Ndivyo mlivyo wanaume wa Kichaga?

Jamaa ni mtanzania mwenye asili ya kichanga, nilifahamiana nae kwa kuwa mwanamke aliyeoa twatoka mkoa mmoja na mimi (lakini si uchagani) na tulikuwa tukifanya kazi ofisi moja na ndipo jamaa alipompatia hapo na mimi nilihusika kwa karibu kufanikisha waoane na kwa heshima huyo Mke huwa anani hesabu kama kaka yake (ana niita Kaka na na jaamaa ana niita shemeji).

Jamaa na Mkewe wote ni wasomi vijana na mungu kawabariki kupata kazi nono tu kila mmoja.

Hivi juzi huyo mke amekuja kunilalamikia, kuwa mumewe alimuomba siku za nyumba wanunue eneo (mbali kidogo na wanapoishi wao sasa), wakakubaliana kukunua na wakajenga vyumba kadhaa kwa mtaji wa mishahara ya kila mmoja. Lengo lilikuwa ni kupangisha, lakini cha ajabu jamaa amewahitisha ndugu wa upande wake (dada zake wawili) toka kijijini ndo wanaishi humo sasa. Bibie anasema amejaribu kumuuliza mume kwa nini iwe hivyo, anasema yeye ndo ameamua kwa kuwa ndo mwenye uamuzi kwenye familia na anapaswa kuwasaidia nduguze kimaisha…
Ndugu wa jamaa wamekuwa wakali kwa huyo mke, alikwenda kuitembelea nyumba , akakuta ndugu wamepangisha chumba kimoja na alipodadisi wakamweleza “kaka ndo amesema tufanye hivi ” lakini yeye (Mke) hakupewa taarifa yoyote na hajui hata kiasi cha kodi iliyokubalika hapo kwenye hiyo nyumba , amemuuliza mumewe kwa nini imekuwa vile anamjibu “ulitegemea wale watapata wapi hela ya kula???”(akimaanisha wale nduguze kwenye hiyo nyumba).
Amemweleza huyo mke asiwe anaenda huko na kuuliza habari zisizo na msingi kwa ndugu asije akaleta matatizo kwenye familia.
Duh, hivi ndivyo mlivyo wachaga?...

Wewe uliyeleta hii habari hapa ndiye mwenye matatizo makubwa. Kajifunze na kujirekebisha ili uweze kusiaidi wengi. Halafu hiyo mikono ulivyonyanyua inaonekana ni mwingi wa mipasho na umbeya.

Tatizo la mtu linaambatanishwa vipi na kabila? Labda, useme kuwa unammendea mke wa mwenzio kwa kisingizio kuwa kabila lake ni ishu! Poor Ngoshwe!
 
Back
Top Bottom