Kosa la Mwigulu Nchemba ni nini?

KUZIMU

New Member
Sep 9, 2022
3
12
Wanajamvi, nimependa namna Mwandishi wa mwanahalisi alivyochambua hoja, ebu tupitie Kwa pamoja link hiyo tulijue kosa la Dkt Mwigulu Nchemba

--
KWA wanaofahamu jinsi serikali inavyofanya kazi, wanaofahamu kutungwa kwa muswada, kufikishwa kwa mswada huo bungeni na hadi kuwa sheria, hakuna shaka kuwa watakubaliana na mimi katika swali hili. Kwamba, “Kosa la Mwigulu, ni lipi?” Anaripoti Mwandishi Maalum … (endelea).

Kwamba, utaratibu wa kupeleka hoja kwenye Baraza la Mawaziri, unaanzia mbali kidogo. Hoja inaanzia kwa wataalam wa wizara chini ya Katibu Mkuu na wakurugenzi wake. Baada ya kuchambua na kujiridhisha na kile wanachokipendekeza, huwasilisha jambo hilo kwa waziri.

Kazi ya waziri, ni kulifikisha wazo hilo kwenye Baraza la Mawaziri, kupitia kitu kinachoitwa, “Cabinet Paper.” Mkutano wa Baraza la Mawaziri unaongozwa na Rais.

Wazo hilo la wataalam wa wizara likishafikishwa kwenye Baraza na iwapo libakubaliwa, linaondoka kwenye mikono ya wizara na kupelekwa kwa Kamati ya Makatibu wakuu wa wizara – Inter Ministerial Technical Committee (IMTC).

Kamati hii, hulichakata wazo lililoletwa na wakishajiridhisha wanalirudisha kwenye Baraza chini ya Katibu Mkuu Kiongozi.

Nalo Baraza likiona liko vizuri, maelekezo yanatolewa kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), kuandika muswada kulingana na maelekezo au mtazamo wa Kamati ya Wataalam ya makatibu wakuu kama ilivyopata baraka za Baraza la Mawaziri chini ya Mheshimiwa Rais.

Kwa muktadha wa sakata la tozo, wote ni mashahidi kuwa wazo lilianzia kwa aliyekuwa Spika wa Bunge, Job Yustino Ndugai. Alilitaka Bunge kuagiza serikali kuandaa muswada kwa ajili ya tozo za miamala ya simu na benki.

Katika mazingira hayo, ni serikali gani duniani itakwenda kinyume na maelekezo ya Bunge, tena ambayo yametolewa na Spika mwenyewe?

Katika suala zima la tozo, Serikali inaweza kusamehewa katika lawama na badala yake Ndugai na Bunge lake, ndiyo inauyopaswa kuwajibishwa.

Hii ni kwa kuwa Ndugai alikuwa na ajenda binafsi na jambo hili, hasa juu ya mkopo wa Sh. 1.3 trilioni ambazo serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan, ilikopa kutoka mashirika ya fedha ya kimataifa.

Ndugai alilenga kuonyesha umma, kuwa Rais Samia anaingiza nchi kwenye mikopo isiyokuwa na tija na hivyo, msimamo wake wa kuleta tozo, umelenga kuwaondolewa wananchi mzigo wa madeni. Kwamba, taifa hili, linaweza kujiendesha bila mikopo au misaada kutoka nje.

Kwa ufupi, alikuwa amejitosa rasmi kwenye mbio za urais 2025. Ndio msingi wa maneno yake, kwamba “ikifika 2025, wananchi wataamua wenyewe, wachague wanaotaka kuendesha nchi kwa mikopo au wanaoweza kuendesha nchi kwa mapato ya ndani.”

Hivyo basi, kwa kuwa tumeonesha jinsi mchakato wa sheria unapoanzia; shinikizo la Bunge lilivyokuwa kubwa katika sakata hili, unaweza kuona dhahiri kwamba kumlaumu Mwigulu, ni kutaka kumtoa kafara.

