Ndoa za siku hizi

Kilambi

Member
Apr 3, 2009
94
18
utanisahihisha kama nimekosea....
  • wanaotunza nyumba( usafi,mazingira, chumbani kwa mabosi) ni mahouse girl
  • wanaotunza watoto ni mahouse girl
  • wanaofuatilia maendeleo ya watoto ndio hao hao
  • wanaomtayarishia baba mahitaji(maji ya kuoga, chai..nk.) bila kulalama uchovu ni mahousegirl
  • bila housegirl chakula hakipo, kikiwepo basi kitachelewa na ladha hairidhishi
  • mpangilio wa chakula mama lazima apate ushauri wake....utasikia ...dada leo tunapika/tunakula nini?
Pamoja na mengineyo mengi
  • akirudi mama huyu bado atampelekesha house girl bila kujali
  • house girl huyu huyu hana uhuru wa kukaa meza moja kula chakula alichokiandaa mwenyewe akiwa na matajiri wake
  • kosa dogo mtaa wa pili watalisikia kwa kelele zitakazotolewa na bibie tajiri
  • akivaa vizuri pia nalo ni kosa endapo atasalimika kutuhumiwa mwizi
  • hana haki ya kupumzika wala kula gudi taimu n.k
  • ole wake acheke au atabasamu akiongea na baba then mama amuone kwa bahati mbaya...atakoma!
Baba mie, sijui wengine__ I find it rahisi kumuomba/kumtuma hg maji ya kunywa, kubrash viatu, maji ya kuoga, n.k kwani atavifanya bila kulalama au kukunja uso__usinielewe vibaya ( sijafika unakofikiria)...TATIZO ni nini hasa? aaaaagghhhh!!!
 
sasa unalalama nini, kama vp fanya mwenyewe, unajua maji yalipo yawe ya kuoga, ya kunywa na nguo kunyoosha unaweza vilevile so fanya. unataka kufanyiwa na mkeo vyote hivyo bila kujali yeye pia katoka kazini kachoka kama wewe na kumsaidia hutaki. enzi za kutumikisha wanawake zishaisha, kama kazini tunaenda wote, na bado nina mzigo wa kubeba mimba na kuzaa na kutunza watoto na ninachangia family expenditures, why then should i still be your maid? Mi nafikiri ifikie mahali wanaume na nyie mbadilike, muone kusaidia kazi za nyumbani si kujidhalilisha, bali ni upendo kwa mkeo na msaada pia.kama ni mama wa nyumbani anaekaa home kusubiri utoke job ulete mahitaji ntakuelewa lakini kama ukiamka na yeye anaamka mnaenda wote job na kurudi, sioni kwa nini uwalaumu wanawake, play your part, they are people just like you.
 
wanaomtayarishia baba mahitaji(maji ya kuoga, chai..nk.) bila kulalama uchovu ni mahousegirl

This is a very chauvinistic approach towards life. Where do you live, under some cave somewhere near Kandhahar?
 
TATIZO ni nini hasa? aaaaagghhhh!!!

NA WAO WANAITAJI UPENDO WA KWELI
 
utanisahihisha kama nimekosea....
  • wanaotunza nyumba( usafi,mazingira, chumbani kwa mabosi) ni mahouse girl
  • wanaotunza watoto ni mahouse girl
  • wanaofuatilia maendeleo ya watoto ndio hao hao
  • wanaomtayarishia baba mahitaji(maji ya kuoga, chai..nk.) bila kulalama uchovu ni mahousegirl
  • bila housegirl chakula hakipo, kikiwepo basi kitachelewa na ladha hairidhishi
  • mpangilio wa chakula mama lazima apate ushauri wake....utasikia ...dada leo tunapika/tunakula nini?
Pamoja na mengineyo mengi
  • akirudi mama huyu bado atampelekesha house girl bila kujali
  • house girl huyu huyu hana uhuru wa kukaa meza moja kula chakula alichokiandaa mwenyewe akiwa na matajiri wake
  • kosa dogo mtaa wa pili watalisikia kwa kelele zitakazotolewa na bibie tajiri
  • akivaa vizuri pia nalo ni kosa endapo atasalimika kutuhumiwa mwizi
  • hana haki ya kupumzika wala kula gudi taimu n.k
  • ole wake acheke au atabasamu akiongea na baba then mama amuone kwa bahati mbaya...atakoma!
Baba mie, sijui wengine__ I find it rahisi kumuomba/kumtuma hg maji ya kunywa, kubrash viatu, maji ya kuoga, n.k kwani atavifanya bila kulalama au kukunja uso__usinielewe vibaya ( sijafika unakofikiria)...TATIZO ni nini hasa? aaaaagghhhh!!!

