Suphian Juma
Senior Member
- Apr 2, 2019
- 133
- 546
MGODI WA SHANTA SINGIDA USIWABAGUE WAZAWA.
BARUA YA WAZI KWA WAZIRI WA MADINI DOTO BITEKO
Na: Suphian Juma Nkuwi
Mheshimiwa Waziri,
Nakusalim kwa Jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Pole na hongera kwa majukumu ya kujenga Taifa letu.
Awali ya yote nitangulize Kongole nyingi kwa Rais Dkt Samia kwa kurejesha na kuimarisha Sera rafiki kwa Wawekezaji na Wafanyabiashara ndani ya miaka miwili ya Uongozi wake kiasi cha kwamba sasa kila mara sote tunashuhudia makampuni mengi ya Uwekezaji ya ndani na nje ya nchi yanawekeza kwa kasi kubwa katika sekta mbalimbali ikiwemo madini ukilinganisha na muongo mmoja nyuma.
Pamoja na matunda haya ya kiuongozi na Uwekezaji, jambo la pili kuu ambalo sote Watanzania tuna kiu ya kulionja ni kuona pasina shaka Uwekezaji huo wa madini unatuletea Chakula mezani kama wananchi wenye Nchi na kukuza pato la Taifa kwa ujumla wake.
Na hapa si Serikali tu pekee bali nasi wananchi mmoja mmoja tuna uhuru, Haki na wajibu wa kufuatilia, kutathimini na kusimamia Uwekezaji ndani ya raslimali zetu zinazotuzunguka kuona zinatufukuzia umaskini na sio kutuvutia umaskini.
Mheshimiwa Waziri,
Na hapa ndio pamenifanya nishike kalamu yangu niseme jambo.
Mkoa wa Singida tuna bahati ya kuwa na Madini ya dhahabu. Rejea kuu kwa sasa ni Mgodi mpya wa uchimbaji dhahabu wa Kati wa Singida Gold Mine unaomilikiwa na Kampuni ya Shanta Gold Mining Company Limited uliopo wilaya ya Ikungi ambao kwa mujibu wa Kaimu Afisa Madini Mkazi Mkoa wa Singida Mjiolojia Chone Malembo mgodi huu umezalisha zaidi ya kilo 49 za dhahabu tangu kuanza uzalishaji mwezi Machi, 2023.
Aidha pia kwa mujibu taarifa ya Mkurugenzi Mtendaji wa mgodi huu wa Shanta Mining Limited Honest Mrema aliyoitoa mwanzoni mwa mwaka huu ni kwamba mgodi ungeaajiri zaidi ya wafanyakazi wa moja kwa moja 220 na wafanyakazi 150 wa muda mfupi.
Mheshimiwa Waziri,
Kwa nyakati tofauti katika ya Machi na Mei mwaka huu kama mdau wa agenda za vijana, madini, Mazingira na kipekee mzawa wa Wilaya ya Ikungi nimepokea malalamiko lukuki ya vijana na wakazi wa vijiji vya Ikungi kwamba mgodi wa huu wa Shanta hauwatendei haki ya kuajiriwa licha ya kwamba wana uzoefu katika kada hitajika katika kuleta ufanisi wa mgodi huo badala yake idadi kubwa ya waajiriwa "wasomi" ni wafanyakazi kutoka nje ya Wilaya ya Ikungi na Mkoa wa Singida.
Hii ni kinyume Sera ya Madini ya Mwaka 2009 na Sheria ya Madini ya Mwaka 2010 pamoja na Marekebisho yake ya Mwaka 2017 ambazo zinatoa mwongozo wa namna Kampuni za madini zinavyopaswa kufungamanisha Sekta ya Madini na sekta nyingine za kiuchumi ikiwemo pia uajiri unapaswa uwe 7/3 yaani uwiano (ratio) uwe wazawa 7 kwa wageni wa 3.
Mheshimiwa Waziri,
Idadi kubwa ya vijana wazawa wanaolalamika ni wale wenye ujuzi wa kitaaluma hususani katika nyanja za ikolojia, afya, Mazingira na ICT (TEHAMA) ambapo madai yao makuu ni kwamba wamejaribu kutuma maombi, na wengine hadi kupeleka nyaraka za kitaaluma hapo mgodini tangu mwaka 2020 punde ulipowekewa jiwe la msingi, ila si tu hawakuteuliwa kuajiriwa bali hawakuitwa kabisa kwenye usaili badala yake wanastaajabu kuona waajiriwa ni wageni bila hata wakati mwingine kuona matangazo ya kuomba kazi humo.
Mheshimiwa Waziri,
Madai haya nimeyafanyia pia utafiti usio rasmi kwa kuwahoji "randomly" wananchi wazawa kutoka Mkoa wa Singida hususani Wilaya ya Ikungi na kipekee wengi kutoka Kijiji cha Mang'onyi ambapo mgodi upo, na kubaini madai haya yamebeba asilimia kubwa ya ukweli.
Mheshimiwa Waziri,
Jambo hili linakingana na Juhudi za Rais wetu Dkt Samia na Serikali yetu ya Chama cha Mapinduzi CCM za kuutangaza umma wa Watanzania kuagana na umaskini kutokana na ujio ridhishi wa Wawekezaji wa Sekta ya madini nchini.
