New Force/Golden Deer kwanini ajali mnapata nyie tu?

Si kweli

Tatizo la New Force ni madereva wako rafu sana barabarani

Zhong Tong ni basi za kazi kama Scania
Zhong tong hana air suspension , ndoo maana ukipanda basi za kichina uwe makini kwenye kuchagua seat ya kukaa , siti za nyuma zinarusha kama mabasi ya kikoloni
 
Kwenye mbio Basi za mchina zipo vizuri, Wechai Cummins engine inamsumbua vizuri Scania.

Mchina kaachwa kwenye suspension systems na braking system upande wa retarder.

Gari ya kichina kama ni roli yenye stop engine ukikimbia kwenye corner ukitumia stop engine ili upate matokeo mazuri lazima uwe below 40kph, wakati ukiwa na retarder ya hydraulic chini ya 60kph ukigusa gari inakupa tokeo zuri.

Basi ya kichina kwenye safari ndefu kama dereva ni mtu wa kukanyaga brake pedal lazima usikie brake drum zikinuka sababu ya ufanisi wa kawaida wa eddy current retarder
 
Zilikuwa zikipata ajali,ila angalia miundo mbinu wakati huo na sasa,angalia teknolojia ya magari wakati huo na sasa….ukija kwa sasa fanya tafiti njia hyo hyo ya dar-mbeya mabasi mangapi aina ya European na mchina yaliyopata ajali,halafu fuatilia mfumo wa kimakenika wa basi za European na basi za mchina unaweza ukapata kitu
Basi linawaka na kuteketea zima zima hapana mchina katisha.Ubora na viwango European watabaki kuwa bora tu kwa wakati wote.Na sasa hivi haya matoleo ya mchina kabana injini kubadilishwa kirahisi.Hivyo baada ya muda kubadili engine,gear box na diff kuweka ya scania itakuwa ngumu,likifa una hela ya kuweka injini mpya ya kichina gari linapaki.
 
Mkuu hizi Zhongtong Climber Mega mchina kaweka limit kwenye engine bay huwezi kuweka ya Scania?
 
Mkuu hizi Zhongtong Climber Mega mchina kaweka limit kwenye engine bay huwezi kuweka ya Scania?
Yutong mpya engine ikichoka uwezi weka ya Scania itakubidi uweke injini ya Yutong Cummins etc hila Zhongtong sijajua japo matoleo yote ya nyuma.ya kichina yalikuwa unaweza kumodify kwa kuvalisha engine ya scania diff na gear box.
 
Km mpk wewe umekubali Baasi hazifaii hizoo
Gari inakimbia utadhani mnawahi kuzimu
Hapana kwa kweli

Bina,sipendi magari yanayotembea mwendo wa kobe,ila siyo kwa ukimbiaji wa new force 🙌
11 kamili tayari lishafika Mbeya,utasema walikuwa wanapaa njiani.
Kama ni mbio tu,zile zimepita kiasi,,hakuna gari Mbeya inakimbia kama New force,haipo!
 
Kaahh...wapuuzi
Sana Bina
Ni matapeli 🤣🤣
Biashara imeisha,limebaki jina na wanaendelea kuchukua pesa za watu.
Walijichanganya huo mchezo wao walimfanyia ndugu yetu,tuliwapeleka LATRA,polisi wakaja kuwasomba.
Hela walirudisha.

Ukikata tiketi kwao, kata at your own risk ila gari hawana.
Watawapandisha lolote bovubovu.
 
Baadhi ya basi za kichina manufacturers anaweka option ya basi kuja na retarder. Na retarder za kwenye basi za kichina zinazokuja ni Eddy Current Retarder hii efficiency yake huwa inapungua maji yakigusa na inatumia umeme.

Kwenye Golden Dragon za UDART mchina kafunga gearbox ya Voith na hydraulic retarder.

European manufacturers wanatumia hydraulic retarder ukicheki kuanzia Volvo,Scania,Man Diesel,Daf,Iveco etc.

Retarder ya Bus za kichina na Scania au European brand uwezi linganisha, dereva wa Scania ana faida kubwa kwenye Braking ukiacha kutumia pedal brake, retarder iliyopo kwenye gearbox inampa faida kwenye brake.
Umetisha mkuu
 
Kwamba ni matatizo ya kiufundi ndio hupelekea ajali za New force kuwa nyingi? Yanaweza kuwa yepi Mkuu?
Baadhi ya basi za kichina manufacturers anaweka option ya basi kuja na retarder. Na retarder za kwenye basi za kichina zinazokuja ni Eddy Current Retarder hii efficiency yake huwa inapungua maji yakigusa na inatumia umeme.

Kwenye Golden Dragon za UDART mchina kafunga gearbox ya Voith na hydraulic retarder.

European manufacturers wanatumia hydraulic retarder ukicheki kuanzia Volvo,Scania,Man Diesel,Daf,Iveco etc.

Retarder ya Bus za kichina na Scania au European brand uwezi linganisha, dereva wa Scania ana faida kubwa kwenye Braking ukiacha kutumia pedal brake, retarder iliyopo kwenye gearbox inampa faida kwenye brake.

Cc:eek:ffshore seaman
 
Back
Top Bottom