Ndoto yangu ni kuwa Mpiga Picha wa Rais

Tuagize

JF-Expert Member
Dec 5, 2021
238
548
Habari Zenu,

Mimi ni Kijana, Umri 24, Ndoto yangu siku moja niwe mpiga picha wa Rais wa Tanzania, nimeanza kazi za upigaji picha, na uchukuaji Matukio kwa mtindo wa Video miaka 9 nyuma nimepata bahati ya kufanya na watu maarufu kadhaa, lakini kiu yangu ni kufanya kazi na Rais wa Tanzania,

Jana nilipokuwa kwenye Shughuli fulani nilimuona Kijana mdogo sana, Mpiga Picha wa Rais wa Zanziabar, Hakika nilivutiwa sana, na Kuamini Na mimi naweza siku moja kuwa miongoni wa wapiga picha wa Rais wa Tanzania, nina mazoea sana na aliyekuwa mpiga picha wa Rais mstaafu JK, Issa michuzi

Kwangu ni kama Uncle, na nilishamweleza kuwa natamani kuja kuwa kama wewe na hiyo ndio ndoto ya maisha, ananipa moyo nakuniambia pambana mungu atakujaalia itakuwa

Baba, Mama, Kaka, Dada zangu, hivi inawezekana mtu tu wa kawaida kuja kuwa mpiga Picha wa Rais, na nitumie Mbinu gani niweze kufanikisha Ndot yangu hiyo.

IMG_0309.jpg

IMG_9353.jpg

IMG_0314.jpg
 
Sio tu kuwa Mpiga picha unaweza hata kuwa wewe ndio Rais wa kupigwa picha

ongeza uzalendo na omba Mola wako

hawa waliowahi kuwa Rais ukimuondoa Jks nani alijipanga kuwa Rais walau kwa mwaka mmoja kabla ya kuwa Rais?

Ni Kweli mkubwa
 
Upo kwenye serikali tayari au any governing body..., una connection ? Huyo Mjomba wako ulivyomuuliza na kumwambia ndoto zako alikwambia ufanye nini ?

Anyway kwa ushauri wangu tengeneza Portfolio, tembelea vikao, na mikutano n.k. hata mikoania au sehemu ulipo piga picha viongozi hata kama utaanzia kwa mwenyekiti wa mtaa, tafuta matukio makubwa na madogo picha hizo zipeleke kwenye media tofauti na wauzie au wape ili upate exposure na kujenga CV, mara kwa mara tuma maombi au omba apprenticeship kwa wapiga picha wa sasa na waonyeshe kazi yao hata ukianza kwa kuwafutia lens na kuwabebea mabegi yao....

Envetually am sure utatoboa wala huenda hautahitaji kuwa mpiga picha wa Rais sababu huenda ukatoa kazi nzuri sana hata Mamlaka zikatumia za kwako...., Onyo ukiwa unafuatilia fuatilia na kupiga picha kila sehemu bila kutoa tahadhari au kuwataarifu Usalama wasije wakasema wewe ni gaidi na unatafuta nini kwahio ndio maana nikasema anza na matukio madogo madogo - kila Tukio nenda piga picha peleka kwenye media (Angalia Picha hizi siziwe za kudhalilisha, Sio unapiga Picha Rais amenuna au anapenga kamasi au anajikuna au kuchokonoa meno)
 
Upo kwenye serikali tayari au any governing body..., una connection ? Huyo Mjomba wako ulivyomuuliza na kumwambia ndoto zako alikwambia ufanye nini ?

Anyway kwa ushauri wangu tengeneza Portfolio, tembelea vikao, na mikutano n.k. hata mikoania au sehemu ulipo piga picha viongozi hata kama utaanzia kwa mwenyekiti wa mtaa, tafuta matukio makubwa na madogo picha hizo zipeleke kwenye media tofauti na wauzie au wape ili upate exposure na kujenga CV, mara kwa mara tuma maombi au omba apprenticeship kwa wapiga picha wa sasa na waonyeshe kazi yao hata ukianza kwa kuwafutia lens na kuwabebea mabegi yao....

Envetually am sure utatoboa wala huenda hautahitaji kuwa mpiga picha wa Rais sababu huenda ukatoa kazi nzuri sana hata Mamlaka zikatumia za kwako...., Onyo ukiwa unafuatilia fuatilia na kupiga picha kila sehemu bila kutoa tahadhari au kuwataarifu Usalama wasije wakasema wewe ni gaidi na unatafuta nini kwahio ndio maana nikasema anza na matukio madogo madogo - kila Tukio nenda piga picha peleka kwenye media

Sipo kwenye Taasisi yoyote ya kiserikali,

Alinimbia nisiwe na haraka taratibu itakuwa t
Kuwa tu
 
Bado mdogo Sana,subiri uzeeke kama kina michuzi,huwezi pewa kazi ya kumpiga picha rais na umri huo

Hapana sio lazima uzeeke ndoto upate hiyo nafasi, Jana tu nilikuwa na mpiga picha wa Rais wa Zanzibar, bwana mdogo sana na nilipiga Picha kali nikamuoneshea, akaipenda ile angle na kwenda, kuipiga kama nilivyoipiga
 
Sipo kwenye Taasisi yoyote ya kiserikali,

Alinimbia nisiwe na haraka taratibu itakuwa t
Kuwa tu
Taratibu itakuwa itakuwaje ? Process ni ipi yaani unakaa tu siku moja ngekewa zinashuka..., yaani huo utaratibu unaufanya ukiwa unafanya nini ? Kupiga Picha za Kitchen Party na Ubatizo ?

Anyway kwanini usichukue Kadi ya Chama Tawala hata uwe mpiga Picha wa kujitolea wa Chama hata ngazi ya mkoa ili hata wakujue kwamba una-exist au kama unadhani kuna chama kitakuja kuwa Tawala anzia huko kawe mpiga picha wao....; Sababu ni ndoto na hobbie yako hata isipokuwa utakuwa umefanya jambo unalolipenda....
 
Inawezekana, Kama Kuna chuo kasomee, ma juzi kwa waziri mkuu alikuwa anaitajika waiter, aliyesomea, food and beverage, kusevu meza za vyakula, kozi hiyo hipo veta miaka miwili, mtu kapata shavu, nazani hiyo kozi itakuwepo ya Mambo ya picha.

Nina uzoefu wa kutosha sana, na nazijua Camera vizuri sana, i mean kwenye camera hakuna kinachonishinda
 
Back
Top Bottom