News Alert: Tanzania yasaidia msaada wa milioni 75 Zimbabwe

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,476
39,994
Serikali ya Tanzania imetoa msaada wa madawa, vifaa na nyenzo mbalimbali kuisaidia nchi ya Zimbabwe kupambana na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu ambao umeushaua zaidi ya watu 500 na ukiendelea kuenea kwa kasi nchini humo na hivyo kuongeza hali mbaya kwa wananchi wake ambao tayari wanakabiliwa na hali mbaya ya kiuchumi, kisiasa na kimaisha.

Msaada huo umetolewa leo kwa Mwakilishi wa Ubalozi wa Zimbabwe nchini. Afisa wa Wizara ya Afya Bw. Berege amesema kuwa msaada huo umetolewa kwa kuzingatia ushirikiano baina ya nchi zetu mbali.

Vyanzo mbalimbali vinadokeza pia kuwa yawezekana serikali ikaandaa timu ya waatalamu kutoka Tanzania ambao wataenda kushirikiana na wenzao Zimbabwe hasa kutokana na uzoefu wa Tanzania kupambana na mlipuko wa ugonjwa huo hasa katika JIji la Dar-es-Salaam.
 
Ni jambo jema kusaidia wenzetu kwenye matatizo kama haya. Lakini viongozi wetu wakumbuke namna bora ya kuondoa matatizo ya Zimbabwe ni kumwambia Bob Mugabe enough is enough!
 
Bailout,

Mugabe na cronies wake wana hela kibao na wakitaka kunyoosha mambo wanaweza.Sisi tunasaidia watu wenye resources zote, matatizo yao uongozi, wakati sisi wenyewe tunahitaji msaada.

Hogwash.
 
Bailout,

Mugabe na cronies wake wana hela kibao na wakitaka kunyoosha mambo wanaweza.Sisi tunasaidia watu wenye resources zote, matatizo yao uongozi, wakati sisi wenyewe tunahitaji msaada.

Hogwash.

Mzee usisahau kuwa wakati Nyerere anaondoka madarakani Tanzania ilikuwa bankrupt, na ni Mugabe aliyetoa fungashe la kuanza kwa awamu ya pili.
 
Bailout,

Mugabe na cronies wake wana hela kibao na wakitaka kunyoosha mambo wanaweza.Sisi tunasaidia watu wenye resources zote, matatizo yao uongozi, wakati sisi wenyewe tunahitaji msaada.

Hogwash.

Yah hela kibao lakini ni shit paper! $ 1 = Zimdollar 10000000000000x1000000000
 
Huo Msaa ni 75million Zimbabwe Dollar au 75 Million US Dollar?.

Hatukatai ni jambo zuri sana kusaidia wenzetu lakini mi nafikiri wema usizidi uwezo na wema usichukuliwe kama another opportunity ya "Ufisadi". Nchi yetu kwa sasa ipo katika njia panda, Huwezi kusaidia mtu hela za Msaada ulizosaidiwa wewe.

Nafikiri Njia pekee ya kuisaidia Zimbabwe ni hizo hela kutumika na jeshi letu kumtoa Mugabe madarakani kama hataki kutoka kwa hiyari yake. Matatizo yote haya ni outcome ya kumwachia Mugabe ang'ang'anie madaraka. Na hapa sasa tunaona kuwa cost ya Mugabe inavuka mpaka mipaka yake. Hizi 75 Mil USD zingeweza kuwarudisha wanafunzi wetu Vyuoni kama Mugabe angeheshimu uamuzi wa wananchi.

Kuna msemo usemao "Warabu wa pemba wajuana kwa viremba", na njia hii inaonesha ni jinsi gani Tanzania inamuona Mugabe kuwa yupo sahihi kwani mchezo alioucheza ni mchezo wetu hata sisi Tanzania * Ref: Uchaguzi wa Zanzibar*
 
1. Pamoja na yote...sisi kama wanadamu Watz tuna wajibu kuwasaidia wananchi wa kawaida Wazimbabwe wanaougua Kipindupindu.. Mugabe awe tatizo or otherwise!

2. Naskia pia Namibia na Afrika ya Kusini pia wametuma madawa..mimi naona Tz tumechelewa!

Huu ni msaada wa Kibinadamu!
 
Mwanakijiji,

..hizo ni USD au madafu?