...upo sahihi hasa!

Tatizo ni kina mama wa kileo kujibweteka! ...wengine usipowatolea uvivu utakuta hata chupi za mkeo na boxers zako zinafuliwa na house girl!...

Muhimu baba mwenye nyumba kuhakikisha hako kabinti nako kanapata mahitaji yake muhimu ya kibinaadamu, ....!
 
sasa unalalama nini, kama vp fanya mwenyewe, unajua maji yalipo yawe ya kuoga, ya kunywa na nguo kunyoosha unaweza vilevile so fanya. unataka kufanyiwa na mkeo vyote hivyo bila kujali yeye pia katoka kazini kachoka kama wewe na kumsaidia hutaki. enzi za kutumikisha wanawake zishaisha, kama kazini tunaenda wote, na bado nina mzigo wa kubeba mimba na kuzaa na kutunza watoto na ninachangia family expenditures, why then should i still be your maid? Mi nafikiri ifikie mahali wanaume na nyie mbadilike, muone kusaidia kazi za nyumbani si kujidhalilisha, bali ni upendo kwa mkeo na msaada pia.kama ni mama wa nyumbani anaekaa home kusubiri utoke job ulete mahitaji ntakuelewa lakini kama ukiamka na yeye anaamka mnaenda wote job na kurudi, sioni kwa nini uwalaumu wanawake, play your part, they are people just like you.

...duuuuh, ....pheeeeeeeewwww! :eek: nilidhani mama watoto Nunda kumbe kuna waliomzidi!
 
Kuna wimbo mmoja wa dancehall jamaa anamwambia mke wake "washing machine, washing machine" na mke wake anamwambia "money machine, money machine"

Ndiyo mentality ya hii thread.
 
Kuna wimbo mmoja wa dancehall jamaa anamwambia mke wake "washing machine, washing machine" na mke wake anamwambia "money machine, money machine"

Ndiyo mentality ya hii thread.

Mmmh huo wimbo sijawahi kuusikia..nani kauimba huo niweze youtube!....

ila ni kweli haya mambo kila kitu housegirl afanye yamezidi sana tuu kwa watanzania.....kwanza hawatakiwi kuitwa housegirl ni Maids bana...i hate that name housegirl limekaa kiutumwa sana tuu
 
Kazi zote za muhimu kama kufanya usafi master bedroom, kufua nguo za mume na chakula cha mume umuaachie house girl hii ni too much. Hata kama ndio umama wa kisasa kwamba kazi nyingi za ofisini zimekuchosha lakini kuna vitu vya muhimu kama mke inabidi umfanyie mumeo.
Mume akichukua house girl uanze kulalamika na wakati mwenyewe umesahau kukaa nafasi yako kama mke.
Nikija kuwa mama hivi vitu vya msingi nitahakikisha nafanya mwenyewe hata kama nimechoka na kazi ya ofisi.
 
Duh inasikitisha jamni kweli ma housegirl wanachoka sna bado kamshahara kadogoo jamni???
 
Unajua hii ndio inachangia hata akina baba kumega tunda ma hao mabeki 3, kwa sababu kama hizo ulizotaja hapo juu, maana yeye kila unachosema hakatai, na mkeo ndio yupo busy au atajidai kachoka kweli kweli, sasa kwa hiyo wewe utaona upendo anao huyo beki3. kuna jamaa mmoja alikua analalamika kweli kweli kuhusu tabia ya mkewe kiasi kwamba akawa ananinymwa hadi unyumba, sasa huyo beki3 ndio akawa anafanya kila kitu amabacho alistahili kufanyiwa na mkewe ndio alipouliza je kwa nini asimuoe huyo beki3 wake kuliko manyanyaso ya mkewe. haya wadada kaeni chonjo
 
...upo sahihi hasa!

Tatizo ni kina mama wa kileo kujibweteka! ...wengine usipowatolea uvivu utakuta hata chupi za mkeo na boxers zako zinafuliwa na house girl!...

Muhimu baba mwenye nyumba kuhakikisha hako kabinti nako kanapata mahitaji yake muhimu ya kibinaadamu

Mbu umenichekesha hapo mahitaji muhimu na ya kibinadamu kama yapi?
 
