News Alert: Mwangunga aliangukia Bunge; asamehewa!

Wazawa ni mimi mlala hoi, ninayepata mlo mmoja kwa siku, ninayepinda mgongo shambani/kazini kutwa kwa malipo kiduchu ni mimi ngozi nyeusi ambaye baba, babu, baba ya babu na babu ya babu yangu mzaa mama na mzaa babu walizaliwa kamachumu muleba na kufia muleba, na mimi ningali Tanzania na wale wengine wote wanaofanana na mie ndio wazawa, usipoelewa hilo basi kammulize Simba

Una hakika kuwa babu wa babu yako alizaliwa Kamachumu?
 
Mtu asiniambie eti Rostam ni mzawa. Si mzawa hata kidogo hata kama babu yake alizaliwa Igunga au Bukene. Hivi partner wake wa karibu asiwe Lowassa ila ni Habib muiran wafilisi nchi? Eti wanaomtetea si mnafuta njaa na leo na kesho kutwa wakati unga unapanda bei?
 
Rostam ameingiaje humu?
 
Akiomba kusamehewa, Mwangunga alisema yote yalifanywa kwa nia njema. Naona nia njema imekuwa utamaduni na uhalali wa maovu yote tunayofanyiwa na wakubwa hawa. Alianza Lowasa akasema serikali kusaini mkataba na Richmond ilikuwa kwa nia nzuri ya kuliepusha taifa na giza baada ya mtera kukauka, juzi Pinda kaangua kilio barazani akidai kauli aliyotoa usukumani aliitoa kwa nia nzuri ya kuwatisha wauuaji wa ndugu zetu Albino, Lipumba naye akaja na yake kutaka kubebwa na chadema huko Mbeya kwa madai kuwa walimuwekea pingamizi Shitambala kwa nia nzuri ili upinzani uchukue kiti cha ubunge. Sitashangaa kesho akisimama Mzindakaya na kusema pesa alizokwapua BOT ilkuwa kwa nia nzuri ya kuwawezesha wananchi wa jimbo lake kupata maziwa!

- Tupo ukurasa mmoja mkuu, saafi sana. Huyu mama majuzi alikuwa anahangaika kugawa rushwa ya kumsaidia Auntie Sophia kuwa mwenyekiti wa UWT, leo anaomba radhi on what?
 
Hivi UKIUWA na wewe ni MBUNGE, tena kwa KUKUSUDIA yaani UNAPANGA na kwenda kufanya kitendo. Mbunge huyu akienda bungeni (kama Dito vile) na kuomba msamaha, basi asamehewe? Kwa kesi ya Pinda naweza kusema ni HASIRA ambayo ilipanda bila kupanga na KUROPOKA. Ila huyu Waziri, aliyepokea maombi, akaweka sahihi na huku akijua alishaahidi kuwa HATAFANYA HIVYO, sidhani kama anastahili msamaha. Ni sawa na kesho, ikitokea PINDA aropoke tena, nitakuwa wa kwanza kumvalia BANGO.
Huyu kweli wapinzani ndiyo walitakiwa kulala naye mbele. Wakati anafanya maovu hayo alikuwa na akili timamu. Alijua anafanya nini. [/SIZE]Na kama alikuwa hajui/kasahau maneno ambayo mwenyewe aliahidi na hayo wala si mengi kama katiba basi huyu wakomae naye.

Inawezekanaje kitu kilichozuiliwa na MUHILI mmoja wa utawala (Bunge) uvunjwe na MUHIMILI mwingine (Serikali), Mwanasheria Mkuu wa serikali alikuwa wapi kugundua hili mapema? Mwanasheria wa Wizara alikuwa wapi asigundue hili? Nasikia harufu ya RUSHWA, hapa ni WIZI MTUPU. Na akiwafutia leseni hao wazungu kama keshakula hela yao wanaweza mkomalia wakaja KUMKOLIMBA, akae mkao wa machale chale. Labda kama Wataliano hawamo maana hawa hawana dogo, mafia kwenda mbele!!!
 
