Ngeleja: Mnyika mnafiki, anapotosha wananchi

du huku mtaani kwetu vijibweni umeme ni mwingi tena wa ziada tunao lakini umekatika toka asubuhi hahaa ndio maana ngeleja nakupenda
 
Mkuu mnafiki sio tusi, ni mtu anayezungumza asiyotarenda au asiyoyaamini, na ni kweli tumeyaona sana kwa baadhi ya wanasiasa wetu hasa wa upinzani. Mnyika anataka kutumia hali kukatika kwa umeme kama chance ya kurejesha imani aliyoipoteza pale UBUNGO.

Mkuu, bado tuna imani ns Mnyika.. Ila hatuna imani na Ngeleja. Umeme umekatika
toka saa 1:30 kurudi saa 6 kama juzi.. Sasa nani muongo/ mnafiki???
 
Nyie Waandishi, tumeshawaomba muache kuandika taarabu, tumechoshwa na habari za kishenzi kila siku na si habari za kuleta maendeleo. Sasa hii ni maana gani ya kutuletea malumbano ya Ngeleja na Mnyika hapa?? Hapa ni JF hatutaki umbeaumbea na habari ndefuuuuuu lakini ukimaliza kuisoma inaishia hapohapo. Porojo tupu Tanzania. Mnatuchosha hembu badilikeni na wapuuzeni hao, wakiona hawaandikwi wataacha wenyewe kuropoka na kuanza kufanya kazi.
We choko kweli!upeo wakufikiri umeishia apo?
 
Ngeleja usituone sisi watoto,wewe ndio wakupuzwa.mkigoma kujiuzulu tuta taka r-o-o zenu siku moja,kama naibu wako ana smg na bastola,wewe siunayo rpg na ak47,na iyo yote niuogatu mjua fika kua wavuja jasho wamechoka.
 
Umeme wa Ziada halafu Unakatika katika? Ha ha ha Ngeleja Bana! Wananchi tunataka Umeme hizo nyingine ni POROJO TU
 
Umeme unaozalishwa kwa sasa ni zaidi ya 1200 MW mahitaji ni 850 MW, tuna ziada ya umeme kwa sasa.

Hongera JMK.

uongo mwingine bwana, hata haufai. hivi ukiwa na ziada ya umeme ndo umeme unakatika ovyo? ndo kamati ya bunge ya nishati watahadharishe? akili nyingine bora hata tope la kirua vunjo
 
Ngeleja usituone sisi watoto,wewe ndio wakupuzwa.mkigoma kujiuzulu tuta taka r-o-o zenu siku moja,kama naibu wako ana smg na bastola,wewe siunayo rpg na ak47,na iyo yote niuogatu mjua fika kua wavuja jasho wamechoka.

wako kipiganaji zaidi, kiburi chote hicho ni kwa kuwa wanamiliki siraha za kisasa. hivi huyu malima DCI kamchukulia hatua gani? hajafikishwa mahakaman kwa kosa la kumiliki SNG kinyume na sheria?
 
namshangaa Ngeleja jana g.mboto umeme ulikatika asubuh ukarud jion, leo alfajiri umekatika tena huo tena sio mgao? Au miundombinu. Acheni kujinadi kwenye vyombo vya habari na data za kuandika. Umeme ungekuwepo kweli tungeuona unafki wa mnyika. Lakini umeme hakuna.
 
Umeme umekatika sasa hivi! Na haukuwapo toka jana! Umewaka nusu saa tu! Shkamoo ngeleja!
Nimekuwa nikimfuatilia Mheshimiwa Mnyika ktk hotuba,taarifa namaelezo yake hata siku moja sijawahi kumsikia akitumia maneno mabovu,lugha chafu,kwanini Ninyi viongozi wa CCM Mnapenda kutumia Maneno machafu nimemsikia Mkapa,Wassira,na Juzi kupitia Mtandao nimemsikia Lusinde akitukana Hadharani na kutishia Kumuua Dr Slaa akikutana nae wapi mnakotupeleka huko Jazba zinatoka wapi mnawafundisha nini vijana na watoto ambao ni taifa la kesho.Mheshimiwa J.Kikwete. ni kweli siasa ni Matusi Majukwaani ?, tunajenga taifa la namna gani,leo Waziri,Mbunge huyu anamwita mwenzie Mjinga mnajua dhamana mlionayo mbele ya jamii.hivi kweli viongozi kama Lusinde.hawa ndio Kioo cha Jamii namkumbuka hata Tambwe Hiza alikuwa mlopokaji lakini hakufikia hapa ambapo Lusinde amefikia.Chama cha Mapinduzi ni chama chenye Historia Ndefu pana,iliyotukuka si Tanzania tu bali Afrika ,ni chama kilichopigania harakati za Uhuru wa nchi nyingi,kinaheshima zake basi chagueni watu wanaolingana na heshima hiyo.MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
Haya wadau upande mwingine wa shilingi!

