Ndugu zangu nimefiwa na baba yangu

Chamkoroma

Senior Member
Sep 6, 2010
186
11
Ndugu yenu nimefiwa na baba yangu jana tar. 18/2/2011 muda wa saa 11 jioni kwa habari toka kwa ndugu zangu, mimi ndugu yenu nipo nje ya TZ, ni vizuri kukaa mbali lkn yanapotokea mambo kama haya inaumiza sn, natamani ningekuwa nyumbani ningewahi mazishi kwani mazazi wangu amefia kijijini kwetu na nimbali na motuary, inaniuma sn kwani sitakuja uona uso wa baba yangu.

Hapa jamvini ni kwetu sote ni vema kupeana habari hizi.

Mungu awabariki sana.
Chamkey.
 
Pole sana mkuu, mungu aiweke mahala pema peponi roho ya baba yako na akupe wewe nguvu na ujasiri katika kipindi hiki cha majonzi, tuko pamoja na again, pole sana.
 
Pole sana ndugu kwa msiba uliokupata. Mungu akupe faraja na akutie nguvu wewe pamoja na waombolezaji wote.
 
mkuu .. pole sana ..... kazi ya mungu haina mipaka ... RIP
 
pole sana Chamkey, inauma mno kupoteza mzazi na inauma zaidi pale unapokuwa mbali bila kuweza kumuaga kwa mara ya mwisho.

Mungu atakutia nguvu, yeye ndie awezae yote, nyie mlimpenda lakini Mungu alimpenda zaidi, mapenzi yake yatimizwe.

Pole sana
RIP Mzee wetu
 
pole sana ndugu yangu! jipe moyo sote ndiyo njia hiyo ni kweli inauma bila kuona hata sura mara ya mwisho! inauma!
 
Pole sana mkuu.hakika ni wakati mgumu sana lakini yote ni mipango ya Mungu.Mungu akupe nguvu ya kuhimili na pia Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi...pamoja sana mkuu
 
Ndugu angu nashukuru sana kwa maneno yenu ya upendo, kweli najisikia faraja kuwa ninao ndugu zangu japo sijawahi kumuona hata mmoja wenu.

Mungu awabariki sana, najiandaa kuondoka kuanza safari kurudi nyumbani kuanzia jumanne au jtano niandae ticket baada ya kupata ruhusa toka kazini, Mungu awabariki sana sana ndugu zangu najisikia amani sana kwa maneno yenu ya kunifariji.
 
Chamkey,
Pokea salamu zangu nyingi sana za pole.
Labda nikufahamishe kuwa tatizo kama ulilo nalo wewe limeshatufika wengi sana, na hakuna jinsi zaidi ya kulibeba na kumwomba Mungu akupe faraja hasa kipindi hiki kigumu kwako.
Mungu aiweke pema peponi roho ya baba yetu mpendwa.

Lakini kwa nafasi ya pili ya jambo hili, naona umeamua kuweka kila kitu kwenye anonimity, huenda ukawa unaamini katika privacy ideology!
Lakini ingekuwa ni mtu kama mimi ambaye sina ideology hiyo ningeweka mambo hadharani, kuwa baba yangu anaishi wapi, na atazikiwa wapi kimaeneo,...huwezi jua bana...dunia hii ni pana na mahusiano hayana mipaka!
Ni mtazamo tu broda huku tukiwa tunaendelea na maombolezo.

Nadhani nimeeleweka...Kaza moyo kaka!
 
Pole ndugu kwa huo msiba mkubwa. Mungu akupe nguvu na akutangulie ktk safari yako
 
Pole kwa msiba mzito uliokupata jipe moyo kuushinda uzuni mungu upanga kila jambo nahiyo nimipango ya mungu hakuna wakuipangua lamsingi nikumwombeakwa mora amwondoshee kila aina ya mizigo huko ahera ili awe huru!!
 
Pole sana kaka.
Mungu akupe moyo wa uvumilivu na busara zaidi kipindi hiki ambacho hautamuona tena baba yako.

Mungu akupe nguvu na ruhusa upate ili kuja kuona japo nyumba ya kudumu ya mpendwa wako.
 
Pole sana ndugu. May the almighty God help u to be strong in this hard time.may tha soul of your dear Dad rest in peace in the eternal light.

Amen
 
Back
Top Bottom