Ngamiani: Mtoto atupwa chooni, Mama mtoto alikana kuwa mjamzito

mtungu

JF-Expert Member
Dec 15, 2021
249
403
Imetokea leo hospital ya Ngamiani inasemekana dogo ni mwanafunzi wa shule kamaliza Sekondari na kafaulu kwenda kidato cha 5.

Alikuwa na mimba anajificha watu wasijue akawa anaumwa anamwambia shangazi yake tumbo linamsumbua Leo akampeleka hospitali wajue Nini tatizo, Daktari kumuliza anamwambia ana fangasi zinamsumbua akaambiwa mbona Kama wewe una mimba? Akawa anakataa kumbe uchungu ulikuwa ushambana Sana ikabidi aambiwe aende akalete mkojo.

Kumbe ndo muda wa kuzaa umefika alipofika chooni akawa anazaa alipomaliza akataka kumsokomeza kwenye sinki la choo mtoto mkubwa akashindwa kupita akamuacha.

Sasa mgonjwa mmoja akasikia mbona chooni kwalia mtoto akaita manesi wakaenda kumchukua kwa kujua mama wa mtoto kakimbia kumbe yupo kwenye foleni.

Watu Wanalaani na shangazi yake pia analaani kumbe ni mwanae kufika zamu yake daktari akamkagua anaona damu, akumuliza tena akakataa akampeleka leba kwa uchunguzi zaidi manesi kumchunguza akaoneka kazaa akakataa akabanwa kuwa anapelekwa polisi ndo akasema kazaa mtoto yupo chooni.
 
Ila watoto wa siku hizi wanahangaika sana jamani.

Hawajui tu kwamba hayo mambo wanayoharakia huwa yapo tu na watayakuta.
Sio wa siku hizi tu, haya mambo ni ya tangu enzi na enzi. Hata bibi zetu walisema "watoto wa siku hizi".
 
Sasa jaman huyo shangazi ake alikuwa aoni kuwa mtoto wao ana mimba? Ama hio mimba yame ilikuweje had watu kushindwa kuitambua
Inawezekana, kuna mwanafunzi alijifungua bila mzazi wala walimu kujua. Mzazi kaja kugundua mtoto ana siiu 8 ndani. Mungu alivyo wa ajabu, alikuwa anamwacha mtoto nyumbani anaenda shule.
 
Mpaka Ke aeleze alichoongea na shetani bustanini Eden kwa kuwa na roho mbaya, tayari WWIII itakuwa ishatokea na Russia, China, North Korea, Iran na Iraq watakuwa washakusanya pointi 3 za ushindi na USA na EU kuwa majivu
 
Sasa jaman huyo shangazi ake alikuwa aoni kuwa mtoto wao ana mimba? Ama hio mimba yame ilikuweje had watu kushindwa kuitambua
Hii kitu isikie ivi ivi usiombe ikukute. Nina shuhuda kama 5 zote za watoto waliobeba mimba wakiwa shuleni mpk wanafikisha 9 months wazazi hawajui, wanapewa taarifa tu ya mtoto kujifungua, Tena na wazazi wakiwepo hospital apo apo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom