TANMO
JF-Expert Member
- Apr 12, 2008
- 11,514
- 11,276
TANMO,
Ahsante sana. Sishangai kuwa sieleweki kwa wengine. Jamii yetu haina mazoea ya watu kama mimi. Lakini najua, kuna wanaonielewa. Natumai iko siku utanielewa.
Maana, kuna wanaofikiri, kuwa Maggid Mjengwa ni CCM. Kuna wanaofikiri kuwa mimi ni CHADEMA, kuna wanaofikiri kuwa mimi ni CUF, kuna wanaofikiri kuwa mimi ni Muislamu. Kuna wanaofikiri kuwa mimi ni Mkristo. Wote hao wanabahatisha.
Sijapata kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa. Ningependa nikumbukwe, kuwa Maggid Mjengwa alikuwa Mtanzania na Mjamaa aliyejitahidi kufanya yale aliyoamini yana maslahi kwa Tanzania, basi.
Maggid,
Iringa,
Jumapili, Februari, 12, 2011
mjengwa
Maggid,
Kuhusu jamii yetu kutokuwa na mazoea ya kuwaelewa watu kama wewe, sijui. Ila binafsi sikuelewi kwa misingi kuwa mwandishi yeyote makini huwa na itikadi pamoja na msimamo wake thabiti juu ya kile anachoandika. Kusema kwamba wewe huna Chama napata mashaka kwa maana kwamba, kama ni kweli, basi ungekuwa unaandika makala zako bila kuegemea upande wowote, vinginevyo unajenga mazingira ya kuonekana mnafki ilhali siyo mnafki au ndiyo matokeo ya watu kutokukuelewa kama inavyotokea kwenye makala zako nyingi.
Kwenye mikanganyiko kama hii kuna mjinga mwiongoni mwetu (siyo kwa maana ya tusi).. Hivyo tuweke hisia kando tuchekeche fikra zetu na tuuondoe ujinga wetu kwa manufaa yetu na Taifa kwa ujumla.
Ubarikiwe sana.
N.B.. Heri ya Jumapili huko kwenu.