Kutaka Bunge kukaa pembeni na kulitupia suala hili lote mikononi mwa Mwigulu, ni kutaka kumuonea. Hii si haki!

Hakuna asiyefahamu jinsi Rais Samia anavyoheshimu demokrasia shirikishi, tangu akiwa waziri katika serikali ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete. Waliokuwapo bungeni wakati huo, wanaweza kuwa mashahidi wa hili.

Kwamba, Rais Samia – wakati huo, akiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), alikuwa anashirikisha hata wapinzani wake wa kisiasa, kwenye mambo yanayohusu maslahi ya umma.

Kwa mwenendo wake huo, Rais hakuzuia wabunge wa chama chake, kuchangia mjadala huu wa tozo kwa uwazi ndani ya Bunge. Hakuzuia maoni ya wabunge wake wala kuwalazimisha kupitisha hoja hiyo. Kila mbunge alikuwa huru kuchangia na kutoa maoni yake.

Kile ambacho kinaonekana sasa, ni hatua ya baadhi ya wabunge – wakiwamo wale waliounga mkono hoja ya Ndugai kuhusu tozo – kutaka kujiweka kando na sakata hili. Hili haliwezi kukubarika.

Yaani mtu amekuwa mbunge au waziri, ameliona jambo hili likipitishwa kote huko na yeye akiwamo, lakini hukulipinga wala kutoa maoni mbadala, kisha leo anataka kuwa wa kwanza kuonekana mtetezi wa wananchi, hili haliwezi kunyamaziwa.

Kuna taarifa zisizo na mashaka kwamba baadhi ya watu wanaokosoa tozo hizo hadharani au kuwatumia baadhi ya wananchi, wanafanya hivyo, kwa maslahi yao binafsi.

Hii ni kwa sababu, baadhi ya wanaopinga tozo sasa, walikuwa na nafasi ya kufanya hivyo ndani ya Bunge. Yawezekana hawakuweza kunyanyua mdomo kwa kuwa walimuhofia Ndugai. Kama madai hayo ni kweli, basi watakuwa wamepoteza sifa ya kuwa viongozi wa umma.

Hauwezi kuwa kiongozi wa umma, kisha ukawa mwoga wa kutetea maslahi ya wananchi au chama chako.

Wengine waliopo kwenye mradi huu, wameshiriki vikao vya Baraza la Mawaziri, ambako hoja hii ilipelekwa baada ya maelekezo ya Bunge la Ndugai. Hawakusema huko, hawakusema bungeni wala hawakusema kwenye vikao vya chama.

Kushindwa kujadili athari za tozo kwenye Baraza la Mawaziri, bungeni au kwenye kikao cha chama, ni hujuma dhidi ya Rais Samia na serikali anayoingoza.

Kwa muktadha huo, zigo hili, haliwezi kuachwa linasukumizwa kwa mtu mmoja – Mwigulu Lameck Nchemba – kwa baadhi ya watu kutaka kukimbia dhana ya uwajibikaji wa pamoja.

Kuendelea kumsakama Mwigulu kwenye hili, kunaweza kuthibitisha madai ya baadhi ya watu, kwamba kinachotafutwa hapa siyo tozo. ni Mwigulu.

Kwamba, watu wameona walitumie jambo hili, kummalizia kisiasa, lengo hasa likiwa uchaguzi mkuu wa 2030 (urais) na ule wa mwaka 2025, hasa kwenye wadhifa wa uwaziri mkuu.

Kwamba, kwa kutumia tozo, kutengenezwe mkakati wa kumpoteza yule anayeweza kuonekana kuwa mshindani wa kundi fulani.

Na huu ndio utaratibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM). Nani asiyejua kuwa Edward Lowassa, alisukiwa zengwe katika sakata la Richmond kwa sababu ya urais na uwaziri mkuu?

Nani asiyejua kuwa Hans Kitine, aliyekuwa waziri wa utawala Bora, katika serikali ya Benjamin Mkapa, alisulubiwa kwa sababu ya mbio za urais?