WAZIRI wa Nishati na Madini, William Ngeleja amemtaka Mbunge wa Ubungo, John Mnyika (Chadema), asitumie kigezo cha kukatikakatika kwa umeme katika baadhi ya maeneo ya Jiji la Dar es Salaam kunakosababishwa na hitilafu za kiufundi, kuwapotosha wananchi.

Amesema huo ni unafiki na kuwataka wananchi wampuuze Mbunge huyo kwa sababu utekelezaji wa miradi ya umeme unafahamika na tayari mipango hiyo imezaa matunda kwa kuwepo kwa umeme wa ziada nchini.

Ngeleja ametoa kauli hiyo ofisini kwake Mtaa wa Samora, Dar es Salaam leo ambako pamoja na mambo mengine, amezungumzia kauli aliyoitoa Mnyika jana akisema umefika wakati wa kufanya mabadiliko makubwa ya kimuundo na kiuongozi katika Wizara hiyo kwa kushindwa kuhimili mahitaji ya sasa.

“Nashangazwa na ukimya wa Serikali kuhusu utekelezaji wa mpango wa dharura wa umeme na maendeleo ya sekta ya nishati ambayo hivi sasa inakabiliwa na changamoto nyingi,” Mnyika alikaririwa akisema juzi.

Lakini Waziri Ngeleja alimshangaa Mbunge huyo ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kutokuwa na taarifa ya utekelezaji wa mpango huo wakati ilitolewa bungeni na amekuwa akishiriki vikao vya Kamati yake hiyo.

“Si kweli kuwa tumeshindwa kuhimili mahitaji ya sasa, nakubali zipo changamoto, lakini Serikali imechukua hatua kadhaa tangu ulipotolewa Mpango wa dharura bungeni Agosti mwaka jana. Namshangaa Mheshimiwa Mnyika kwa sababu ni mbunge na Mjumbe wa Kamati ya Nishati na Madini, anayajua haya. Huu ni unafiki mkubwa na wananchi wanapaswa kumpuuza,” amesema Ngeleja.

Akizungumzia sekta ya madini, amesema mafanikio ni pamoja na kutungwa kwa Sera ya Madini (2009) na Sheria ya Madini (2010) ambavyo zimeimarisha usimamizi wa sekta hiyo; kutokana na sheria hiyo sasa Serikali inamiliki hisa katika migodi ya uchimbaji ikiwamo Buckreef Serikali ina hisa asilimia 45 kupitia Stamico; Mchuchuma na Liganga ina hisa asilimia 20 kupitia NDC na Ngaka ina hisa asilimia 30 pia kupitia NDC.

Amesema pia migodi mikubwa inatakiwa kujisajili katika masoko ya hisa na kwa kuanzia, tayari Kampuni ya Barrick imeshaanza kusajili hisa zake, wakati huo huo Mgodi wa Dhahabu wa Geita, Resolute, Tulawaka na TanzaniteOne, imeshalipa kodi ya mapato serikalini ya asilimia 30.

Kuhusu madini ya urani, ameeleza kuwa, Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini pamoja na Wizara ya Maliasili na Utalii wanaendelea na mchakato wa kupata kibali kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kwa mujibu wa Itifaki ya Kimataifa na itaendelea kutoa taarifa kwa kadri mchakato unavyoendelea.


HabariLeo | Ngeleja- Mnyika mnafiki, anapotosha wananchi

Hapo mnafiki ni yupi? Maana ngeleja anachoongelia kinaishia kuwa maneno tu na siyo vitendo kama inavyotakiwa na wanaposahihishwa wanakuja na maneno mengi zaidi badala ya kuja kwa vitendo
 
Nimekuwa nikimfuatilia Mheshimiwa Mnyika ktk hotuba,taarifa namaelezo yake hata siku moja sijawahi kumsikia akitumia maneno mabovu,lugha chafu,kwanini Ninyi viongozi wa CCM Mnapenda kutumia Maneno machafu nimemsikia Mkapa,Wassira,na Juzi kupitia Mtandao nimemsikia Lusinde akitukana Hadharani na kutishia Kumuua Dr Slaa akikutana nae wapi mnakotupeleka huko Jazba zinatoka wapi mnawafundisha nini vijana na watoto ambao ni taifa la kesho.Mheshimiwa J.Kikwete. ni kweli siasa ni Matusi Majukwaani ?, tunajenga taifa la namna gani,leo Waziri,Mbunge huyu anamwita mwenzie Mjinga mnajua dhamana mlionayo mbele ya jamii.hivi kweli viongozi kama Lusinde.hawa ndio Kioo cha Jamii namkumbuka hata Tambwe Hiza alikuwa mlopokaji lakini hakufikia hapa ambapo Lusinde amefikia.Chama cha Mapinduzi ni chama chenye Historia Ndefu pana,iliyotukuka si Tanzania tu bali Afrika ,ni chama kilichopigania harakati za Uhuru wa nchi nyingi,kinaheshima zake basi chagueni watu wanaolingana na heshima hiyo.MUNGU IBARIKI TANZANIA

Chama cha mapinduzi kilichokua kimetukuka ni kile cha mwalimu Nyerere,sio hiki cha sasa!kumebaki uhuni na utapeli tu
 
Sisi hatutaki maneno mengi na dhihaka bali tunataka UMEME. Kama wameshindwa kutimiza majukumu yao basi wawajibishwe
 
Siasa na uongo mtupu...wiki nzima hii ya mwisho wa march 2012 tanesco na serikali watumia vyombo vya habari ati hakuna mgao !!! ukweli upo wazi ni kwamba mfano maeneo ya Tabata kila siku hakuna umeme...maeneo ya mjini sehemu za HinduMandhal Hospital kila siku hatupati umeme kwa masaa kadhaa...kwa uchache hatupati umeme kati ya masaa 4 mpaka 8 kwa siku...eneo lote la katika kati ya mjini...
oungo haufai umeme hakuna na ni mgao kwani hapa eneo la mjini unawashwa kwa awamu hii ni mgao..Tanesco waache kupiga porojo..waje na data..sio uongo na siasa...hali hii ndio maana shirika haliendelei..nchi inadorora...bila ya umeme tusidanganyane...ati uchumi unakua!!!
maeneo ya upanga kila siku tunakatiwa umeme....jumapili na jumamosi ndio tumesahau kabisa ....na umeme ni mdogo huwezi kuwasha hata TV....UKIUPIMA UKO CHINI YA 120 V.....
pale Namanga madukani nao kila siku umeme hamna ....
tuache porojo...alisema zito kama hakuna mgao kawaulizeni wananchi ...
jukumu lenu waandishi kweli kuwabana hawa Tanesco na wizara husika mpaka kieleweke na wawe wakweli
 
Mkuu mnafiki sio tusi, ni mtu anayezungumza asiyotarenda au asiyoyaamini, na ni kweli tumeyaona sana kwa baadhi ya wanasiasa wetu hasa wa upinzani. Mnyika anataka kutumia hali kukatika kwa umeme kama chance ya kurejesha imani aliyoipoteza pale UBUNGO.

Watu wengine mlizaliwa kuishi kwa shida hapa duniani hivyo tunajua hamwezi kukemea uzembe wa aina yoyote ile hata kama unaathari kubwa namna gani kwenye maisha yenu.

Mimi naishi magomeni, Ni hii wiki pekee ndio sijaona umeme kukatikakatika tena kwa vipindi virefu na ninaimani kubwa sana hata hii ni baada ya viongozi kutoka CHADEMA kuanza kuuliza ni nini kinaendelea.

ZITTO ameeleza vizuri sana juzi, wananchi wanataka umeme sio maneno, kwa hiyo kama mnyika ni mnafiki au la sisi hiyo sio issue tunataka umeme tumechoka kusikia megawat mia kila siku we need our homes get powered, we need our offices get powered, mnatutia hasara kubwa sana bwana.

Kodi tunalipa, umeme mmepandisha bei, tunalipa, tatizo ni nini sasa, mmekuwa kama chuma ulete
 
Kukatika kwa umeme mara kwa mara kunatokana na hitilafu za KIUFUNDI

Utekelezaji wa miradi ya umeme imezaa MATUNDA kwa kuwepo umeme wa ziada

Only a moron can utter that STUPIDITY! And We know WHO is STUPIDY between Mnyika and Ngeleja!
 
Duh wananchi wana hasira, mnataka umeme usikatike na wanaouza majenereta wakale polisi? mnaambiwa tatizo sio umeme tatizo ni uchakavu wa miundombinu basi UBISHIIII. kweli hiki kizazi kinafaa kuongozwa na JWTZ na si vinginevyo.
 
Ngeleja haaminiki, Ngeleja hana uwezo wa kuongoza wizara ya nishati na madini, Ngeleja hana uwezo wa kutunza kumbukumbu ya mambo anayoyazungumza kama ambavyo hana kumbukumbu ya ahadi za kumaliza mgao wa umeme anazozitoa kila mara.

Kwa nchi zenye raisi imara anayejali maslahi ya wananchi wake hakuhitaji kushauriwa na mtu yeyote ili amchague Ngeleja kuwa waziri, ama kuendelea kumuacha kuwa waziri, let alone wizara ya nishati na madini.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom