NEWS: Meneja wa Jengo la PPF Mwanza apewa kibano na FFU

Biohazard

JF-Expert Member
Aug 21, 2011
2,197
1,459
Hii ni habari ya kusikitisha na nimeshindwa kuelewa HAKI iko wapi ama nani ana HAKI.

Siku ya Jana katika jengo la PPF PLAZA mwanza Maaskari wamempa kipigo Meneja wa Jengo hilo wakati walipokua wakishusha pesa za Benki ya TIB(Tanzania Investment Bank). Sababu ya kipigo ilikua kumtetea kijana ambaye ni mpangaji katika Jengo hilo aliyekuakuwa amewekwa chini ya ulinzi na kupigwa kwa sababu alipita katika eneo hilo wakati pesa ikishushwa ndani ya Gari la Security Group ambalo ndio mlango wa kuingia ofisi mbali mbali katika jengo hilo.

Mapolisi hao walikua wakiongea kwa sauti kubwa mbele ya umati wa watu wakisema Hatujali cha Meneja wa nn tunaangalia ulinzi wa pesa ngoja tumpeleke kituoni ndipo atueleze vizuri huo umeneja wake.

Gari ya FFU ilikuja na kumchukua bwana mkubwa huku akiwa amevimba uso kwa kipigo na baadae alirudi ofisini kwake.#

My Take:

Mie naona haikua HAKI kumpiga meneja yule wa jengo na kama walikua na wasi wasi wangemweka chini ya ulinzi pasipo kumzalilisha kwa kipigo.

Swali

Je huyo Meneja anaweza kufungua kesi na akashinda? Au ndo tuseme hawa jamaa wamepia mamlaka yote kama wanasafirisha pesa.

UPDATES

Police leo wamefungua Jalada wanadai Meneja huyo aliwazuia kufanya kazi yao.
 
kila mtu kawa muoneaji kwa nafasi yake....kulikuwa hamna sababu ya wao kumpiga,,,
hata huyo kijana alokuwa ananatetewa na meneja, hakuwa na kosa kuita ilo eneo,,,kama polisi walikuwa hawtaki mtu apite wakati wakishusha pesa, basi wangezusha utepe wa njano.
 
Asanthe mkuu hii inatisha kwa kweli
 
hawa majamaa wakivaa vigwanda vyao vilivyopauka wanakuwaga mafioso kweli
leo asubuhi wakati nawahi ofsini nimemkuta mwanajeshi mmoja anamtandika
mtoto wa umri kama miaka 9 viboko umati umemzunguka sijui alichofanya
lakini umri wa yule dogo na yule akari na mazingira yenyewe yanaonyesha
ailikuwa anatumia nguvu za ziada kwa dogo yule
shame on poli cc
 
haaaa mwisho wa dunia si 21.12.2012 hahahaha
wapuuzi kweli hawa wanakeera sasa uende pale kituoni
lol utadhani uko jehanam utazungushwa weewe
utahangaishwa ilimradi tu watengeneze mazingira ya rushwa tuu
Wasubirie mwaka 2014 watapewa magwanda mapya wapendeze kama ilivyokuwa mwaka 2009/2010!
 
Hii ni habari ya kusikitisha na nimeshindwa kuelewa HAKI iko wapi ama nani ana HAKI.

Siku ya Jana katika jengo la PPF PLAZA mwanza Maaskari wamempa kipigo Meneja wa Jengo hilo wakati walipokua wakishusha pesa za Benki ya TIB(Tanzania Investment Bank). Sababu ya kipigo ilikua kumtetea kijana ambaye ni mpangaji katika Jengo hilo aliyekuakuwa amewekwa chini ya ulinzi na kupigwa kwa sababu alipita katika eneo hilo wakati pesa ikishushwa ndani ya Gari la Security Group ambalo ndio mlango wa kuingia ofisi mbali mbali katika jengo hilo.

Mapolisi hao walikua wakiongea kwa sauti kubwa mbele ya umati wa watu wakisema Hatujali cha Meneja wa nn tunaangalia ulinzi wa pesa ngoja tumpeleke kituoni ndipo atueleze vizuri huo umeneja wake.

Gari ya FFU ilikuja na kumchukua bwana mkubwa huku akiwa amevimba uso kwa kipigo na baadae alirudi ofisini kwake.#

My Take:

Mie naona haikua HAKI kumpiga meneja yule wa jengo na kama walikua na wasi wasi wangemweka chini ya ulinzi pasipo kumzalilisha kwa kipigo.

Swali

Je huyo Meneja anaweza kufungua kesi na akashinda? Au ndo tuseme hawa jamaa wamepia mamlaka yote kama wanasafirisha pesa.

Bangi tuu hakuna kingine polisi wengi tanzania ni wehu hawatumii akili wanapo shughulika na raia utafikira wanachunga ngombe kwani mtu kama kapita bahati mbaya si unamuonya au kumrudisha kwa mongezi ya kiungwana kama akikaidi ndio hatua zingine zifuate lakini hawa wa kwetu takataka kabisa hawana lugha nzuri.mmoja juzi nimetoka benki .
 
polisiccm ndio zao..wana stress za maisha...

Duu yani yule bwana mkubwa kiukweli walimuonea isitoshe alijitambulisha mie ni meneja wa jengo wakamwambia umeneja wako peleka huko.
 
hawa majamaa wakivaa vigwanda vyao vilivyopauka wanakuwaga mafioso kweli
leo asubuhi wakati nawahi ofsini nimemkuta mwanajeshi mmoja anamtandika
mtoto wa umri kama miaka 9 viboko umati umemzunguka sijui alichofanya
lakini umri wa yule dogo na yule akari na mazingira yenyewe yanaonyesha
ailikuwa anatumia nguvu za ziada kwa dogo yule
shame on poli cc

Aisee hawa jamaa wenye kaki cjui ni vipi?
 
Bangi tuu hakuna kingine polisi wengi tanzania ni wehu hawatumii akili wanapo shughulika na raia utafikira wanachunga ngombe kwani mtu kama kapita bahati mbaya si unamuonya au kumrudisha kwa mongezi ya kiungwana kama akikaidi ndio hatua zingine zifuate lakini hawa wa kwetu takataka kabisa hawana lugha nzuri.mmoja juzi nimetoka benki .
Mmoja juzi umetoka benki.... Jamani simulizi umeliacha kwenye chorus
 
inawezekana pia meneja alikuja kwa shari, na kutaka kutaka kuonehsa umeneja wake. unajua pesa za watu ukipewa kusindikiza si mchezo, sasa mtu akileta za kuleta, inatakiwa adhibitiwe mara moja. mpaka hao njagu wanasema tutampeleka kituoni atueleze huo umeneja wake, maana yake alionesha kudinda.

halafu kulikuwa hakuna haja ya kubagain nao wakati bado wako kazini, angesubiri wamalize shughuli yao, halafu aende kuongea nao. nadhani hayo yote yasingetokea. kwa bahati mbaya, askari wanafundishwa kutokumwamini mtu yeyote yule, hivyo meneja anaweza kutumia tittle yake kufanikisha uhalifu
 
Kwa akili ya kawaida nijuavyo mimi; watu hawa washushapo au kupakia Pesa gari yao husogezwa kabisa mlangoni na hujiekea mipaka asikatze mtu wakati wafanyapo zoezi hilo kwa kuamini kuwa Jambazi hana alama na yeyote aweza kutumika kwa kuwazuga askari na wao wakafanya tukio, so hop Meneja au huyo kijana hawakua waelewa wala subira hata wakajibishana vbaya na kutofautiana lugha, naamini pia ujambazi ungetokea pale tungewalaumu Polis hebu tuwaache wafanye majukumu yao, kuna cases hazihitaji kubembelezana"
 
Mmoja juzi umetoka benki.... Jamani simulizi umeliacha kwenye chorus

Ha haaa mambo mengi kuninterference kidogo ilijitokeza. nimetoka benki na fuko la pesa nimesimama hapo nje nasubiri dereva asogeze gari nisepe si unajua bongo huchelewi kupigwa ngwara ananifukuza toka hapa bila salamu wala kuuliza,nikaona ni mwehu alitaka nikasimame wapi na anaona nimetoka benki na fuko langu nikamkatalia nikamwambia niende wapi labda kama atanipe ulinzi hadi huko anakotaka nikasimame alipoona na msimamo akawa mpole ila ningetetemeka nafikiri hata makwenzi ningepigwa.
 
Back
Top Bottom