Kitine – mkurugenzi wa zamani wa usalama wa taifa (TISS) na baadaye mbunge wa Makete – alituhumiwa kujinufaisha binafsi katika matibabu ya mkewe nchini Canada.

Aliyeibua sakata hilo bungeni, akatoa nyaraka na kuaminisha umma kuwa waziri huyo, ametumia madaraka yake vibaya, haikuwa muda alijitambulisha rasmi kuwa yuko upande gani kwenye mbio za kumrithi Mkapa.

Hata kilichompata Iddi Simba, mmoja wa wanasiasa mashuhuri na waziri mwenye nguvu katika serikali ya Mkapa, aliyelazimishwa kujiuzulu katika kilichoitwa, “kashifa ya sukari,” ilikuwa ni mbio za urais za mwaka 2005.

Shamsi Vuai Nahodha, aliyepata kuwa waziri Kiongozi wa Zanzibar na baadaye akateuliwa na Kikwete kuwa waziri wa mambo ya ndani, anaweza kuingizwa kwenye orodha ya walioathirika na mbio za urais.

Ni baada ya wabunge kumshikia bango ajiuzulu, kufuatia ripoti ya Kamati Teule ya Bunge juu ya utekelezaji wa Operesheni Tokomeza, kuwataja maofisa wa polisi kutenda uhalifu.

Lakini ndani ya mioyo ya wasuka mkakati, hoja haikuwa Tokomeza. Bali, ni mbio za urais wa Zanzibar mwaka 2020. Vuai na wenzake watatu – Balozi Khamis Sued Kagasheki, Emmanuel Nchimbi na Mathayo David – walilazimishwa kujiuzulu 20 Desemba 2013.

Kwa muktadha huu, kinachotengenezwa dhidi ya Mwigulu sasa kupitia tozo, ni mwendelezo uleule wa kutengenezeana kile ambacho Kikwete alikiita kwa Lowassa, “ajali ya kisiasa.” Kwamba, anayetafutwa hapa ni mtu, sio tozo. Tusidanganyane.

Chanzo: Mwanahalisi Online
 
Na umaskini wote huu nyie mnawaza urais 2030?

MNA uhakika mtafika?

Yupo WAPI JPM mliosema atawale milele?

KIFUPI MAKOSA YA MWIGULU NI MENGI:

Ugaidi: SOMBETINI ARUSHA

Wizi: SINGIDA BIG STARS

Wizi: TOZO

Dharau: MKAISHI BURUNDI

Kuanza kampeni za urais: 2025, 2030

Kumpotosha Rais: Tozo n.k
 
  • Sisi tunamjua Mwigulu Nchemba aliyeapa hadharani hayo ya kutuambia sijui makatibu, ... Hayatuhusu. Yaani mpishi upike chakula kibovu, kisha ujitetetee sijui fulani alileta kuni, fulani hakuchochea vizuri, ... HAYATUUSU!
  • Viongozi waumize akili kukuza TAX BASE, si wanarahisisha mambo, kisha mtu mmoja mwenye kopato kiduchu anakamiliwa kila mara; watu wakichachamaa wanaambiwa kama hawataki 'kunyonywa' wahamie Burundi.
  • Viongozi waumize akili kwani wakirahisisha mambo wajue watalazimika kunywa chungu walioipika, haijalishi waliambiwa ng'ombera kiasi gani!
 
Wanajamvi, nimependa namna Mwandishi wa mwanahalisi alivyochambua hoja, ebu tupitie Kwa pamoja link hiyo tulijue kosa la Dkt Mwigulu Nchemba

--
KWA wanaofahamu jinsi serikali inavyofanya kazi, wanaofahamu kutungwa kwa muswada, kufikishwa kwa mswada huo bungeni na hadi kuwa sheria, hakuna shaka kuwa watakubaliana na mimi katika swali hili. Kwamba, “Kosa la Mwigulu, ni lipi?” Anaripoti Mwandishi Maalum … (endelea).
serikali anayoingoza.

