Ndoa huongeza muda wa kuishi.... naomba tujadili!

kabanga

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
37,208
18,476
[h=3][/h]

ndoa-kuishi-sana.jpg

Tafiti nyingi zinaonesha kuwa watu wengi walio funga ndoa wamewapiku wale wasio funga ndoa kwenye umri wa kuishi. Watafiti hawa wamebainisha kuwa mfumo wa maisha wa mtu aliye kwenye ndoa huchangia mabadiriko yake kifikira na hata kiuchumi hivyo kwa njia moja au nyingine ndio sababu ya wale walio kwenye ndoa kuishi kwa muda mrefu.
Wakati ndoa huchangia kuongea muda wa kuishi na faida nyingine nyingi kwenye afya ya binadamu, tafiti zinaonesha kuwa wale walio achika / tengana au wajane umri wao wa kuishi huwa mfupi kuliko wale wasioolewa /oa kabisa.

Bandugu, tujadili....
 
^^
Labda Umpate mnaendana kitabia,,ama sivyo jiandae kutumia vidonge vya kupunguza maumivu.
^^
 
ndoa zingine zinapunguza life expectancy,nyumbani hakukaliki kila muda kelele tu
 
Kivip? Na inakuwaje familia nyingi unakuta baba or mwanaume ndiye wakwanza kufa kuliko mama? Na hii imekaaje?
 
Kwa mtazamo wangu inaweza kuongeza muda wa kuishi na kupunguza muda wa kuishi. Inaongeza muda wa kuishi kama ndoa hiyo ina amani yaani wanandoa kama wanapendana kweli kweli. Inapunguza muda wa kuishi iwapo ndoa hiyo haina amani. Unajua amani inapokosekana ndani ya nyumba huongeza maumivu ya moyo na hii hupelekea mwanandoa mmojawapo kupata maradhi na hata kupoteza uhai wake kabla ya wakati
 
Khaa! Wacha nifloo hapa!
Ebhana unalosema SIO KWELI mkuu.....!
Wanandoa (ndoa bora) huonekana kuishi miaka mingi coz ma-single wengi huishi ovyo ovyo! Hapa kama tunawazingatia wenye ndoa bora ndio huishi sana, na upande wa pili tuzingatie single bora bas! Hapa tunapata jibu Single bora hugonga miaka ya kobe, refers Marehemu B kidude!
 
Kivip? Na inakuwaje familia nyingi unakuta baba or mwanaume ndiye wakwanza kufa kuliko mama? Na hii imekaaje?
Hii inatakiwa kuwa kama TOPIC Inayojitegemea hata mimi huwa nafikiria familia nyingi hata kama wazeeke vipi wa kwanza kufa huwa na BABA,
Mini nafikiria yafuatatayo:
1.KI Biblia baba ndo Kichwa cha familia,hivyo familia nyingi baba ndo anawaza kila kitu na utekelezaji wake,namna gani vitu viende,hata kama mama ana hela bt Mama hawezi kuwaza kama Baba,yaani kuchukua nafasi ya Baba.
2.Maumbile:
Shughuli za nguvu,risk,kujitoa,vyote humfanya baba aishe mapema,muda wote huwaza kutafuta while mama muda mwingi huwaza kutumia hata kama akitafuta.
3.kujitegemea...mwanamke anaweza kujitegemea anapokuwa mzee bila shida yoyote,na kufanya shughuli za kijamii,wakati mwanaume hawezi,husahau hata kujipikia,hivyo kuona ni kama mateso.
4......
 
Kivip? Na inakuwaje familia nyingi unakuta baba or mwanaume ndiye wakwanza kufa kuliko mama? Na hii imekaaje?
Hii mara nyingi inachangiwa na lifestyle za wazazi wetu wa kiume wakati mama (wengi wao) unamkuta katulia home anahangaikia watoto Dingi yupo bar anagonga mtungi,wakati mama anahangaika watoto watakula nini watasomaje dingi na midevu yake ka kambale unalikuta limekumbatiwa na nyumba ndogo mtaa wa 7 kama toto dogo,unajua mwisho kinachotokea ni nini???? Ni wazazi wa kiume kuwahi kufa kwa kisukari,pressure,ukimwi nk na hii huwa inachangiwa na manung'uniko ya watoto na mama juu ya anchokifanya dingi hapa mtaani kwetu ninapokaa kuna mifano hai kibaooooooo
 
kwenye ndoa nyingine wanaume wanawahi kufa kutokana na kuuliwa na wake zao.
 
Siamini hiyo....
Kamuzu Banda amefariki akiwa na umri 99
Papa John Paul alikufa aged 85
 
Back
Top Bottom