- Tupo ukurasa mmoja mkuu, saafi sana. Huyu mama majuzi alikuwa anahangaika kugawa rushwa ya kumsaidia Auntie Sophia kuwa mwenyekiti wa UWT, leo anaomba radhi on what?

Jamani, huwezi kuwa kiranja wa kugawa RUSHWA kama nawe si mla RUSHWA. Tusubiri tu ikiundwa sekretariati ya Umoja wa wanawake Mwangunga kama mgawa rushwa wakati wa uchaguzi, atapata cheo kinono toka kwa Sofia wa Simba. Akina mama oyeee!!!
 
- Tupo ukurasa mmoja mkuu, saafi sana. Huyu mama majuzi alikuwa anahangaika kugawa rushwa ya kumsaidia Auntie Sophia kuwa mwenyekiti wa UWT, leo anaomba radhi on what?

Ulimkamata? Huoni kama ungefanya hivyo ungeondoa aibu ya chama chako kaka? in simple language ulipomuona ulifanya nini? au unadhihirisha Chukua Chako Mapema?
 
Inawezekanaje kitu kilichozuiliwa na MUHILI mmoja wa utawala (Bunge) uvunjwe na MUHIMILI mwingine (Serikali), Mwanasheria Mkuu wa serikali alikuwa wapi kugundua hili mapema? Mwanasheria wa Wizara alikuwa wapi asigundue hili? Nasikia harufu ya RUSHWA, hapa ni WIZI MTUPU. Na akiwafutia leseni hao wazungu kama keshakula hela yao wanaweza mkomalia wakaja KUMKOLIMBA, akae mkao wa machale chale. Labda kama Wataliano hawamo maana hawa hawana dogo, mafia kwenda mbele!!!

Mimi tatizo langu ni bunge kuingilia utendaji wa serikali. Bunge lina mamlaka gani ya KUAMURU serikali? Kama ni ushauri, basi serikali ina haki ya kuchagua kufuata au kutofuata.
 
Ni lini watawajibika au kuwajibishwa? msamaha maana yake umekubali makosa na kaa pembeni wengine wafanye kazi. lakini muda bado upo itabidi waangaliwe.

Kuwawajibika au kuwajibishwa au kuomba msamaha wakati mwingine ni too late. Kinachotakiwa ni proper vetting. List ya waborongaji inazidi kuwa ndefu .. na Mwangunga is just another entry.
 
Utamaduni wa kuomba samahani ni mzuri.Ila usitumike kama janja ya kukwepa uwajibikaji.Nafikiri kama tunafuata utawala wa sheria ni vyema mtu awajibishwe kwa mujibu wa sheria zilizopo then samahani aombe baadae. Hii itakuwa ikitumika kama janja ya kukwepa uwajibikaji. Jambo lihusulo maslahi ya taifa sheria na taratibu zilizopo under ministerial responsibilities zifuatwe.
 
Ulimkamata? Huoni kama ungefanya hivyo ungeondoa aibu ya chama chako kaka? in simple language ulipomuona ulifanya nini? au unadhihirisha Chukua Chako Mapema?

- Kwani hapa JF tumewahi kuwakamta wangapi wala rushwa tunaowasema hapa kila siku? Yaaani ni waste of my time hata kuendelea kukujibu.

Have a nice day mkuu!
 
KLHN International

Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Shamsa Mwangunga amekuwa Waziri mwingine wa serikali ya Rais Kikwete kuomba radhi Bungeni kufuatia kile ambacho kimeelezewa kuwa ni kudharau Bunge kwa kuchukua maamuzi ambayo hayakuzingatia hoja ambayo iko mbele ya Bunge. Mhe. Mwangunga ameliangukia Bunge leo hii baada ya Mbunge wa Kwera Mhe. Chrisant Mzindaka kuona kuwa Waziri huyo amedharau hoja yake ambayo ilikuwa inasubiriwa kutolewa maamuzi Bungeni kuhusu suala la vitalu vya uwindaji.

