MpigaFilimbi
JF-Expert Member
- Apr 30, 2008
- 1,169
- 182
kwa Bahati mbaya sana wengi wetu huwa tunakariri propaganda za CCM nsa kuamini kwamba ndiyo ukweli wenyewe. upinzani sasa hivi una nguvu zaidi maeneo ya Vijijini kuliko mijini.
vyama vingine vimeanza kupata kura nyingi zaidi vijijini kuliko mijini. wakati sehemu nyingine za Tanzania CHADEMA imepata viti vingi kwenye serikali za mitaa,lakini imeambulia viti vinne tu kwenye jiji la Dar es salaam!!
hoja hii ya kuelimisha wanavijiji ni sawa na ile inayosema vyama vingine viungane ili kuitoa CCM. inawezekana kweli timu nyingine ziungane ili ziitoe Simba kileleni? ili nani awe mshindi kati yao?
Umesema kweli kabisa. Tatizo la watu wa mjini wengi ni maopportunists sio watu wanaotafuta mabadiliko ya kweli. Watu wa vijijini wakiamua kumng'a hata kiongozi wao wa kijiji wanaweza kwa kumwambia waziwazi. Tumeona mifano mingi, katika wabunge wa upinzani wangapi wanatoka mjini? Na je hiyo ni sababu ya elimu? Siku zote nashangazwa na hili, mjini watu wanaamini katika kupata mlo wao tu, ni wa binafsi kupindukia. Na hata jamii ya wasomi inastahili lawama katika hili, wengi wetu tuko very sensitive na vibarua vyetu wako radhi wampigie magoti fisadi. Mfano ni hao mafisadi wanavyojitanua, unadhani wafuasi wao wako vijijini ambao hawana elimu? this is so disgusting!!