Ndugai: Mawaziri kutokuwepo Bungeni wakati hoja inajadiliwa ni Sawa!

Marire

JF-Expert Member
May 1, 2012
12,328
5,270
Muda mfupi uliopita Mh Kangi Lugola ameomba muongozo kwa Naibu spika kutaka kujua inakuweje leo wanajadili wizara muhimu kama ya chakula ambayo ndio tegemeo la Watanzania, ila ndani ya ukumbi wa bunge kuwepo mawaziri 5 na manaibu waziri 5 tu?
akajibiwa muongozo utatolewa baadae.

Mhe. Ndugai leo saa 6 na dk 11 mchana ametetea kutokuwepo kwa mawaziri bungeni wakati hoja zao (wakati huo) hoja ya Wizara ya kilimo inajadiliwa.

Akatoa mfano wa mfumo wa Bunge wa Kenya ati kuna kuna Mabunge 2 SENETI & BUNGE la kawaida ambako sasa mawaziri si wabunge na hawakanyagi bungeni, so akawaambia wabunge kutokuwepo mawaziri bungeni Si kitu cha kigeni.

JE NDUGAI analinganisha Bunge la Kenya & TZ? Sisi TZ hatujafikia kwa Mawaziri kutohudhuria Bungeni wakati hoja zao zinajadiliwa Bungeni.

Hivi wakati mawzairi wanakuja kujibu hoja huwa wanajibu hoja gani wakati hawakuwepo bungeni? Ni kweli mawaziri wanakuja kujibu kwa usahihi kama zilivyotolewa na wabunge?
 
Mbunge wa Mwibara,mh.Kangi lugola,ameomba muongozo wa naibu spika akihoji uwepo wa mawaziri 5 na manaibu mawaziri 5 tu ndani ya bunge leo hii.Mh.Lugola amehoji inakuwaje mjadala wa bajeti nyetia kama ya kilimo na chakula inakuwa na jumla ya mwaziri na manaibu waziri 10 tu ndani ya bunge!Hata hivyo,naibu spika ameahidi kutoa muongozo wake hapo badae.MY TAKE:HIVI KWELI KAULI MBIU YA "KILIMO KWANZA" IKO KWA VITENDO?JE, WAHESHIMIWA HAWA HAWATALIPWA SITTING ALLOWANCE KWA SIKU YA LEO?
 
Inatia hasira sana, hata wakiwepo huwa wanaongea ongea tu, tena kama huyo PM ndio kabisaaa!
 
Mhe. Ndugai leo saa 6 na dk 11 mchana ametetea kutokuwepo kwa mawaziri bungeni wakati hoja zao (wakati huo) hoja ya Wizara ya kilimo inajadiliwa.

Akatoa mfano wa mfumo wa Bunge wa Kenya ati kuna kuna Mabunge 2 SENETI & BUNGE la kawaida ambako sasa mawaziri si wabunge na hawakanyagi bungeni, so akawaambia wabunge kutokuwepo mawaziri bungeni Si kitu cha kigeni.

JE NDUGAI analinganisha Bunge la Kenya & TZ? Sisi TZ hatujafikia kwa Mawaziri kutohudhuria Bungeni wakati hoja zao zinajadiliwa Bungeni.

Hivi wakati mawzairi wanakuja kujibu hoja huwa wanajibu hoja gani wakati hawakuwepo bungeni? Ni kweli mawaziri wanakuja kujibu kwa usahihi kama zilivyotolewa na wabunge?
 
Sasa kwani waliwasilisha bungeni wasiwsilishe katika ofisi zao DSMS? Hiyo sio bajeti yetu watanzania? Sifahamu kanuni za bunge lakni common sense yangu inasema ni lazima wawepo bungeni wakati wote na hasa hoja zao zinapojadiliwa
 
Kwa Bunge la TZ hata wasipokuwepo Bungeni wana uhakika kuwa hakuna lolote baya litakalofanyika(ikiwamo bajeti ya wizara kutopitishwa) maana namba ya wabunge ya CCm ni kubwa sana na wana uhakika bajeti itapita tu baada ya makelele ya hapa na pale ya wapinzani Kutounga Mkono Bajeti.
 
