New alert: 96.8 Live Hamad Rashid

Inaonyesha kiti cha ubunge kinamuuma sana HR maana wapambe wake wanaongea kwa kuwaangukia wapigakura wake. Inaonyesha walihaha sana kuomba asifukuzwe lakini jamaa waligoma. Inaonekana pamoja na kuwatishia kuwa Mungu anatisha lakini bado wakamtimua tu. n
 
Hivi inakuwaje mtu anakuwa na majina mengi mpaka inachosha kumsikiliza wakati akiwa anajitambulisha. Kuna jamaa anaongea eti ni mwkiti wa cuf aliyefukuzwa ametaja majina zaidi ya sita.
 
Naona katumia njia ya 'Masheikh' Mkutano wote umetawaliwa na hotuba za Masheikh! Hii kali ya mwaka.
 
Kumbe HR alikuwa anachuniwa na Maalimu Seif hata alipokuwa akienda kwake! Alikuwa akiongea kama radio jamaa anauchuna. Hii kali sasa.
 
...."nawasaidia wakulima wa pemba 50%"...., duh hawa wapambe wake nao na kelele, nadhani kuna watu wengi sana huko.
 
Jamaa anaponda lakini! Ngoja tuone kama Maalim atakuja kuvaa nguo maana jamaa anamvua ile mbaya!
 
Anasema yeye vimulimuli alianza navyo miaka ya 1982 na wala hamuonei ghele, ha ha ha ha, hii mipasho sijui.
 
Hivi hii ya kulalamika kuwa wabunge wa CUF hawana elimu ndiyo maana wamepitwa na wabunge wachadema kwa hoja jamaa kasema ukweli nini?
 
Naona wameamua kuvuana nguo hawa, ngoja sie yawe yetu masikio, maana naona ndo anajibu mapigo ya Maalimu Seif. Anawaambia wanaomfuata maalimu hawataiona pepo.
 
Hivi hii ya kulalamika kuwa wabunge wa CUF hawana elimu ndiyo maana wamepitwa na wabunge wachadema kwa hoja jamaa kasema ukweli nini?

nadhani ni kweli maana kasema CUF imepanda bangi bungeni kinategemea kuvuna nini? Inaonesha wabunge wa CUF ni vilaza. Kasema wabunge wa CHADEMA wasomi.
 
Anasema hata Nyerere alisema kioo kikiingia vumbi hupanguswa na kikipasuka huondoshwa na CUF kimepasuka kwa hiyo kiondoshwe.
 
Anamponda Duni eti kama ni mwanaume akagombee jimboni asingojee apointment, si matusi haya kweli.
 
Back
Top Bottom