Neno La Leo: Utamjua Mwafrika Anapohama!

maggid

JF-Expert Member
Dec 3, 2006
1,084
1,246
Na Maggid Mjengwa,


UKITAKA kumjua Mwafrika, basi, mwangalie siku anapohama. Ndivyo tulivyo. Hata kwenye uongozi, ni hivyo hivyo. Mwangalie kiongozi wa Afrika anapoingia na anapotoka kwenye madaraka.


Ndio, hana tofauti sana na Mswahili anayehama kutoka Mwananyamala kwenda Magomeni. Mswahili wa Mwananyamala, hata kama atahakikishiswa, kuwa anakohamia Magomeni vyumba vyote vina taa za balbu na pazia za madirishani na milangoni, bado, Mswahili huyu atahakikisha, kabla ya kuhama, anang’oa balbu na pazia zote kutoka nyumba anayohama. Mpangaji mpya atakayekuja atajua mwenyewe! Huyo ndio Mwafrika, ingawa si wote, hata ukimchanja kwenye damu yake, utakuta chembe chembe za ushamba uliochanganyika na hila.


Hakika, hizo ni hulka za Mwafrika, hata azaliwe na kukulia Ulaya au Marekani. Si tumesikia majuzi, Waziri aliyepoteza ubunge alihakikisha anahamisha mpaka pazia kutoka kwenye ofisi ya mbunge jimboni kwake. Naambiwa, kuwa Waziri huyo kakulia Marekani. Kumbe, kukulia Marekani hakumwondolei Mwafrika hulka zake! Na hilo Ni Neno La Leo.


( Hii ni sehemu ya makala yangu ( Raia Mwema) ikichapwa, kesho Jumatano.)



Maggid
Iringa
Desemba 28, 2010.
 
Na Maggid Mjengwa,

Hakika, hizo ni hulka za Mwafrika, hata azaliwe na kukulia Ulaya au Marekani.


( Hii ni sehemu ya makala yangu ( Raia Mwema) ikichapwa, kesho Jumatano.)


Maggid
Iringa
Desemba 28, 2010.

mkuu..... salaam...... hulka hii unayoisema ya mwafrika je? ni constructive au destructive...... will this attitude give value to a true African..... please clarify
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom