Neno Fupi La Usiku Huu: Mshindwa Mzuri Ni Yupi?

maggid

JF-Expert Member
Dec 3, 2006
1,084
1,246
Ndugu zangu,

Mshindwa mzuri ni yule anayeamini kuwa katika ushindani kuna kushinda na kushindwa. Yu tayari kuinua mkono na kumpongeza mpinzani wake aliyemshinda. Ni yule anayejitathmini ili kuangalia makosa yake ya kimkakati. Ni mshindwa aliye tayari kujifunza kutoka kwa mshindi.

Katika siasa, ni yule anayetamka na kumaanisha kuwa yuko tayari kumsaidia mshindi katika kutekeleza majukumu yake yaliyotokana na ushindi huo, endapo mshindi atahitaji msaada huo.

John McCain ni mfano wa mshindwa mzuri pale ambapo, si tu aliinua mkono kumpongeza Barack Obama kwa ushindi wake, bali pia alimkumbatia Obama na kuonyesha utayari wake kumsaidia Obama katika utawala wake, maana, katika ushindani wao, kilicho kikubwa kabisa ni kulinda maslahi ya taifa la Marekani.

Na mshindwa mbaya ni yupi? Tusubiri Neno Fupi la Usiku wa kesho. Alamsiki!

Maggid Mjengwa,
Dar es Salaam.
0788 111 765
Mjengwa Blog::Habari,Picha,Matangazo
 
Back
Top Bottom