Mheshimiwa Waziri,
Kabla ya kuendelea naomba kuambatanisha ujumbe wa moja ya vijana wasomi kutoka Wilaya ya Ikungi ambaye amenitumia kupitia mtandao wa WhatsApp Machi 02, 2023 akilalamikia madhila haya. Naomba jina lake nisilitaje, na pale anapojitaja niondoe kwa Usalama wake na kulinda faragha yake.
NANUKUU:
Hello bro,
Habari. Natumai uko poa.
Ndg Suphian, Mimi naitwa.... (jina nalihifadhi), kijana wa chama cha mapinduzi na mkazi wa Kijiji cha Puma, nilikufahamu 2020 wakati wa uchaguzi mkuu, lakini zaidi nimekufahamu kupitia machapisho yako katika kurasa za mitandao ya kijamii ukuweka bayana yale mazuri yanayo fanya na Rais wetu mpendwa, Mhe, Samia Suluhu Hassan, hongera sana Kaka.
Ndg Suphian, ni muda mrefu sasa nimekuwa nikikufuatilia na nimeona dhahiri uwezo na karama ya uongozi ndani yako! Wilaya ya Ikungi, hususani jimbo la Singida-Magharibi linahitaji watu wa kariba yako kutuwakilisha na kutusemea katika Bunge letu tukufu.
Ndg Suphian, katika wakati huu wa mpito jina na sauti yako imezidi kuwa kubwa! Mungu ameshakupa kibali, ni wakati sasa wakutafuta kibali kwa wananchi wa jimbo la Singida magharibi.
Ndg Suphian, yapo mengi yanayoweza kukupa kibali kwa wananchi wa jimbo la Singida-Magharibi, ila leo nataka niseme jambo moja tu.
Ndg Suphian, bila shaka unatambua mradi mkubwa wa uchimbaji wa madini ya dhahabu unaotekelezwa na kampuni ya Shanta gold mining Ltd ndani ya wilaya yetu ya Ikungi.
Ndg Suphian, mradi huu ni fursa kubwa kwa maendeleo ya ujumla ya wilaya yetu ya Ikungi na maendeleo ya mtu mmoja mmoja (wazawa). Pamoja na mgodi kuwa ndani ya wilaya yetu, ni vijana wachache sana wazawa (local content) walio nufaika na kupata ajira katika mgodi huu ingawa wapo vijana wengi wazawa wenye sifa za kupata ajira katika mgodi huu.
Ndg Suphian, walio stahili kutusemea wamenyamaza kimya! Ikikupendeza, paza sauti yako kwa viongozi wa chama na serikali wa wilaya ili vijana wenye sifa ndani ya wilaya tunufaike kwa mradi huu.
Kumbuka: Kuna sauti yao, halafu kuna sauti ya mteule wa Mungu Suphian Juma Nkuwi
Kwa hayo machache ya muhimu naomba kuwasilisha.
Ni mimi,
....... . (Jina nalihifadhi).
MWISHO WA KUNUKUU.
Mheshimiwa Waziri,
Raia zangu kwako;
1) Naomba uunde Kamati/Tume kuchunguza madai haya na kupata taarifa rasmi ya Serikali na kuchukua hatua stahiki.
2) Naomba Wizara yako ya madini iagize viongozi wake wakazi pamoja na Taasisi na mamlaka zingine za Serikali kuchukua hatua za makusudi kuwaelimisha na kuwahamasisha wananchi wazawa uliopo mgodi huu ili wafahamu haki zao na kufaidika na ushirikishwaji wa uhakika kufaidi keki itokanayo na dhahabu hii iliyovumbuliwa katika ardhi yao.
Mheshimiwa Waziri,
Napenda pia kutumia baraza hii kuwaomba kwa unyenyekevu mkubwa viongozi wa Chama changu cha Mapinduzi CCM na Jumuiya zake zote ngazi ya Wilaya ya Ikungi na Mkoa wa Singida kukupa Ushirikiano, ikiwemo kwa kufanya ziara kufuatilia jambo hili na kutafuta ufumbuzi wake kwani kulipuuza litasababisha chama chetu kukosa mvuto hao wazawa ambapo kimsingi ndio wapiga kura wetu wenye imani kubwa nasi kwa zaidi ya nusu karne sasa.
Mheshimiwa Waziri,
Nawasihi pia ndugu zetu Wawekezaji wa mgodi wa Shanta kuwa waaminifu na waadilifu kwenye eneo la kuwashirikisha na kuwaajiri wazawa kwani kinyume chake tumeshuhudia maeneo kadhaa nchini na mengi duniani yenye madini wazawa na wanaponyanyapaliwa kugeuka "mbogo", kuanzisha mgogoro na kusababisha uharibifu wa migodi na kuleta maafa yasiyotamanika. Tusifike huko.
Mheshimiwa Waziri,
Samahani na Ahsante kwa kutumia muda wako kukushirikisha jambo hili adhimu, na muda wowote utapohitaji Ushirikiano wangu kwenye hili, nipo tayari.
Katika Serikali ya Rais Samia, wananchi tunaimani.
Suphian Juma Nkuwi,
Kada wa CCM,
Mzawa wa Ikungi, Singida,
Mei 04, 2023.
Simu: +25517027973
Email: yessuphian@gmail.com