Muda mfupi uliopita Mh Kangi Lugola ameomba muongozo kwa Naibu spika kutaka kujua inakuweje leo wanajadili wizara muhimu kama ya chakula ambayo ndio tegemeo la watanzania, ila ndani ya ukumbi wa bunge kuwepo mawaziri 5 na manaibu waziri 5 tu?
akajibiwa muongozo utatolewa baadae.

mkuu Marire, vuta subira, bado kitambo tutawapumzisha,wananchi tunaona ambavyo hawatimizi wajibu wao
 
wakuu,muongozo umetolewa kuwa mawaziri wapo hapo hapo dodoma na wanafuatilia shughuli za bunge huku wakijiandaa kwa bajeti zao
 
wakuu,muongozo umetolewa kuwa mawaziri wapo hapo hapo dodoma na wanafuatilia shughuli za bunge huku wakijiandaa kwa bajeti zao .
 
TZ imekuwa na bunge la mazoea tu. Kuhusu Kilimo Kwanza ni CHAKA LA KUTAFUNIA PESA ZA WALIPA KODI kwa kuanzia KUAGIZA NJE YA NCHI MBEGU, MATREKTA, POWER TILLER, MBOLEA, kununulia MSHANGINGI,PESA ZA UTAFITI, SEMINA/MAKONGAMANO, kuendesha MAONYESHO ya 8-8 pale MOROGORO kila Mwaka.
 
wakuu,muongozo umetolewa kuwa mawaziri wapo hapo hapo dodoma na wanafuatilia shughuli za bunge huku wakijiandaa kwa bajeti zao .
Mhh,
kama ndivyo basi hawajawahi kuwa serious
 
Ni jambo la kutia aibu, alafu bado rais anasema ajashindwa kuongoza nchi, Jaman Mungu tusaidie.
 
hata kama wangekuwepo sioni kama kungewepo na la maana ,mambo ni yale yale kwa watu walewale.
 
wakuu,muongozo umetolewa kuwa mawaziri wapo hapo hapo dodoma na wanafuatilia shughuli za bunge huku wakijiandaa kwa bajeti zao .

bila shaka wamejipumzisha mahotelini wanacheki kwa tv.
Tanzania tambarare sana.!!
 
wakuu,muongozo umetolewa kuwa mawaziri wapo hapo hapo dodoma na wanafuatilia shughuli za bunge huku wakijiandaa kwa bajeti zao .

Sheer stupidity as usual from these people!
They are never serious with anything....... hadi hapo watakapojikuta wametupwa nje ya utawala na hawataamini!
 
Mhe. Ndugai leo saa 6 na dk 11 mchana ametetea kutokuwepo kwa mawaziri bungeni wakati hoja zao (wakati huo) hoja ya Wizara ya kilimo inajadiliwa. Akatoa mfano wa mfumo wa Bunge wa Kenya ati kuna kuna Mabunge 2 SENETI & BUNGE la kawaida ambako sasa mawaziri si wabunge na hawakanyagi bungeni, so akawaambia wabunge kutokuwepo mawaziri bungeni Si kitu cha kigeni. JE NDUGAI analinganisha Bunge la Kenya & TZ sisi TZ hatujafikia kwa Mawaziri kutohudhuria Bungeni wakati hoja zao zinajadiliwa Bungeni. Hivi wakati mawzairi wanakuja kujibu hoja huwa wanajibu hoja gani wakati hawakuwepo bungeni? Ni kweli mawaziri wanakuja kujibu kwa usahihi kama zilivyotolewa na wabunge?

kuna mzee mmoja aliwahi kuniambia kuwa katika uongozi wa maslahi mkitaka kupata kiongozi mkuu lazima awe kilaza yaani awe ni mtu asiyejiamini alafu washauri wanakuwa ni wale wanaotaka maslahi ya failure ya uongozi. anasema katika hali kama hiyo ndiyo maslahi binafsi yanakamilika na katika haya ya bungeni naamini hivyo kabisa
 
Back
Top Bottom