Ndege ya Lowassa inayopaa, na abiria walioachwa wameduwaa!

shame on you MwanakJJ! how dare you? uhuru wa mawazo siyo kufanya ulivyofanya yaani umechukua mstari mmoja na kuigeuza ili kumdhalilisha Waziri wetu Mkuu. Sijui inakupa furaha gani wewe huyo mzee kila akiamka anataka kujua magazeti yameandika nini kuhusu yeye. Umeshamsema inatosha anza wengine!
asante.

Mzee mwanakijiji dua la kuku limempata waziri mkuu na unamkoma nyani giladi kisawa sawa na huyu ngedere anaomba umwachie hafahamu kwamba shamba la bibi bado lina mazao, ataachiwa akimbilie kwenye mti aking'atuka.

BRAVO Mwanakijiji.
 
Waziri Mkuu anafanya kazi kwa ridhaa ya Rais na hadi hivi sasa hakuna utata kuwa Rais anaridhika na utendaji wake wa kazi. Kama Bunge linaona Waziri Mkuu hafai linaweza kupiga kura ya kutokuwa na imani naye. So, huyo ndiyo Waziri wetu Mkuu na anastahili heshima zote kama Waziri mkuu.

asante.

Bi senti ni kweli ndiye waziri wetu mkuu, hakuna anaye bisha, na hapa hatumlishi maneno nikweli ni maneno yake amesema mwenyewe kwa akili zake timamu bila kulazimishwa na mtu yeyote,

Eti amekaa Dom na viranja wake wakatugawia kasungura?? tunacho uliza kwanini watugawie kasungura? Yule ngombe wetu yuko wapi?

Bi senti.. Nakushauri umsaidie PM hekima ya kuongea, ila siyo kulaumu wote wanao ona mapungufu ya yale anayo ongea!

Ukimsaidia yeye akawa anaongea point basi wakumkosoa watakosa la kukosoa, kuliko uzuie/ulaumu wanao mkosoa wakati yeye anaendelea kutokosa!
 
shame on you MwanakJJ! how dare you? uhuru wa mawazo siyo kufanya ulivyofanya yaani umechukua mstari mmoja na kuigeuza ili kumdhalilisha Waziri wetu Mkuu. Sijui inakupa furaha gani wewe huyo mzee kila akiamka anataka kujua magazeti yameandika nini kuhusu yeye. Umeshamsema inatosha anza wengine!

asante.

nnazani haitoshi hadi akate roho kama dada amina ndio afurahi roho yake.

kwani wengine wanga kidogo
 
6laxl34.jpg


Kipanya naona ameanza 'kuua' kwa mabomu ya mionzi sasa... picha hisani ya Mjengwa Blog.


SteveD.
 
6laxl34.jpg


Kipanya naona ameanza 'kuua' kwa mabomu ya mionzi sasa... picha hisani ya Mjengwa Blog.


SteveD.
si angonesha moja kw amoja ushcumi umeporomoka huku ndee ya EL na dMuungwan ikipaa kwa kasi ya ajabu..
nchi hii bwana,labda turude kule kwa jirani zetu nadhani mambo yatakuwa mazuri,
Sawa wanachi wameelewa ,jewako tayari kuchukua hatua??tafakari
 
Siyo swala la kukurupuka kama alivyo zoea yule kiongozi hodari, shujaa na mahiri.

Issue si kupaa. Swala ni kuwa inaelekea wapi? Ndege ya Lowasa imepoteza mawasiliano hivyo hakuna uwakika wa kutua tena salama.
Kama nchi hii vyombo vya habari ususani magazeti, radio na Tv na Internet vitasambaa na kuwafikia watu wengi zaidi basi Lowassa ni historia ktk uongozi wa nchi hii. Serikali hii ipo madarakani kutokana na ignorance ya watanzania wengi ambao waishio vijijini. Serikali ilianguka pale JK alivyodondoka Jangwani na kamwe haiwezi kuinuka. Alikwepa Pale kirumba lakini jangwani alishindwa na huko Ikulu ni kushindwa tu na ndo maana mtu kama Edo yupo kwenye wadhifa aliyonao leo.
 
Mgambo wanane hoi wakikusanya michango

2007-12-12 09:22:57
Na Gideon Mwakanosya, PST Songea

Askari wa mgambo wanane wamejeruhiwa vibaya baada ya kupigwa na wananchi wakati wakiendesha msako wa wasiolipa michango ya ujenzi wa sekondari katika Kata ya Lilambo, Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma.

Kufuatia tukio hilo, watu watano wametiwa mbaroni na wanahojiwa na polisi.