..na kwasababu fedha hizo zimetolewa kwa mwakilishi wa zimbabwe/mugabe Tanzania ina maana Tanzania inatambua utawala ulioko madarakani Zimbabwe?
 
Tunaangalia matawi ya juu ya tatizo badala ya kuangalia mzizi wa tatizo.

Kama Zimbabwe ikiendelea kuwa na Mugabe for the next 10 years na kutokana na policies zake mbaya kipindupindu kikaendelea miaka 10 tutaendelea kuwasaidia for the next 10 years?

Kiini cha tatizo ni Mugabe na siasa zake mbaya, akiondoka Mugabe kuna uwezekano mkubwa sana Zimbabwe ika shine once again.

Mtoeni Mugabe mambo mengi tu yatakaa sawa.
 
Pundit,
Nakubaliana na wewe.

Ila kwa sasa hivi.... yaani leo hii...kuna kipindupindu Zimbabwe...je tumtoe kwanza Mugabe ndo wananchi wapewe dawa? Namaanisha leo hii!

May be tukisaidia Zimbabwe kwa sasa.. halafu tukikaa nae.. huenda akabadilika.. kwa kuona aibu.

Nadhani ni Shs 75 m (kama USD 70,000)
 
Tanzania yaisaidia Zimbabwe dawa za kipindupindu
Na Exuper Kachenje

SERIKALI ya Tanzania imetoa msaada wa dawa na vifaa mbalimbali kwa serikali ya Zimbabwe kwa ajili ya kupambana na ugonjwa wa kipindupindu unaoindama nchi hiyo.

Msaada huo umetolewa na Serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na kuuukabidhi kwa maafisa Ubalozi wa Zimbabwe katika hafla iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wizara hiyo jijini Dar es Salaam jana.

Akikabidhi msaada huo kwa niaba ya Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Profesa David Mwakyusa, Mkurugenzi wa Tiba wa Wizara ya Afya, Dk Zacharia Berege, alisema Rais Jakaya Kikwete na serikali ya Tanzania imeguswa na matatizo ya Zimbabwe, hivyo kuiagiza wizara hiyo kutafuta namna ya kuisaidia.

Dk Berege alisema: "Baada ya kupata taarifa ya kipindupindu kushamiri nchini humo, Rais Jakaya Kikwete aliona kuna umuhimu wa kuwasiadia wenzetu na wizara inatoa dawa na vifaa mbalimbali vyenye thamani ya Sh75 milioni kwa serikali ya Zimbabwe".

Dk Berege alisema Rais kikwete aliagiza lifanyike hilo kutokana na uhusiano mzuri ulipo baina ya nchi hizo na kuokoa maisha ya watu ambao wako hatariki kuuawa na ugonjwa huo.

Msaada huo unajumuisha maboksi zaidi ya arobaini ya dawa za vidonge aina ya Ciprofloxacin, Doxycline, Erythromycin, Unga wa Erythromycin, Sodium Lactate, Sodium Chroride na Cresol.

Nyingine ni dawa aina ya Chlorinated lime, Methylated spirit, plasta, bandeji, pamba ambazo zilipokelewa na maafisa wawili wa ubalozi wa Zimbabwe nchini, Kumbirayi Taremba na Zvidzai Taliwa.

Akizungumza baada ya kupokea msaada huo, Taremba alimshukuru Rais Kikwete, serikali na wananchi wa Tanzania kwa kutambua matatizo ya Zimbabwe na kuwapatia msaada huo.

Alisema msaada huo unaonyesha uhusiano na mshikamamo iliyopo baina ya Tanzania na Zimbabwe tangu nchi hiyo ilipokuwa katika harakati za kupigamia Uhuru wake kutoka kwa wakoloni wa Uingereza.

"Mnajua Zimbabwe inakabiliwa na janga la kipindupindu unaoua wananchi wetu ambao ni nguvu kazi, wakiwamo wanawake na watoto. Tunamshukuru Rais Jakaya Kikwete, Serikali ya Tanzania na watu wake kwa msaada huo, asanteni sana," alisema Taremba.

Mwanakijiji,

..hizo ni USD au madafu?

..na kwasababu fedha hizo zimetolewa kwa mwakilishi wa zimbabwe/mugabe Tanzania ina maana Tanzania inatambua utawala ulioko madarakani Zimbabwe?

