Elections 2010 NEC yasimamisha Chadema kufanya kampeni Maswa

demokrasia hakuna hapa! Wanataka serikali ichaguliwe na nec na siyo sisi wapiga kura! Hii inasikitisha sana!
 
Kama ni kweli huu ni ujinga NEC sio mahakama, na ndio vitu vya kupuuzi kama hivi vinaweza kuliletea taifa mambo mabaya kama ya kenya
 
Kwa sheria ipi wamezuia kampeni, kwani tarehe imefika? Au ni kwa amri toka juu?
 
Hivi yule OCD aliyepigwa ngwara anaendelea kufanya kazi? Kweli pesa inatudhalilisha!
 
demokrasia hakuna hapa! Wanataka serikali ichaguliwe na nec na siyo sisi wapiga kura! Hii inasikitisha sana!
 
Sijaelewa wanwezaje kuzuia kampeni? Maana kuna za nyumba kwa nyumba. Kuna za sisi kuwapigia wagombea kampeni sasa wamezuia zipi? za majukwaani?
 
NEC ni moja ya vyombo nchini vinavyosababisha uvunjifu wa amani nchini.
Ninashauri vyombo vya habari msije tia chumvi katika hili maana mkitangaza kuwa Shibuda kaondolewa mjue gharama yake itakuwa kubwa kuliko msiba uliompata yule dereva wa mgombea wa CCM.

Uhai wa mtu hauwezi kulinganishwa na kitu chochote no matter una itikadi ipi. NEC kuweni macho sana kuchezea akili za watanzania. Hizo mbinu zote hazitafaa, watanzania wanajua zaidi ya hayo. Tumeshachoka na UFUSKA wenu. Ndiyo nimesema UFUSKA.
 
Acha hasira kaka, ni kweli nimeongea na jamaa yangu yupo Maswa ni kweli kuanzia leo amesimamishwa kampeni mpaka siku ya uchaguzi, meaning hakuna kampeni bali watapiga kura tu,...inauma!

Kama Shibuda amezuiwa kufanya kampeni Maswa mpaka siku ya uchaguzi, basi MwanaJF yeyote anayeweza kuwasiliana na Dk. Willibrod Slaa amwombe Mgombea u-Rais huyu aite Press conference ashughulikie hii confusion.

Wananchi wa Jimbo hilo la Maswa waambiwe wajitokeze wote Jumapili tarehe 31 Oktoba kupiga kura, wakifahamu kwamba shujaa wao John Shibuda amenyimwa haki yake ya kuzungumza nao siku hizi mbili za mwisho wa kampeni. Wananchi hawa wakumbushwe kwamba Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Bw. Manumba, baada ya uchunguzi wa kina, amemwona John Shibuda hakuhusika na mauaji ya yule dereva wa CCM.

Shibuda hana hatia. Kwa hiyo wapiga kura wampigie kura ili aendelee kuwakilisha wananchi wa Maswa . Sasa Shibuda akichaguliwa kwa tikti ya CHADEMA atakuwa Mbunge mwenye tija na jasiri zaidi, hasa ikizingatiwa kwamba sera zinazofafanuliwa na Dk. Slaa ndizo atazopigania.
 
Habari nilzopata sasa hivi ni kwamba NEC imekisimamisha Chadema kufanya kampeni katika jimbo la Maswa. Hiyo imemuaffect Marando ambaye amezuiwa kuingia Maswa kufanya kampeni.

Kwa habari nilizoambiwa jana na jamaa yangu aliyepo Maswa,kaniambia kuwa NEC ilimsimamisha Shibuda kuanzia siku ya Jumatatu hadi Jumatano; hukumu ya jaji Makame kwa Shibuda ilikoma Jumatano na leo(alhamis)karuhusiwa kuendelea na kampeni zake kama kawaida!

Hizi ni habari za kuambiwa tu na siwezi kuthibitisha nani ni mkweli zaidi kati ya mleta mada hii ambaye anasema kuwa Shibuda kazuiwa leo hadi siku ya kupiga kura na jamaa yangu aliyeniambia kwa simu kuwa Shibuda kazuiwa Jumatatu hadi Jumatano na sasa karuhusiwa kuendelea na kampeni zake!

Mliopo karibu zaidi na Maswa tuelezeni uzuiwaji wa Shibuda ni kwa siku gani?Je ilikuwa toka Jumatatu hadi Jumatano au Alhamis hadi Jumapili?
 
Back
Top Bottom