Mwanamayu
JF-Expert Member
- May 7, 2010
- 11,361
- 6,485
Yaelekea CCM na NEC wamegundua mbinu mpya za medani za kuchakachua kura kiulaini kwani NEC wataiagiza polisi kufukuza watu watakaokuwa wanataka kubaki vituoni ili kulinda kura kwa madai ya kuwa hiyo siyo kazi yao.
NEC yadai kubaki vituoni kunaweza kusababisha fujo lakini hawana tatizo na mashushu kuwepo vituoni. Hii ni changamoto mpya kwani Kenya mbona wapiga kura hubaki vituoni ili kutenda haki?
NEC ina maelezo gani juu ya watumishi wa Idara ya usalama wa taifa ambao sasa hivi wanatawanya kona za Nchi ili kuchakachua kura zetu aisee.
Hapa nina wasiwasi ya kuwa tone la damu laweza kudondoka.
Chadema yapaswa kuwasiliana na NEC haraka iwezekanavyo ili kuweka utaratibu wa uwazi wa wapiga kura kushuhudia uhesabuji wa hata kwa kuwa nje ya kituo chao cha kupiga kura ili kumulika mashushu wabebao mikoba myeusi iliyorundikana mapesa.
Bila ya kufanikisha hilo basi CCM atatumaliza kabisa.
Kama mbinu hizi Chadema hazitazitafutia muarobaini mapema basi kilio na kusaga meno cha wasubiri
Hivi sheria si kuwa mbali na kituo kama mita mia moja au mia mbili? Wananchi tukae umbali huo na tuangalie nani anaingia na nani anatoka kwa mbali. Ikiwezekana tutumie binoculars ambazo zipo nyingi tu kwa wamachinga!