Kwa muktadha huu, kinachotengenezwa dhidi ya Mwigulu sasa kupitia tozo, ni mwendelezo uleule wa kutengenezeana kile ambacho Kikwete alikiita kwa Lowassa, “ajali ya kisiasa.” Kwamba, anayetafutwa hapa ni mtu, sio tozo. Tusidanganyane.

Chanzo: Mwanahalisi Online
Mkuu KUZIMU, asante sana kwa bandiko hili, very informative.

Kwa vile serikali zinaongozwa na watu na sio malaika, na hao watu wanaweza kukosea kwa kuikosesha serikali, hivyo inapotokea serikali imekosea, then ni lazima atafutwe mtu atolewe kafara, kwa kufanywa mbuzi wa kafara, scapegoat, kwa Kizaramo ni "bangusilo" ili kuiokoa serikali.

Hivyo ikotokea ni kweli tozo ina tatizo genuine na kuna makosa, serikali imefanya kwenye tozo, serikali haiwezi kuwajibishwa, waowajibishwa ni watu, hivyo lazima atafutwe mbuzi wa kafara, achinjwe ili kuitumia damu ya kafara hiyo kuisafisha serikali, kwenye hili la tozo, mbuzi wetu ni mmoja tuu, the one and only!.
P
 
JamiiForums1772048058.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanajamvi, nimependa namna Mwandishi wa mwanahalisi alivyochambua hoja, ebu tupitie Kwa pamoja link hiyo tulijue kosa la Dkt Mwigulu Nchemba

--
KWA wanaofahamu jinsi serikali inavyofanya kazi, wanaofahamu kutungwa kwa muswada, kufikishwa kwa mswada huo bungeni na hadi kuwa sheria, hakuna shaka kuwa watakubaliana na mimi katika swali hili. Kwamba, “Kosa la Mwigulu, ni lipi?” Anaripoti Mwandishi Maalum … (endelea).

Kwamba, utaratibu wa kupeleka hoja kwenye Baraza la Mawaziri, unaanzia mbali kidogo. Hoja inaanzia kwa wataalam wa wizara chini ya Katibu Mkuu na wakurugenzi wake. Baada ya kuchambua na kujiridhisha na kile wanachokipendekeza, huwasilisha jambo hilo kwa waziri.

Kazi ya waziri, ni kulifikisha wazo hilo kwenye Baraza la Mawaziri, kupitia kitu kinachoitwa, “Cabinet Paper.” Mkutano wa Baraza la Mawaziri unaongozwa na Rais.

Wazo hilo la wataalam wa wizara likishafikishwa kwenye Baraza na iwapo libakubaliwa, linaondoka kwenye mikono ya wizara na kupelekwa kwa Kamati ya Makatibu wakuu wa wizara – Inter Ministerial Technical Committee (IMTC).

Kamati hii, hulichakata wazo lililoletwa na wakishajiridhisha wanalirudisha kwenye Baraza chini ya Katibu Mkuu Kiongozi.

Nalo Baraza likiona liko vizuri, maelekezo yanatolewa kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), kuandika muswada kulingana na maelekezo au mtazamo wa Kamati ya Wataalam ya makatibu wakuu kama ilivyopata baraka za Baraza la Mawaziri chini ya Mheshimiwa Rais.

Kwa muktadha wa sakata la tozo, wote ni mashahidi kuwa wazo lilianzia kwa aliyekuwa Spika wa Bunge, Job Yustino Ndugai. Alilitaka Bunge kuagiza serikali kuandaa muswada kwa ajili ya tozo za miamala ya simu na benki.

Katika mazingira hayo, ni serikali gani duniani itakwenda kinyume na maelekezo ya Bunge, tena ambayo yametolewa na Spika mwenyewe?

Katika suala zima la tozo, Serikali inaweza kusamehewa katika lawama na badala yake Ndugai na Bunge lake, ndiyo inauyopaswa kuwajibishwa.

Hii ni kwa kuwa Ndugai alikuwa na ajenda binafsi na jambo hili, hasa juu ya mkopo wa Sh. 1.3 trilioni ambazo serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan, ilikopa kutoka mashirika ya fedha ya kimataifa.

Ndugai alilenga kuonyesha umma, kuwa Rais Samia anaingiza nchi kwenye mikopo isiyokuwa na tija na hivyo, msimamo wake wa kuleta tozo, umelenga kuwaondolewa wananchi mzigo wa madeni. Kwamba, taifa hili, linaweza kujiendesha bila mikopo au misaada kutoka nje.

Kwa ufupi, alikuwa amejitosa rasmi kwenye mbio za urais 2025. Ndio msingi wa maneno yake, kwamba “ikifika 2025, wananchi wataamua wenyewe, wachague wanaotaka kuendesha nchi kwa mikopo au wanaoweza kuendesha nchi kwa mapato ya ndani.”

Hivyo basi, kwa kuwa tumeonesha jinsi mchakato wa sheria unapoanzia; shinikizo la Bunge lilivyokuwa kubwa katika sakata hili, unaweza kuona dhahiri kwamba kumlaumu Mwigulu, ni kutaka kumtoa kafara.

Kutaka Bunge kukaa pembeni na kulitupia suala hili lote mikononi mwa Mwigulu, ni kutaka kumuonea. Hii si haki!

Hakuna asiyefahamu jinsi Rais Samia anavyoheshimu demokrasia shirikishi, tangu akiwa waziri katika serikali ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete. Waliokuwapo bungeni wakati huo, wanaweza kuwa mashahidi wa hili.

Kwamba, Rais Samia – wakati huo, akiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), alikuwa anashirikisha hata wapinzani wake wa kisiasa, kwenye mambo yanayohusu maslahi ya umma.

Kwa mwenendo wake huo, Rais hakuzuia wabunge wa chama chake, kuchangia mjadala huu wa tozo kwa uwazi ndani ya Bunge. Hakuzuia maoni ya wabunge wake wala kuwalazimisha kupitisha hoja hiyo. Kila mbunge alikuwa huru kuchangia na kutoa maoni yake.

Kile ambacho kinaonekana sasa, ni hatua ya baadhi ya wabunge – wakiwamo wale waliounga mkono hoja ya Ndugai kuhusu tozo – kutaka kujiweka kando na sakata hili. Hili haliwezi kukubarika.

Yaani mtu amekuwa mbunge au waziri, ameliona jambo hili likipitishwa kote huko na yeye akiwamo, lakini hukulipinga wala kutoa maoni mbadala, kisha leo anataka kuwa wa kwanza kuonekana mtetezi wa wananchi, hili haliwezi kunyamaziwa.

Kuna taarifa zisizo na mashaka kwamba baadhi ya watu wanaokosoa tozo hizo hadharani au kuwatumia baadhi ya wananchi, wanafanya hivyo, kwa maslahi yao binafsi.

Hii ni kwa sababu, baadhi ya wanaopinga tozo sasa, walikuwa na nafasi ya kufanya hivyo ndani ya Bunge. Yawezekana hawakuweza kunyanyua mdomo kwa kuwa walimuhofia Ndugai. Kama madai hayo ni kweli, basi watakuwa wamepoteza sifa ya kuwa viongozi wa umma.

Hauwezi kuwa kiongozi wa umma, kisha ukawa mwoga wa kutetea maslahi ya wananchi au chama chako.

Wengine waliopo kwenye mradi huu, wameshiriki vikao vya Baraza la Mawaziri, ambako hoja hii ilipelekwa baada ya maelekezo ya Bunge la Ndugai. Hawakusema huko, hawakusema bungeni wala hawakusema kwenye vikao vya chama.

Kushindwa kujadili athari za tozo kwenye Baraza la Mawaziri, bungeni au kwenye kikao cha chama, ni hujuma dhidi ya Rais Samia na serikali anayoingoza.

Kwa muktadha huo, zigo hili, haliwezi kuachwa linasukumizwa kwa mtu mmoja – Mwigulu Lameck Nchemba – kwa baadhi ya watu kutaka kukimbia dhana ya uwajibikaji wa pamoja.

