Ndugu yangu ana mashetani, je ofisini kwake nipeleke supporting document gani?

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,870
155,831
Ndugu yangu anasumbuliwa na mapepo wachafu wenye kuongea kiarabu kitupu, tangu Ijumaa anaongea makorokocho.
Je ninapoenda kumuombea ruhusa ofisini nipeleke kithibitisho gani?
 
Ni mgonjwa huyo, Mpeleke Kimara KKKT kwa mapacha apate maombezi mapepo yote yatatimkia baharini.
 
Document inayotambuliwa na taasisi yoyote ni ripoti ya daktari(ED). Ama kwa tiba mbadala,Mbanikie ulimi wa kitimoto ukauke vizuri paka chumvi kiasi kisha mpe ale. Atapona.
 
Hapo kazi ipo.sidhani kama bosi wake ataamini kuwa ana mapepo.mpeleke job atleast amuone
 
Hana haja ya ED. Akiombewa anarudi tu kazini mara moja. Usichelewe nae we mpeleke mara moja na watumishi watamwombea na yatamtoka kwa jina la Yesu. Jaribu kuomba likizo ya dharura kama hajaenda kazini muda mrefu. Usichelewe hayo cha mtoto kwa bwana Yesu.
angekuwa mgonjwa angeenda hospitali angepewa ED, je huko KKKT wanatoa document gani kuonyesha kuwa jamaa ni mgonjwa
 
Record hayo makorokocho anayoongea halafu nenda nayo ukaape kwa mwanasheria au mahakamani kuwa kweli hayo yameongewa na huyo ndg yako. Wakishasaini peleka hivyo vyote ofisini. Wakikataa basi wenyewe ndo waliomtupia madubwasha hayo.
 
kweli hizi sasa ni siku za mwisho

tena yawezekana wateule washanyakuliwa na inaelekea ni wachache mno,tuliobaki including yule mdingi alipiga hesabu za 21 may,tunataabika na mambo ya maluweluwe,ooops sijui itakuwaje huko mbeleni?!!!!
 
Ndugu yangu anasumbuliwa na mapepo wachafu wenye kuongea kiarabu kitupu, tangu Ijumaa anaongea makorokocho.
Je ninapoenda kumuombea ruhusa ofisini nipeleke kithibitisho gani?

hebu tuwekee hapa jamvini hayo makorokocho ....!
 
bujibuji,u a so funy.
kwani hakuna makonda wanao ongea kiarabu?ha ha haaaaa.
 
Ndugu yangu anasumbuliwa na mapepo wachafu wenye kuongea kiarabu kitupu, tangu Ijumaa anaongea makorokocho.
Je ninapoenda kumuombea ruhusa ofisini nipeleke kithibitisho gani?
Mfukize kwa majani ya kitunguusomu na mavi ya Tembo na na mavi ya punda siku hiyo anapozungumza lugha hiyo ya kiarabu kama kweli anayo mashetani wachafu watamkimbia hawata kuja tena kumletea

matatizo wakati unamfukiza avae shuka nyeupe huku unamuombea kwa jina la Mwenyeezi mungu yamtoke hayo mapepo wanayomsumbuwa wakati unapomfukiza useme maneno haya ( Ewe pepo uliyekuwepo ndani ya taja jina lake (fulani bin fulani) ninakuondosha utoke ukimbilie baharini kwa jina la Mwenyeezi Mungu mmoja toka haraka) Sema mara 3 usikae mbele yake wakati unapomfukiza asije kukuvamia wewe kisha umfukize asubuhi na usiku kwa muda wa siku 3 yatamkimbia mwilini hayata rudi tena hayo mapepo yaliyomkumba.
 
Mfukize kwa majani ya kitunguusomu na mavi ya Tembo na na mavi ya punda siku hiyo anapozungumza lugha hiyo ya kiarabu kama kweli anayo mashetani wachafu watamkimbia hawata kuja tena kumletea matatizo wakati unamfukiza avae shuka nyeupe huku unamuombea kwa jina la Mwenyeezi mungu yamtoke hayo mapepo wanayomsumbuwa wakati unapomfukiza useme maneno haya ( Ewe pepo uliyekuwepo ndani ya taja jina lake (fulani bin fulani) ninakuondosha utoke ukimbilie baharini kwa jina la Mwenyeezi Mungu mmoja toka haraka) Sema mara 3 usikae mbele yake wakati unapomfukiza asije kukuvamia wewe kisha umfukize asubuhi na usiku kwa muda wa siku 3 yatamkimbia mwilini hayata rudi tena hayo mapepo yaliyomkumba.
Hiyo ndio supporting document ya kupeleka ofisini kwake kuonyesha kwamba hajaenda kazini kwa kuwa ana mapepo?
 
Mpeleke hospitali kitengo cha magonjwa ya akili aonwe na psychiatrist, lazima tu atapata diagnosis fulani na atakupa document za kukusaidia kuomba ruhusa kazini..problem solved..ila itakuja problem nyingine ambayo inaweza ikahatarisha ajira ya mshkaji, kama ana ugonjwa wa akili ataweza kufanya kazi? usalama wa colleagues zake? unyanyapaa?

Chagua mwenyewe.
 
Back
Top Bottom