Mfanyakazi wa Mgodi wa North Mara adaiwa kuuawa kwa kupigwa risasi

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,309
5,464
MAUAJI MGODI WA NORTH MARA, Mfanyakazi katika mgodi wa Dhahabu wa North Mara unaomilikiwa na Kampuni ya Barrick North Mara, Emmanuel Mgesi (25) mkazi wa kijiji cha Kemakorere wilayani Tarime anadaiwa kuuawa kwa kupigwa risasi na askari wanaolinda mgodi huo.

Kwa muujibu wa maelezo ya meneja wa mgodi huo kwenda kwa wafanyakazi jana usiku,anaeleza kwamba askari hao walikuwa kwenye ukaguzi mgodini humo ambapo walipomuona wakaanza kumkimbiza wakihisi anafanya uhalifu huku akiwa amevaa mavazi rasmi ya kazi.

Fq_-Zb_WcAE_Rrx.jpg
Chanzo: Jambo TV

=============

UFAFANUZI WA JESHI LA POLISI
Akitoa ufafanuzi, Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Tarime/Rorya, Godfrey Sarakikya amesema “Hakupigwa risasi, alijirusha kwenye shimo ndani ya mgodi akafariki Dunia baada ya kukutwa akichimba madini kwa kuiba mawe yadhaniwayo kuwa dhababu.”

Ameongeza: “Amekutwa na mawe sehemu ambayo siyo aliyopangiwa kufanya kazi, tunasubiri mwili wa marehemu ufanyiwe uchunguzi na daktari kisha ndugu watakabidhiwa mwili kwa ajili ya maziko.”
 
Mfanyakazi mwenye sare kwanini akimbizwe na askari waliokuwa kwenye ukaguzi eneo la kazi yake?
Na kwanini akimbie, wewe ni mpishi mgahawani na askari wamekuja kwenye mgahawa kufanya doria kwanini ukimbie?

Kuna kitu hakijawekwa sawa kwenye tukio au ripoti
Kuna mengi yalio jificha mkuu, huyu dogo kwa nilivyo mfahamu na yanayo semwq ni tofauti kama mbingu na ardhi..😭
 
MAUAJI MGODI WA NORTH MARA, Mfanyakazi katika mgodi wa Dhahabu wa North Mara unaomilikiwa na Kampuni ya Barrick North Mara, Emmanuel Mgesi (25) mkazi wa kijiji cha Kemakorere wilayani Tarime anadaiwa kuuawa kwa kupigwa risasi na askari wanaolinda mgodi huo...
Mnauana kwajili ya kulinda mali ya mzungu
 
Back
Top Bottom