Kuendelea kumsakama Mwigulu kwenye hili, kunaweza kuthibitisha madai ya baadhi ya watu, kwamba kinachotafutwa hapa siyo tozo. ni Mwigulu.

Kwamba, watu wameona walitumie jambo hili, kummalizia kisiasa, lengo hasa likiwa uchaguzi mkuu wa 2030 (urais) na ule wa mwaka 2025, hasa kwenye wadhifa wa uwaziri mkuu.

Kwamba, kwa kutumia tozo, kutengenezwe mkakati wa kumpoteza yule anayeweza kuonekana kuwa mshindani wa kundi fulani.

Na huu ndio utaratibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM). Nani asiyejua kuwa Edward Lowassa, alisukiwa zengwe katika sakata la Richmond kwa sababu ya urais na uwaziri mkuu?

Nani asiyejua kuwa Hans Kitine, aliyekuwa waziri wa utawala Bora, katika serikali ya Benjamin Mkapa, alisulubiwa kwa sababu ya mbio za urais?

Aliyeibua sakata hilo bungeni, akatoa nyaraka na kuaminisha umma kuwa waziri huyo, ametumia madaraka yake vibaya, haikuwa muda alijitambulisha rasmi kuwa yuko upande gani kwenye mbio za kumrithi Mkapa.

Hata kilichompata Iddi Simba, mmoja wa wanasiasa mashuhuri na waziri mwenye nguvu katika serikali ya Mkapa, aliyelazimishwa kujiuzulu katika kilichoitwa, “kashifa ya sukari,” ilikuwa ni mbio za urais za mwaka 2005.

Shamsi Vuai Nahodha, aliyepata kuwa waziri Kiongozi wa Zanzibar na baadaye akateuliwa na Kikwete kuwa waziri wa mambo ya ndani, anaweza kuingizwa kwenye orodha ya walioathirika na mbio za urais.

Ni baada ya wabunge kumshikia bango ajiuzulu, kufuatia ripoti ya Kamati Teule ya Bunge juu ya utekelezaji wa Operesheni Tokomeza, kuwataja maofisa wa polisi kutenda uhalifu.

Lakini ndani ya mioyo ya wasuka mkakati, hoja haikuwa Tokomeza. Bali, ni mbio za urais wa Zanzibar mwaka 2020. Vuai na wenzake watatu – Balozi Khamis Sued Kagasheki, Emmanuel Nchimbi na Mathayo David – walilazimishwa kujiuzulu 20 Desemba 2013.

Kwa muktadha huu, kinachotengenezwa dhidi ya Mwigulu sasa kupitia tozo, ni mwendelezo uleule wa kutengenezeana kile ambacho Kikwete alikiita kwa Lowassa, “ajali ya kisiasa.” Kwamba, anayetafutwa hapa ni mtu, sio tozo. Tusidanganyane.

Chanzo: Mwanahalisi Online
Hayo yote hakuna asiyejua. Wote tunayajua kwa ufasaha kabisa..

Labda ukijibu maswali haya, unaweza kufungua ufahamu wako;

1. Una uhakika gani kuwa sheria hii ya tozo ambayo inafanya kazi sasa ilipitia hizo hatua..?

2. Viongozi wa serikali hii ya CCM, "impunity" imekuwa ni Jadi na utamaduni wao. Huyu Mwigulu ana character zote za "u - Magufuli". Magufuli hakuwahi kujali utaratibu, sheria wala katiba. Ndivyo alivyo Mwigulu Nchemba. Wewe una maoni gani kuhusu huyu mtu..??

3. Kosa la Mwigulu kubwa kabisa ni kukosa maadili ya kiuongozi. Kukosa kutuheshimu sisi wenye nchi yaani wananchi tuliompa dhamana ya u - waziri wa fedha afanye kazi kwa niaba yetu..

