Ndoa za siku hizi

Carmel taratibu bi shost watakutoa macho hawa , si wote wenye utovu wa nidhamu katika ndoa zao.

Ofcourse wanaofanya vema haitawasumbua, ila watakaoreact na kunitoa macho wameguswa, si unajua ukilamba pilipili lazima uwashwe?

Mi sina ugonvi na wanaume, maana hatuwezi kuishi bila wao and wao pia hawawezi kuishi bila sisi, nachofanya ni kuwasaidia tu washtuke in case they have gone astray.
 
Hahahahaha luv angalia usije ukapasua keyboard mwisho wa siku wewe utabakia kuwa mwanamke na mmeo atabakia kuwa mwanaume tu lazima umlee kama mtoto mdogo ambae ananyonya.


c mpaka?...nyie mmepata hao wanawake wenu wenye wacwac/mashaka na ndoa, wanaona bila ndoa hawawezi kuishi kwenye hii dunia, mie walaaa nafanya kila kitu kwa kiac/kipimo chake wala cjiumizi eti kumfikiria cjui nicpofanya hivi atatoka nje cjui atafanya hivi na vile ahhh ni limtu lizima na akili zake linaloweza kunirekebisha pale linapokosea sio la kukimbilia plan b ambayo ni ya kipuuzi na itakayom cost.....
 
mhh mnaniudhi sasa, ya kwake anaipeleka wapi?...mnawaambiaga mpka salary zenu khaaa, mie pesa yangu ni yangu yake yetu.

You are lucky kama yako ni yako, mimi yangu ni yetu na yake vilevile yetu though i feel i am not supposed to contribute and then niwe maid. kama ninacontribute that means i deserve the same treatment. so atafua, atanyoosha, atasaidia kazi zote coz we decided to be equal partners. thats why sikubaliani na hizi story za mfulie baba, mpige mswaki baba, as a general rule, no, labda nifanye out of love tu na siyo general rule. na ndo maana hawezi kunifukuza na kunibebesha rambo kama fidel anayosema, labda aondoke yeye akichoka coz i have as much right to stay as he does
 
bora umetuwekea kiburudisho katikati...hii thread ingekuwa tunaiwakilisha live ningemtoa mtu jicho walaaah....
afadhali nimepata break na kuchekaa. du thanks shost si unajua hadi presure inapanda mida flani lol.
 
Yani Mwanajamii unaongea point sana leo du! Hii ndo dilema iliyoko kwenye ndoa nyingi sasa hivi, wanaume hawako responsible kabisaa, yani mke huioni pesa ya mumeo kisa anaamini unafanya kazi na una kipato, hawatoi pesa za matumizi ya wake zao, wanataka wake zao wachangie kwenye kila kitu kuanzia kula, kodi ya nyumba, ujenzi na hata kununua usafiri and yet bado wanalalama hapa eti wanawake wawafulie n bla bla,. The moment mlivyoacha kuwa responsible kama vichwa vya familia mlipoteza haki ya kufanyiwa mengine yote. kama dozi pia unaweza kuta wengine hata hawapati ya kuridhisha, at leat i am lucky in that one, phweeee!

carmel dada yangu yaani ndo yale yale tunayosema kila siku wengine wanalilia kuingia wakati wengine wanatamani kutoka.

Hapo kwenye Red- tena utakuta pamoja na kumfanyia kila kitu nata hiyo wanayosema haki yako ya ndoa huipati ukashiba. Yale yale anakugusa gusa tu yeye akishafika mwisho wa safari anakupa mgongo korroorrrooo korrooorrroooooo anakuacha unahesabu matundu kwenye siling board au unahesabu pingili za mabati.

Si ajabu ndo mana wengine wanasaidiwa na viserengeti
 
naomba nipingane na post ya mj1 kwamba wanawake wanachangia budget!NEVER ON EARTH(for the african women,NEVER)


haaa nasema kweli kumwaibisha shetani, mie ni wa kwanza...hata senti ctoi, c ndo mnajidai vichwa vya nyumba? sasa mnatakaje tena.
 
Ukipata mwanamke kama carmel mmmh! mm siku hiyo hiyo nakuacha inaonekana wewe katili sana yaani unamwachia mme ajifulie kufuli! eti kazi kusaidiana mmh wewe mama hebu tema mate juu.
 
haaa nasema kweli kumwaibisha shetani, mie ni wa kwanza...hata senti ctoi, c ndo mnajidai vichwa vya nyumba? sasa mnatakaje tena.

Sasa kama hutoi mbona kufuli humsaidii kufua sasa muelimishe huyo carmel naona anapotosha fikra za mwanamke wa kiafrica ambapo uasilia wake haupo hivyo
 
wapi Chriss, Masanilo, Geof, Fidel &Co? Mshasepa au mnapanga mashambulizi
 
Ukipata mwanamke kama carmel mmmh! mm siku hiyo hiyo nakuacha inaonekana wewe katili sana yaani unamwachia mme ajifulie kufuli! eti kazi kusaidiana mmh wewe mama hebu tema mate juu.
mi sitasema uongo, nacontribute home, sasa tena kwa nini iwe sheria mi kuwa maid wake? na kwa nini udhani mi katili just because hubby anasaidia kazi ndani? hudhani kuwa katili ni yule mwanaume ambaye hagusi kitu wala kutoa msaada kwa mkewe? badili mtazamo fidel.
 
Inategemea mkeo anafanya kazi gani na si kulalamika tu. kama mkeo ni mama wa nyumbani kweli kuna kazi nyingine hapaswi kufanya haosegirl kabisa ila kama mkeo wote mnatoka asubuhi manaenda kazini na kurudi jioni unategemea huyohuyo mkeo akirudi aanze kufanya hizo kazi zote ulizozitaja hapo?
 
mkuu Carmel,
chupi ya mumeo unafua au hufui?
nImesema nafua kwa upendo, nikijisiakia kufua lakini si general rule na hakuna anayeniuliza kwa nini nguo zangu chafu coz jibu analijua. so nafua nikiwa na muda. otherwise na mimi niko busy kusaka mahela si natakiwa nicontribute home? sasa nikitumia muda kufua na kupika na kunyoosha, ntapata wapi muda wa kusaka hela?
 
nImesema nafua kwa upendo, nikijisiakia kufua lakini si general rule na hakuna anayeniuliza kwa nini nguo zangu chafu coz jibu analijua. so nafua nikiwa na muda. otherwise na mimi niko busy kusaka mahela si natakiwa nicontribute home? sasa nikitumia muda kufua na kupika na kunyoosha, ntapata wapi muda wa kusaka hela?

safi,
kume wewe UNAFUA!
 
Its good umeshakubaliana na hali, after all ndoa ni kuvumiliana. just play your part kama ana akili na akiona wewe unafanya part yako vizuri basi atajirudi. just give her time, na kama kuongea naye usiongee naye kama unamforce kufanya unachotaka wewe. Jitahidi siku mko kwenye gud times, mdiscuss taratibu kwa upendo na atakuelewa.


Thanks , i guess you could be an angel that GOD has send to rescue my happiness !
 
Sasa kama hutoi mbona kufuli humsaidii kufua sasa muelimishe huyo carmel naona anapotosha fikra za mwanamke wa kiafrica ambapo uasilia wake haupo hivyo

Hujamwelewa nyamayao yeye hajakana kuwa hafui alikuwa anamshangaa mwanamke anayemwachia housegirl afue vyupi na boxers za mumewe.
 
Back
Top Bottom