Mwaka jana Bw. Mzindakaya alitoa hoja Bungeni ili serikali isitishe kutoa leseni kwa wawindaji wa nje ambao muda wao unamalizika mwaka huu mpaka taarifa itakapotolewa na Waziri juu ya mapendekezo yaliyotolewa kuboresha sekta hiyo ya uwindaji. Hata hivyo imekuja kugundulika kuwa Waziri Mwangunga ameshatoa maamuzi hayo na kuwaongezea leseni wawindaji hao kitu ambacho "kilimkorofisha" Mhe. Mzindakaya. Endapo Bunge lingeamua kupitia hoja hiyo na kumchukulia hatua Mhe. Mwangunga basi angekutwa na dharau ya Bunge (Contempt of parliament) kosa ambalo linalingana na lile la kudharau Mahakama (Contempt of court). Adhabu ya kosa hilo ni siku saba jela.

Vyanzo vyetu kutoka Dodoma vinasema kuwa baada ya kuona kuwa upepo hauendi upendo wake Mhe. Mwangunga akifuata njia iliyotengenezwa na Waziri Mkuu Pinda jana ambaye aliomba msamaha kwa wale wa Tanzania wanaoona amekosea naye mama Mwangunga aliona hana njia nyingine isipokuwa kuomba msamaha kwa Wabunge. Inaonekana Bungeni kumekuwa na hali ya huruma na baadhi ya wabunge wa CCM na hata wale wa upinzani wametangaza kumsamehe.

Hata hivyo haijulikani huko mbeleni ni kiongozi gani mwingine naye atakuwa tayari kuomba msamaha kwa mtindo huu na hivyo kukwepa kuwajibishwa. Maoni ya watu mbalimbali ambao wamekuwa wakifuatilia masuala haya wanaona kuwa itakuwa vigumu sana huko mbeleni kumwajibisha mtu yeyote kwani wotesasa watakuwa wanasimama kuomba samahani na wengine kumwaga machozi kwa "uchungu".

Kazi pevu sasa Tumsubiri Rais Mr mkapa nae akalipage chozi pale Bungeni na kusamehewa (we live in very intresting country)God Bless me and God Bless all Good TANZANIANS

Hivi vilio vya na machozi ya mamba embu wabunge ondoeni uchovu,maana PM kaonyesha njia ya kupenya wengine wote watafuata huku wakisemba mbona yule kaachiwa na mimi nina haki ya kuachiwa maana hata sijafikia amri ya kuruhusu watu kuuwana kwa visingizio vya kumbaka albino.
 
Tatizo la nchi hatutaki kufuata taratibu na sheria. Waziri amedharau bunge, kuomba radhi kwa maneno pekee haitoshi, ilitakiwa zifuate hatua zingine za uwajibikaji ili kukomesha mambo ya namna hii. Kesho atatokea mwingine atafanya uozo then ataomba radhi. Huu si utawala bora unaotakiwa kwa ajili ya maendeleo ya Taifa na watu wake. Tuache mzaha na maslahi ya taifa letu. Sheria zifuate kwa wote na si kubagua huyu mkuu huyu mdogo. Ifikie mahali tusioneane haya na tutangulize maslahi ya Taifa mbele zaidi ya maslahi ya Vyama vya Siasa.
 
I believe our constitution knows nothing of msamaha! Let the rule of law operate then msamaha baadae! Wasitake kulazimisha huruma from wananchi...Angalia zito anavyosema 'Tukiwa makini na kufuata Sheria namba 3 ya mwaka 1988 ya Haki,Madaraka na Hadhi ya Bunge,tunaweza tukaamua leo waziri aende keko kwa siku saba. Hata hivyo,hatuwezi kufika huko kwa sababu amekuwa muungwana, ameomba radhi' Hata wakina Lowassa,Karamagi,Msabaha,Chenge,Mramba,Yona na Mgonja wakiomba radhi kwa misingi ya kwamba waliyafanya waliyoyafanya kwa nia njema itakuwaje? tusiisaidia sheria kufanya kazi. tuiache itawale.Kwa alieomba na asioeomba radhi,tuiache iamue
 
