikaririwa akisema juzi.
Lakini Waziri Ngeleja alimshangaa Mbunge huyo ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kutokuwa na taarifa ya utekelezaji wa mpango huo wakati ilitolewa bungeni na amekuwa akishiriki vikao vya Kamati yake hiyo.
Si kweli kuwa tumeshindwa kuhimili mahitaji ya sasa, nakubali zipo changamoto, lakini Serikali imechukua hatua kadhaa tangu ulipotolewa Mpango wa dharura bungeni Agosti mwaka jana. Namshangaa Mheshimiwa Mnyika kwa sababu ni mbunge na Mjumbe wa Kamati ya Nishati na Madini, anayajua haya. Huu ni unafiki mkubwa na wananchi wanapaswa kumpuuza, amesema Ngeleja.
Akizungumzia sekta ya madini, amesema mafanikio ni pamoja na kutungwa kwa Sera ya Madini (2009) na Sheria ya Madini (2010) ambavyo zimeimarisha usimamizi wa sekta hiyo; kutokana na sheria hiyo sasa Serikali inamiliki hisa katika migodi ya uchimbaji ikiwamo Buckreef Serikali ina hisa asilimia 45 kupitia Stamico; Mchuchuma na Liganga ina hisa asilimia 20 kupitia NDC na Ngaka ina hisa asilimia 30 pia kupitia NDC.
Amesema pia migodi mikubwa inatakiwa kujisajili katika masoko ya hisa na kwa kuanzia, tayari Kampuni ya Barrick imeshaanza kusajili hisa zake, wakati huo huo Mgodi wa Dhahabu wa Geita, Resolute, Tulawaka na TanzaniteOne, imeshalipa kodi ya mapato serikalini ya asilimia 30.
Kuhusu madini ya urani, ameeleza kuwa, Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini pamoja na Wizara ya Maliasili na Utalii wanaendelea na mchakato wa kupata kibali kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kwa mujibu wa Itifaki ya Kimataifa na itaendelea kutoa taarifa kwa kadri mchakato unavyoendelea.
HabariLeo | Ngeleja- Mnyika mnafiki, anapotosha wananchi
Naona sera za CCM siku hizi ni matusi tu na kuita watu wanafiki. Wameshindwa kujibu hoja.
Nimekuwa nikimfuatilia Mheshimiwa Mnyika ktk hotuba,taarifa namaelezo yake hata siku moja sijawahi kumsikia akitumia maneno mabovu,lugha chafu,kwanini Ninyi viongozi wa CCM Mnapenda kutumia Maneno machafu nimemsikia Mkapa,Wassira,na Juzi kupitia Mtandao nimemsikia Lusinde akitukana Hadharani na kutishia Kumuua Dr Slaa akikutana nae wapi mnakotupeleka huko Jazba zinatoka wapi mnawafundisha nini vijana na watoto ambao ni taifa la kesho.Mheshimiwa J.Kikwete. ni kweli siasa ni Matusi Majukwaani ?, tunajenga taifa la namna gani,leo Waziri,Mbunge huyu anamwita mwenzie Mjinga mnajua dhamana mlionayo mbele ya jamii.hivi kweli viongozi kama Lusinde.hawa ndio Kioo cha Jamii namkumbuka hata Tambwe Hiza alikuwa mlopokaji lakini hakufikia hapa ambapo Lusinde amefikia.Chama cha Mapinduzi ni chama chenye Historia Ndefu pana,iliyotukuka si Tanzania tu bali Afrika ,ni chama kilichopigania harakati za Uhuru wa nchi nyingi,kinaheshima zake basi chagueni watu wanaolingana na heshima hiyo.MUNGU IBARIKI TANZANIA
Mkuu mnafiki sio tusi, ni mtu anayezungumza asiyotarenda au asiyoyaamini, na ni kweli tumeyaona sana kwa baadhi ya wanasiasa wetu hasa wa upinzani. Mnyika anataka kutumia hali kukatika kwa umeme kama chance ya kurejesha imani aliyoipoteza pale UBUNGO.