Neno "KAMBI YA UPINZANI" LIFUTWE badala yake tutumie "KAMBI YA UTETEZI".

CCM walitumia neno "UPINZANI" kuwatisha watanganyika wengi hasa wanaoishi vijijini (wenye elimu ya kawaida) psychologically. Kuhusu kubadilisha jina, mkuu umeona mbali
 
I support Kwa kweli neno hili SIO zuri . . Kama wapinzani kambi Yao inaitwa uponzani JE kambi ya Chama tawala ITAITWAJE?!?
 
Ndio utetezi wa umma, umenena vizuri sana. Lakini inaonekana misukule ipokila mahala.
 
Yani umefiria mbali sn mkuu wale sio wapinzani kwa sababu ni wawakilishi na watetezi wa wananchi walio wanyonge na wasioweza kusikika


Sent from my BlackBerry 9360 using JamiiForums
 
weka hoja na sababu, jumlisha umaana.

>>>>>sijakuelewa

Unaposema Upinzani Maana yake Pinga(always oppose) sidhani Kama ni tafsiri ya nzuri Kama tunavyoitumia. Na Bunge Lina Kazi nyingi SIO kila siku watakuwa Kwenye marumbano ya Hoja. Kuna Bajeti, maswali na majibu, Hoja, kamati mbalimbali Na kadhalika bila kusahau michezo.

Kwa Maana hiyo kumwita mbunge mpinzani inamaana kila kitu apinge Hata Kwenye michezo apinge, vikao vya Kamati apinge kila kitu apinge sidhani Kama ndio Maana yake. Sasa kama SIO Maana yake KWANINI kumpa Mtu Jina ambalo SIO Maana ya utendaji wake?

Bunge ni Debating Chamber, wakati wa hoja wabunge Wote wana Haki ama kuunga mkono Hoja au kuipinga. Tafsiri ya Bunge la sasa umelifanya Bunge kuwa la KIDIKTETA zaidi. Wabunge wamejikuta wakinyang'anywa haki Yao ya kutoa maoni Na kulazimika kufuata mkumbo Hata Kama hawautaki. Huu ni udhalilishaji wa utu wa mtu unaomfanya mbunge kuharibika Na kutoka kuwa mwakilishi wa wananchi Na kuwa mwakilishi wa fikra Za Chama chake apende-asipende.

Si kweli Kwamba wabunge wote wa CCM wanaunga Mkono maamuzi ya Chama chao Hata Kama hayana weledi Na mustakabali wa kitaifa, si kweli kwamba wabunge wote wa CDM au CUF wanaunga Mkono kila alichokisema mbunge wa Chama chao Kwa Jina la Upinzani, I mean si kila neno la mpinzani mmoja ndio Sauti ya wapinzani wote! . Kila Mtu anao Uhuru wa kipima semi na hoja Na kuunga mkono kadiri serikali ya Kichwa chake itavyomuongoza Maana serikali ni mawazo ya watu. Mawazo bora zaidi huleta serikali yenye Neema Kwa wananchi sisi, Na mawazo ya kidikteta, yasiyo Na demokrasia ya Mtu mmoja-mmoja huleta taifa mzigo mzito sana.

Nadhani ufike sasa wakati muafaka wa kufutilia mbali kupachikiana majina nuksi Kama haya. Ufike wakati muafaka wa kila mbunge kujitambua sasa Kwamba amepewa ridhaa Na wananchi kuwakilisha Na si ujingaujinga Mwingine Wa wengi wape Hata Kama ni uwingi wa uovu tuepukane nao

Kuwa wengi SIO hoja ikiwa mko Kwa ajili ya uovu, Kwenye Historia ya Biblia watu wengi waovu walipiga kelele "BWANA Yesu asulubiwe" ingawa hakuwa Na kosa maskini ya Mungu Sauti zao zikashinda, wakamsulubisha , ingawa sauti zao hazikuwa Za Haki.

Nashauri Jina Hili Upinzani lifutwe Kama la Utetezi halita pata nafasi Basi wataalam wa lugha watafute jina sahihi SIO HILI.
 
Back
Top Bottom