Dotto Biteko: Makali ya umeme kupungua 2024

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Makali ya umeme yatapungua kwa kiasi kikubwa kufikia mwanzoni mwa 2024, kupitia juhudi za Serikali kupunguza upungufu wa umeme kutoka Megawati 810 na kufikia megawati 240.
-
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam katika hafla ya utiaji saini wa hati ya makubaliano ya ushirikiano (MoU) kati ya Wizara ya Nishati na Wizara ya Maji, Nishati na Madini ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam.
-
“Tunafanya jitihada za kupunguza makali ya umeme. Makali yakipungua huku, pia Zanzibar yatapungua,” amesema Biteko.
-
Katika hatua nyingine, Dkt.Biteko amesema kuwa, msisitizo kwa wananchi wa kutumia nishati safi ya kupikia sasa hautaishia Tanzania Bara pekee bali hatua za uhamasishaji zitafanyika hadi Zanzibar hivyo Wazanzibar watafaidika pia kwa kupata mitungi ya gesi lengo likiwa ni kuwahamasisha kutumia nishati safi ya kupikia.
 
Njooni na mbadala wa nishati ya umeme, tuondoeni kwenye kutegemea maji mnatutesa na migao isiyo ya lazima, jua na upepo pia ni vyanzo rahisi zaidi vya umeme.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom