Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,483
- 40,008
Serikali ya Tanzania imetoa msaada wa madawa, vifaa na nyenzo mbalimbali kuisaidia nchi ya Zimbabwe kupambana na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu ambao umeushaua zaidi ya watu 500 na ukiendelea kuenea kwa kasi nchini humo na hivyo kuongeza hali mbaya kwa wananchi wake ambao tayari wanakabiliwa na hali mbaya ya kiuchumi, kisiasa na kimaisha.
Msaada huo umetolewa leo kwa Mwakilishi wa Ubalozi wa Zimbabwe nchini. Afisa wa Wizara ya Afya Bw. Berege amesema kuwa msaada huo umetolewa kwa kuzingatia ushirikiano baina ya nchi zetu mbali.
Vyanzo mbalimbali vinadokeza pia kuwa yawezekana serikali ikaandaa timu ya waatalamu kutoka Tanzania ambao wataenda kushirikiana na wenzao Zimbabwe hasa kutokana na uzoefu wa Tanzania kupambana na mlipuko wa ugonjwa huo hasa katika JIji la Dar-es-Salaam.