Tatizo la nchi hatutaki kufuata taratibu na sheria. Waziri amedharau bunge, kuomba radhi kwa maneno pekee haitoshi, ilitakiwa zifuate hatua zingine za uwajibikaji ili kukomesha mambo ya namna hii. Kesho atatokea mwingine atafanya uozo then ataomba radhi. Huu si utawala bora unaotakiwa kwa ajili ya maendeleo ya Taifa na watu wake. Tuache mzaha na maslahi ya taifa letu. Sheria zifuate kwa wote na si kubagua huyu mkuu huyu mdogo. Ifikie mahali tusioneane haya na tutangulize maslahi ya Taifa mbele zaidi ya maslahi ya Vyama vya Siasa.

Nasisitiza sheria ifuate mkondo wake. Kwa haya maneno ya Zitto aliyoyasema bungeni, nanukuu, "Tukiwa makini na kufuata Sheria namba 3 ya mwaka 1988 ya Haki,Madaraka na Hadhi ya Bunge tunaweza tukaamua leo waziri aende Keko kwa siku saba.Hata hivyo,hatuwezi kufika huko kwa sababu amekuwa muungwana,ameomba radhi" wingine wakiomba radhi itakuwaje? Think of Yona,Mramba,Lowassa,Karamagi and many more...
 
Kwa kuwa amekiri alikosea, ina maana alitakiwa kufuta hivyo vibari na kupisha hoja ya Wabunge indelee na mkondo wake sio?

Samahani bila kurekebisha makosa ina manufaa gani kwa Watanzania?

Subutu!!!! Afute vibali wakati wameshakula vya watu,,, Tayari walishakunja mikwanja yao, wa kupeleka mtoto ulaya keshaenda,,, wa kununua nyumba kesha nunua, wa Vog naye keshalipia,,,, hela hawana tena. Kama unabisha wathubutu kufuta hivyo vibali uone waliotoa pesa zao watakavyong'aka.
Hata hivyo mikikimikiki ya wizara hii haiwezi.
 
Na tatizo ndo hilo maana kwa maelezo yake ametahadharisha kunaweza kuwa na some economic and legal implications. If u try to read between lines....Mwangunga anasema 'Naomba mnisamehe maana kuongeza muda nismeshaongeza muda tena kwa mkataba halali wa serikali( japo umekaa kiwiziwizi kwa maslahi ya wazungu) hivyo kubadilisha ni ngumu. changa la Macho kwa wabunge.Wanazugwa kwa 'sorry' neno raisi sana kutoka kinywani kwa mzungu lakini chugu kama shubiri kutika kinywani mwa mwafrika hasa anapokuwa na kacheo.
 
sheria ifuate mkondo wake. Kwa haya maneno ya Zitto aliyoyasema bungeni, nanukuu, "Tukiwa makini na kufuata Sheria namba 3 ya mwaka 1988 ya Haki,Madaraka na Hadhi ya Bunge tunaweza tukaamua leo waziri aende Keko kwa siku saba.Hata hivyo,hatuwezi kufika huko kwa sababu amekuwa muungwana,ameomba radhi"

Naomba iwekwe hiyo sheria namba 3 ya mwaka 1988 inayoipa madaraka kumpeleka lupango waziri kwa kutekeleza wajibu wake. Hawa wasitudanganye. Kama wamechukizwa na utekelezaji wake wapige kura ya kukosa imani na serikali yao! Huku kupenda kujikwaza katika jamii yetu ndiko kunakotuletea matatizo. Bunge linataka kuiendesha serikali, waziri kumuendesha katibu mkuu wake, n.k. Kwa mwendo huu basi hawa waheshimiwa watatka hata kuwaendesha majaji na mahakimu!

Amandla...........
 
Back
Top Bottom