Ndoa yangu imeanza kuingia kirusi cha aina yake

Kwa topic hii ya mshikaji sasa naanza kuamini kuwa kuoa/kuolewa ni suala la kujipanga kiakili na kiroho na wala sio suala la kuwa na pesa/nyumba/kazi
 
Inavyoelekea una hamu sana ya mtoto wakati mwenzio hana mpango wa kuwa na mtoto hivi karibu.Kwa mtizamo wangu suala la mtoto mlipaswa kujadili mkiwa bado wachumba.Hata hivyo hamjachelewa,Kaeni chini mufikie muafaka mnataka kuwa na watoto wangapi na lini.Mengine sameheaneni ikiwezekana muweke wazi kuwa una wasiwasi ili jambo hilo lisiendelee kukuuma.
 
Back
Top Bottom