Mgambo hao ambao walikuwa ni miongoni mwa 42, waliendesha msako huo usiku wa Desemba 5, mwaka huu, katika vijiji vitano vya kata hiyo.

Walifanya hivyo baada ya kuaminiwa na Ofisa Mtendaji wa Kata hiyo, Bw. Mapunda.

Naye Bw. Mapunda anadaiwa kuagizwa kufanya msako huo na Mkuu wa Wilaya ya Songea, Bw. Thomas Ole Sabaya.

Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma, Bw. Ectory Tenge, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Aliwataja watuhumiwa wanaoshikiliwa kuhusiana na tukio hilo kuwa ni Orestus Mbunda (41), Andrew Kihwili (43), Robert Luambano (32), Paul Haule (38) na Edwin Lugome (25) wote wakazi wa kijiji cha Lilambo `A`.

Taarifa zaidi zilieleza kuwa, siku hiyo ya tukio, askari hao mgambo walipita nyumba hadi nyumba na kuwakamata wananchi wasiolipa michango ya Sh. 10,000 kila mmoja, jambo ambalo lilionekana kuwa ni kero kwa wananchi.

Baadhi ya wakazi wa vijiji hivyo, ambao hawakutaka majina yatajwe walisema kuwa nyakati za usiku askari hao walivamia kwenye nyumba zao na kuwapiga sehemu mbali mbali za mwili huku, wakidai watoe michango ya ujenzi wa shule ya sekondari ya kata.

Wananchi hao wameuomba uongozi wa serikali ya mkoa wa Ruvuma kuona umuhimu wa kuingilia kati kusimamisha zoezi hilo, ambalo limeonekana kuwa ni kero kwa wananchi wa kata hiyo.

Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Songea, Bw.Yusuph Mruma, alikiri kuwepo kwa tukio hilo ambalo alidai kuwa limekwenda tofauti na maagizo yaliyotolewa na Mkuu wa wilaya.

Alisema kuwa pamoja na kutokea kwa tatizo hilo, Ofisi yake kwa kushirikiana na vyombo vya dola bado inaendelea kufanya uchunguzi.

Jitihada za waandishi wa habari kuwapata viongozi wa hospitali za Peramiho na ya mkoa Songea, hazikuzaa matunda baada ya kutokupatikana licha ya kuwepo kwa taarifa kuwa baadhi ya majeruhi wapo katika hospitali hizo kwa matibabu.

Bw. Tenge, alisema awali inadaiwa kuwa askari hao wa mgambo waliwakamata wananchi kadhaa ambao inadaiwa kuwa walishindwa kulipa michango hiyo ya ujenzi wa sekondari.

Alisema kuwa wananchi hao, walikamatwa na kufungiwa kwenye Ofisi ya Mtendaji wa kijiji cha Lilambo A lakini baadae wananchi wengine wa vijiji vitano vya Lilambo A, Lilambo B, Likuyufusi, Sinai na Mwanamonga, walifika kwenye ofisi hiyo na kuizingira kisha wakang`oa milango na madirisha na kuwatoa mahabusu hao ambao idadi yake haikujulikana mara moja.

Kutokana na kitendo hicho,. ndipo mapigano yalipoanza kati ya askari mgambo na wananchi ambao walikuwa wakipinga wenzao kuwekwa mahabusu na kwamba kuna baadhi ya askari mgambo walipigwa na kujeruhiwa vibaya lakini mpaka sasa hawajulikani waliko kufuatia kukimbia wakati wa tukio hilo.

Alitaja uharibifu wa samani kuwa ni meza mbili,milango miwili, madirisha mawili vyote vikiwa na thamani ya shilingi laki tano.

* SOURCE: Nipashe
 
Michango ni hiari na siyo lazima. Kama mtu hana hizo 10,000 wanataka akaibe ili alipe huo mchango? Siku zote lawama zimekuwa zikienda kwa viongozi wa upinzani na hasa kama mbunge ni wa kutoka upinzani. Katika hali yoyote ile hakuna ambaye anaweza kukubaliana na huu uhuni wa michango ya hiari kuwa malipo ya lazima. Nadhani sasa tunapata version mpya ya Kodi ya Maendeleo ya zama zile ambayo baadaye ilikuja kufutwa kwa sababu gharama za ukusanyaji zilikuwa kubwa na pia ilikuwa kero kwa wananchi. Ni vyema haya yanatokea kwenye eneo ambalo Mbunge na viongozi wa serikali wanatoka kwenye chama kimoja.