Mimi nilishasema na kuandika hapa mara nyingi tu kuwa tuna ndoa za kihuni katika enzi hizi zetu. Eti siku hizi tunatafutana wake na waume tunaopendana na sio kuchaguliwa na wazazi wetu kwa sababu ilikuwa staili ya zamani na imepitwa na wakati.
Aaaah! Aaah Kama tunapendana mbona tunakula maha-housegirl na wengine kuliwa na maha-houseboy. Aaah! Aaah! Imekula kwetu kizazi hiki Wallahi tena nawaambia
 
Hizo za kumuachia Hg amuhudumie mzee kwa huduma zote kuanzai kumkaribisha home, kumfulia nguo, kumtandikia kitanda, kumnawisha wakati na baada ya kula, kumpikia chakula, kumpelekea maji ya kuoga n.k

Kwanini asimalizie na huduma yenyewe maana wazee husema "mke mwenye bidii ya kazi ni stadi pia kwenye majamboz"
 
Ukiamua kufukuza mke wako na kuoa au kumpa madaraka hausi gelo wa kuumiliki mwili wako hivi nae atatafuta nae hausi gelo yeye abakie kuwa boss?
 
Hizo za kumuachia Hg amuhudumie mzee kwa huduma zote kuanzai kumkaribisha home, kumfulia nguo, kumtandikia kitanda, kumnawisha wakati na baada ya kula, kumpikia chakula, kumpelekea maji ya kuoga n.k

Kwanini asimalizie na huduma yenyewe maana wazee husema "mke mwenye bidii ya kaji ni stadi pia kwenye majamboz"

lakini nyie wanaume
habu imagine hizi kazi zetu ,labda mme muda wa kutoka job saa tisa na nusu mke 11 or nakuendelea ,mnategemea na yeye atatoka saa tisa akamkaribishe mme ndo arudi job ?

Pia mwanaume una sauti katika nyumba kama hupendi kula menu ya H/G kwa nini usimwambie wife kama huridhiki kupikiwa na beki tatu.
lazima wife hata kama amechoka kiasi gani atakuandalia tu vile utakavyo
hii mambo ya kula mahousegal ni tamaa zenu tu
zipu ziko open everytime :)
 
...duuuuh, ....pheeeeeeeewwww! :eek: nilidhani mama watoto Nunda kumbe kuna waliomzidi!

Kaka I feel your feelings!! But with due respect kaka sometimes inabidi nanyi mara moja moja muwe mnayatia mapenzi chachu hata kwa kufanya kakitu kadogo kuonyesha kuwa unamsaidia wife. Sio unakuta mwingine kaka yeye anachojua ni kufanyiwa tu mfano
1. Anaamka asubuhi anakuamsha ukamwekee maji kwenye ndoo (na yanatoka bombani na ni master bedroom)
2. Umwekee dawa ya meno kwenye mswaki (usipoweka ataoga kisha atatoka kuja kuulizia mswaki wake)
3. Anatoka bafuni (hapo unakuta pant yake kaivua kaitupia kwenye sink anasubiri uje uife!)
4. Akitoka ushampigia pasi anavaa, anakunywa chai ulomwekea kisha huyooo funguo za gari zi wapi na akifika ndani ya gari ni honi mtindo mmoja unamchelewesha na usipokimbia na viatu mkononi anakuacha unakwenda ofcn kwa daladala au ukifanikiwa kuingia kwenye gari basi kusemwa mtindo mmoja unamchelewesha teke.

MCHANA KUTWA HATA KUKUPIGIA SIMU YA SALAMU AU SMS YA I MISS YOU!

5. Akirudi jioni akute chai yake mezani na maji bafuni
6. Atizame TV huku akisubiri chakula au asome magazeti yake
7. Akishakula huyooo kitandani analala huku akisubiri wewe uje ushushe neti na kumfunika na shuka!
8. Uingie kitandani baada ya kumaliza kazi zako akudake tayari kwa chakula cha usiku.
The life continues!

Kwa style hii kweli unategemea mkeo atakuwa anamapenzi na wewe? Si atajihisi hana tofauti na huyo housegirl jamani!

Jamani mara moja moja ukinisaidia kushusha net au hata kunipigia na mimi pasi I tell you nitaikumbuka kwa muda mrefu na moyo wangu kukongwa vilivyo!!
 
Back
Top Bottom