Pdidy
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 50,956
- 22,148
Habari zaidi!
Ndoa ya mtoto wa Mungai bado kitendawili
Frank Leonard, Iringa
Daily News; Tuesday,February 24, 2009 @19:18
kura
Mahakama ya Mkoa wa Iringa imeshindwa kutoa uamuzi kesi ya madai namba moja ya mwaka 2009 inayomkabili mfanyabiashara maarufu wa mjini hapa, Jofrey Mungai baada Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Iringa kuitisha jalada la kesi hiyo.
Jofrey Mungai alishitakiwa mahakamani hapo na mkewe Vivian Mtasiwa waliyeishi kwa zaidi ya miaka 11 na kuchuma mali nyingi, baada ya kusikia Kanisa Katoliki Parokia ya Mshindo Iringa Mjini likitangaza ndoa mpya baina ya mumewe huyo na mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Tumaini Kampasi ya Iringa, Safina Herihaki.
Ndoa hiyo ilipangwa kufanyika Jumamosi ijayo, Februari 28.Mahakama hiyo iliyokuwa itoe uamuzi wake juzi baada ya Mungai kwa kupitia wakili wake, Basil Mkwata kuweka pingamizi kupinga madai yote ya mkewe huyo ambaye hajamtaliki.
Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mkoa wa Iringa, Firmin Matogoro aliyesikiliza pingamizi la kesi hiyo Februari 18 na kuahidi kutoa uamuzi Februari 23, alisema mahakamani hapo kwamba uamuzi dhidi ya pingamizi hilo haupo tena baada ya mmoja wa wahusika katika kesi hiyo (hakumtaja) kupeleka malalamiko ya mwenendo wa kesi hiyo kwa Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Iringa, Fakiri Jundu ambaye aliitisha jalada la kesi hiyo.
Pamoja na kumfikisha mahakamani, Mtasiwa aliweka pingamizi kanisani kuzuia ndoa hiyo isifanyike mpaka pale madai yake ya msingi dhidi ya mumewe huyo yatakaposikilizwa na mahakama.
Kanisa Katoliki kwa kupitia Katekista wake, Idfonce Kilamlilo ambaye pia ni Mwandikishaji wa Ndoa kanisani hapo lilithibitisha kupokea na kulikubali pingamizi la Mtasiwa mpaka pale wawili hao watakapomaliza tofauti zao au mahakama itakapotoa maelekezo mengine.
Katika mahakama hiyo, Mtasiwa anaomba amri ya mahakama ya kuzuia ndoa baina ya mumewe na Safina Herihaki mpaka pale madai yake yatakaposikilizwa na kutolewa uamuzi.
Katika hati ya madai anataka kupewa nusu ya mali zote walizochuma pamoja na mumewe huyo, matunzo kwake na watoto wawili waliozaa na kupata mgao wake kutokana na faida inayopatikana kutoka katika kampuni yao ya ujenzi ya GNMS.
Mungai ambaye ni mmoja wa wakurugenzi wa Kampuni ya ujenzi ya GNMS na mmiliki wa Hoteli ya kifahari ya White Horse Villa ya Iringa ni mtoto wa Charles Mungai ambaye ni mdogo wake na Waziri Mkongwe wa zamani, Joseph Mungai.