Humanitarian aid cant be politicized.. unataka tusubiri wamalize mgogoro usioisha then tusaidie.. ??lol
 
kinyambiss said:
Humanitarian aid cant be politicized.. unataka tusubiri wamalize mgogoro usioisha then tusaidie.. ??lol

kinyambiss,

..huo siyo mtizamo wangu. ukifuatilia mijadala ya zimbabwe jamii forums utabaini hilo.

..lakini nadhani ukipitisha opinion poll hapa usije ukashangaa kwamba wengi wanapendelea mambo yazidi kuharibika wakitegemea Mugabe atalazimika kuondoka madarakani.
 
Humanitarian aid cant be politicized.. unataka tusubiri wamalize mgogoro usioisha then tusaidie.. ??lol

Hata mwenyewe umecheka !!!. Migogoro iliyopo DRC ni mikubwa na kama ni humanitarian nadhani hapa tutakiwa tuonyeshe juhudi zetu vilevile.

Kumsaidia Mugabe kuna political elements ndani yake kutokana uhusiano mkubwa ulipo kati ya ZANU na CCM politburos.

Tanzania ingeweza kutumia 75USD kwa mambo mengi tu iwapo serikali ya Zimbabwe ingeweza kusafisha mambo yake ya ndani.

Kipindupindu kinatokana na watu kunywa maji machafu. Na waZimbabwe wangeweza kujikinga kwa kutumia very low-tech bila msaada wa Tanzania.
 
Hata mwenyewe umecheka !!!. Migogoro iliyopo DRC ni mikubwa na kama ni humanitarian nadhani hapa tutakiwa tuonyeshe juhudi zetu vilevile.

Kumsaidia Mugabe kuna political elements ndani yake kutokana uhusiano mkubwa ulipo kati ya ZANU na CCM politburos.

Tanzania ingeweza kutumia 75USD kwa mambo mengi tu iwapo serikali ya Zimbabwe ingeweza kusafisha mambo yake ya ndani.

Kipindupindu kinatokana na watu kunywa maji machafu. Na waZimbabwe wangeweza kujikinga kwa kutumia very low-tech bila msaada wa Tanzania.[/QUOTE]

Zakumi i agree with you, lakini the bolded part is a bit of an understatement, kusema uchafu tuu haitoshi. Kipindupindu husababishwa na kula kinyesi cha binadamu mwingine mwenye vijidudu vinavyo sababisha kipindupindu, huo ndio ukweli ambao nafikiri kikwete angeujua angeconvince au members majeshi yakamshushe Bob from his high horse au sijui ni unicorn! Aibu iliyoje kuachia watu wake wanakufa coz of ingesting fellow humans excreta!! Oh South Rhodesia....what hath become of thee?
 
Nina rafiki zangu waZimbabwe walio nje ya nchi na wanalalamika jinsi gani viongozi wetu wanavyomkumbatia Bob.

Siku Bob akiondoka kuna uwezekano mkubwa new generation ya waZimbabwe wakasahau tuliyofanya wakati wa ukombozi na kuona kuwa sisi tuliwasaliti.
 
kuokoa maisha ya binadamu asie hatia hakuhitaji debate, ingekuwa ni mugabe mwenyewe ndio kapigwa na kipindu pindu hapo ingekuwa another story, lakini hawa innocent victims of evil political games kwanini tuwasusie wakati kosa sio lao?. nakumbuka kuna kipindi tanzania visiwani tulikumbwa na kipindu pindu mpaka maiti tukawa tunaziona ni jambo la kawaida, ni maradhi mabaya sana yakiwa out of control. huzuni zangu zote nazielekeza kwa raia waathirika wa zimbabwe, na naipongeza serikali ya tz kwa kusaidia na kama wana uwezo wa kusaidia zaidi ya hapo basi nipo pamoja nao.
 
Swali. Zimetoka kwenye fungu gani? Au ni mafisadi wametoa walizoiba na kuwapelekea jamaa zetu Zimbabwe. Inachekesha sana wakati wazee wa EAC, waalimu na wengine wana madai mengi tu serikali inasema haina hela. huku mabulungutu yakipelekwa Zimbabwe. Sijui kuna interest gani huko. Mwanakijiji ukiweza chimba tupate motive ya kupeleka hizo hela, labda kuna ajaneda ya siri.
 
Back
Top Bottom