Kitendo chake cha kushindwa kuitetea serikali kwa lugha rahisi na yenye staha dhidi ya malalamiko ya wananchi kuhusu tozo na badala kututukana kwa kutuambia "...tunaolalamikia ukali wa tozo na kama hatutaki kulipa, basi tuhamie Burundi.." ni ishara ya kiwango cha juu kabisa cha ukosefu hekima na maadili kwa kiongozi wa umma mwenye dhamana ya uwaziri...

Hii pekee inaweza kuthibitisha bila shaka kuwa, tozo ni mchongo wa watu fulani tu ndani ya serikali akiwemo Rais Samia Suluhu. Hii jeuri ya waziri wake ya kutukana wananchi huku yeye akiwa amenyamaza kimya, ni uthibitisho kuwa ujinga huu wa waziri wake una baraka zake...

Kwa hiyo wote Rais Samia na waziri + cabinet yote wamekosa credibility ya kutuongoza. Hawawezi kututukana sisi. THEY MUST GO AWAY..!!!

4. Kutumia udhaifu wa kiuongozi wa Rais Samia Suluhu kufanyia uhuni wananchi. Ni kosa kubwa jingine..

Whether we like it or not, huyu mwanamke is unfit to be the main leader of this beautiful nation...

✓ Kwanza ni mwanamke ambaye hakuandaliwa kabisa kushika nafasi hiyo kubwa ya uongozi.

✓ Pili, ni mtu wa taifa jingine (hili hata yeye anajua na linamsumbua kiasi cha kutembea na "guilty conscious" inayopelekea asijiamini ktk kutekeleza majukumu yake)

✓ Kwa kutumia udhaifu huu, watu kama kina Mwigulu ndani ya serikali wanatumia fursa hii kupiga kwelikweli...

Kwa hiyo, kosa la Mwigulu ni kutumia udhaifu wa kiuongozi wa Rais Samia Suluhu kuhujumu wananchi kwa kuwaletea mateso huku yeye bila aibu akifanya mambo kama haya...

Huyu ana makosa na anastahili adhabu...!!
 
Kosa la rais wa mawe ni moja.kiburi na majivuno.

Huwezi waambia wananchi wasio ridhika na maamuzi ya kinyonyaji ya serikali wahamie Burundi.ile ilikua ni kejeli isiyo vumilika
Waache waparulane. Wakikosa wa kupingana naye nje (upinzani) wanapingana wao kwa wao
 
Bunge lilitunga sheria ya tozo. Bunge haikuweka viwango. Wqziri akatimga regulations zilizoweka namna ya kutoza na viwango. Namlaumu waziri. Alishindwa nini kuweka kiwango cha juu kuwa 2000?
 
Makala ni ndefu lakini bado imeshindwa kumuondoa Mwigulu kwenye lawama.Kwanza yeye ndiye Waziri wa fedha na mchakato Mwandishi anasema unaanzia kwa wataalaamu wa Wizara na baadaye Waziri wa fedha ndiyo anaupeleka kwenye Baraza la Mawaziri!!
Sasa yeye Waziri wa fedha anapelekaje hoja ambayo anajua kabisa ikipitishwa italeta mtikisiko kwenye Uchumi wa nchi?Kwani yeye Waziri wa fedha kama mchumi hajui kusoma na kuchambua mambo?
Mwandishi amezunguka kuanzia Bungeni akaja mpaka kwenye mbio za Urais 2025!
Je,tukisema kuwa Mwigulu naye alipeleka hoja kwenye Baraza la Mawaziri kwa mpango wa kumchafua Rais Samia mbele ya Wananchi ili aonekane anawakandamiza kwa tozo,tutakuwa tumekosea?maana Mwigulu naye anautaka Urais!!
Kwa kifupi ni Mwigulu kachemka na mwambieni,"Sabuni ya Mkaa haiwezi kusafisha kanzu nyeupe"
Uongozi unapewa na Mungu,Hakuna Mwanasiasa ambaye aliumba watu wa kumpigia kura,kama uamini kamuulize Lowasa na Raila Odinga kilichowapata
 
Back
Top Bottom