Marire
JF-Expert Member
- May 1, 2012
- 12,328
- 5,270
Muda mfupi uliopita Mh Kangi Lugola ameomba muongozo kwa Naibu spika kutaka kujua inakuweje leo wanajadili wizara muhimu kama ya chakula ambayo ndio tegemeo la Watanzania, ila ndani ya ukumbi wa bunge kuwepo mawaziri 5 na manaibu waziri 5 tu?
akajibiwa muongozo utatolewa baadae.
akajibiwa muongozo utatolewa baadae.
Mhe. Ndugai leo saa 6 na dk 11 mchana ametetea kutokuwepo kwa mawaziri bungeni wakati hoja zao (wakati huo) hoja ya Wizara ya kilimo inajadiliwa.
Akatoa mfano wa mfumo wa Bunge wa Kenya ati kuna kuna Mabunge 2 SENETI & BUNGE la kawaida ambako sasa mawaziri si wabunge na hawakanyagi bungeni, so akawaambia wabunge kutokuwepo mawaziri bungeni Si kitu cha kigeni.
JE NDUGAI analinganisha Bunge la Kenya & TZ? Sisi TZ hatujafikia kwa Mawaziri kutohudhuria Bungeni wakati hoja zao zinajadiliwa Bungeni.
Hivi wakati mawzairi wanakuja kujibu hoja huwa wanajibu hoja gani wakati hawakuwepo bungeni? Ni kweli mawaziri wanakuja kujibu kwa usahihi kama zilivyotolewa na wabunge?