utanisahihisha kama nimekosea....
- wanaotunza nyumba( usafi,mazingira, chumbani kwa mabosi) ni mahouse girl
- wanaotunza watoto ni mahouse girl
- wanaofuatilia maendeleo ya watoto ndio hao hao
- wanaomtayarishia baba mahitaji(maji ya kuoga, chai..nk.) bila kulalama uchovu ni mahousegirl
- bila housegirl chakula hakipo, kikiwepo basi kitachelewa na ladha hairidhishi
- mpangilio wa chakula mama lazima apate ushauri wake....utasikia ...dada leo tunapika/tunakula nini?
- akirudi mama huyu bado atampelekesha house girl bila kujali
- house girl huyu huyu hana uhuru wa kukaa meza moja kula chakula alichokiandaa mwenyewe akiwa na matajiri wake
- kosa dogo mtaa wa pili watalisikia kwa kelele zitakazotolewa na bibie tajiri
- akivaa vizuri pia nalo ni kosa endapo atasalimika kutuhumiwa mwizi
- hana haki ya kupumzika wala kula gudi taimu n.k
- ole wake acheke au atabasamu akiongea na baba then mama amuone kwa bahati mbaya...atakoma!