Ngeleja atembelea Mgodi wa Barrick, Tulawaka

Ndibalema

JF-Expert Member
Apr 26, 2008
10,956
4,648
Habari za ndani kutoka kwa mdau aliyepo ndani ya mgodi wa Tulawaka uliopo mkoani Kagera unaomilikiwa na kampuni ya Barrick.
Waziri wa Nishati na madini Mh. William Ngeleja yupo ndani ya mgodi huo.

Haijulikani Mheshimiwa huyo amefuata nini lakini ameambatana na msafara wa magari aina ya V8 yasiyopungua nane.

Sasa hivi mheshimiwa akisindikizwa na Meneja wa Mgodi huo wanaelekea mesini kupata chakula cha mchana huku msafara wa magari aliyokuja nayo yakielekea sehemu maalumu ya kujazia mafuta tayari kwa kujazwa mafuta ya bure.

Ngeleja anaonekana ni mwenye furaha na hafichi tabasabu lake kila anapopena mikono wa wazungu wa hapo, pengine kuna kitu kinamfurahisha mgodini hapo.
 
vyakula mbali mbali alivyovipata umesahau hapo ni mgodini na yeye ni waziri wa madini
 
Unategemea kuwa Ngeleja amefuata mlungula huko mgodini na msafara wake wote huo?

Yaani akili zao zooote zishindwe kufikiria namna nyingine ya kupeana huo mlungula (kama upo) mpaka wakapeane kwenye mgodi? Hao wachimbaji wanaoweza kulipulia mbali mlima mzima ili wapate madini yaliyo chini ya huo mlima? Wenye kuweza kujenga hospitali ya maana kilomita moja chini ya ardhi? Na huyo Ngeleja na akili zake zooote za mjini?

Hebu fikiria tena jamani.
 
Lazima acheke cheke tuu Lazima atakuwa kapewa vitofali vya dhahabu sii chini ya ishirini -Tanzania Shamba la Bibi kweli na wananchi wake wote mazezeta wasiojitambua
 
Huyu jamaa si ameambiwa afukuze wawekezaji wa madini na sisiemu nahisi na yeye ameenda kuchukua kitofali chake na mlungula kama jamaa wa wivu wa kike alivyochukua
 
Jamani mmeshau mwezi Jan ulivyo na matumizi makubwa(ada,kilimo etc) so Ngeleja kafill deficit kidogo kaona akalambe mlungula pale kwa kuanzia wese la bure alafu kwa ofisi wataandika walijaza tena full tank
 
kwani kashamaliza ile mikutano yake kuibomoa chadema kanda ya ziwa?
 
Huyu jamaa , habari toka migodin inasemekana amepewa tenda ya kuchukua vyuma chakavu migodi yote ya barrick,duuuu jamaa noma!!! eti anasafisha mgodi!!! hiyo tenda alipataje na ilitangazwa gazeti gan??
 
Unategemea kuwa Ngeleja amefuata mlungula huko mgodini na msafara wake wote huo?

Yaani akili zao zooote zishindwe kufikiria namna nyingine ya kupeana huo mlungula (kama upo) mpaka wakapeane kwenye mgodi? Hao wachimbaji wanaoweza kulipulia mbali mlima mzima ili wapate madini yaliyo chini ya huo mlima? Wenye kuweza kujenga hospitali ya maana kilomita moja chini ya ardhi? Na huyo Ngeleja na akili zake zooote za mjini?

Hebu fikiria tena jamani.

tofali kadhaa za zahabu, huwa wanang'oka nazo wanaenda kuuza
 
Unategemea kuwa Ngeleja amefuata mlungula huko mgodini na msafara wake wote huo?

Yaani akili zao zooote zishindwe kufikiria namna nyingine ya kupeana huo mlungula (kama upo) mpaka wakapeane kwenye mgodi? Hao wachimbaji wanaoweza kulipulia mbali mlima mzima ili wapate madini yaliyo chini ya huo mlima? Wenye kuweza kujenga hospitali ya maana kilomita moja chini ya ardhi? Na huyo Ngeleja na akili zake zooote za mjini?

Hebu fikiria tena jamani.

Ndio leo nimesikia kwamba Ngeleja ana akili nyingi za mjini.
Siku ya pili leo Morogoro hakuna umeme!
Yeye anachecheka tu kama tahira huko migodini!
 
Back
Top Bottom