Viongozi wa kuchaguliwa na wananchi wanatakiwa kuwa makini zaidi na kuibana serikali ili isitumie mabavu kukusanya michango hiyo. Kwani wameshindwa kuwashawishi wananchi kutoa michango bila ya kutumia nguvu? Kazi kwao viongozi wa kuchaguliwa na wananchi, na wale wateule wa Rais wataendelea kupeta, lakini ndiyo wajue kwamba hata umaarufu wa Rais aliyewateua unashuka, maana hakuna mwananchi ambaye atampenda Rais anaeteua viongozi wa wilaya na mikoa ambao wanatumia nguvu badala ya ushawishi ili watu watoe michango yao kwa hiari.

Report ya REDET inaonyesha kwamba JK umaarufu wake umeporomoka kutoka asilimia 67 mpaka 44. Kama wakuu wa wilaya wataendelea na mwendo huu pasipo JK kuwakemea wazi wazi basi ajue wazi kwamba next time ataruka na asimilia ya namba ya kiatu, na wala asije akashangaa kuona umaarufu wake unashuka zaidi!
 
hii ni habari poa sana, nani atawasemea hawa wanavijiji kama hawatajichukulia hatua mikononi mwao. halafu sio kila mtu anaweza kuwa na sh 10,000 hasa wa kijijini ktk hali ngumu ya sasa hivi. halafu michango hii hailazimishwi watu wanachoka kodi kila mahali halafu bado na michango ya hiari lazima kwa nguvu tena.

wawape muda wajikusanye na sio kusema tunataka sekondari ijengwe kwa miezi kadhaa. Na hao wanamgambo waliowakamata kama ni wanavijiji wa hivyo vijiji nina hakika kuna ambao hawajalipa na wanasambaza kibano tu. Tuwe wastaarabu na misako ya usiku wapi na wapi mkiitwa majambazi itakuwaje.

na hivyo vifaa vilivyotajwa hapo vyenye thamani laki 5 let us be ralistic tusikuze mambo jamani.
 
Hii ni aibu kubwa kwa serikali ya CCM ambayo inawasamehe mafisadi kodi kwenye rasilimali zetu za madini na viongozi wake kujipendekeza kwa wageni ambao ndio wamewapa kipaumbele kwa sababu ya matumbo yao. Serikali imekosa mwelekeo.
 
hii inasikitisha sana, unajua unaposema mchango wa hiyari kisha ukatumia ubabe unakaribisha hii hali.

na usishngae wananchi wakaamua sasa kutokutoa makusudi waangalie liwalo na liwe.


hapa serikali yangu mmechemsha na nnaomba haraka hatua za muhimu zichukuliwe na hao waliosababisha hio hali wachukuliwe hatua.

nnaamini hili sio agizo la serikali kuu, serikali kuu imeeleza wazi kuwa michango ni ya hiyari iweje temna kwa mgambo usiku na vitisho.


hivi tunatengeneza waasi kwa mikono yetu ? jamani tuwe makini hii dunia nyengne sio ile ya mzee wa vijiji vya ujamaaa
 
Ache wale mkong'oto washenzi hawa wananyanyasa sana raia wema. Baada ya kichapo wapeleke ujumbe kwa boss wao,,, too much bullshit!!!!!
 
Mtu wa Pwani,

Una uhakika gani kwamba hilo siyo agizo la serikali? Last week kulikuwa na news inamhusu Masilingi kuwakoromea mkuu wa wilaya na watendaji wa kata kwamba wanatumia nguvu na vitisho kukusanya michango, huku wakimpaka matope yeye (Masilingi).

Leo ni news ya kutoka Songea, mgambo wameagizwa na Mkuu wa Wilaya na watendaji wa kata. Ninadhani kuna maeneo mengine mengi tu ambako haya yanafanyika lakini kwa kuwa vyombo vya habari havipo hakuna kinachoripotiwa redioni au magazetini. Serikali ya awamu ya nne sina imani nayo na hasa PM (EL) maana ndiyo kinara wa swala la elimu na michango. Inawezekana hao jamaa wana operate kwa agizo kutoka huko juu au wanashinikizwa kuhakikisha kwamba kila kata ina shule wakati wananchi hawana ubavu wa kuchangia ujenzi wa hizo shule. Je, utawatetea serikali kuu kwamba hawana mkono kwenye haya mabavu?

Miezi kama 2 iliyopita Kandoro alikuja na agizo kama hili, lakini yeye kwa kuwa ana wafanyakazi wengi maofisini aliamua kuwakata mishahara wafanyakazi, na pia magari kuyatoza ushuru (sikumbuki jina la ushuru), lakini watu walipopiga kelele jamaa alikaa kimya na kujitetea kwamba ilikuwa hiari. Itakuwaje hiari kwa kukata mshahara wa mfanyakazi moja kwa moja? Hiari ni pale mtu anapopeleka mshiko yeye mwenyewe bila kulazimishwa na mtu.

Kwa kifupi hapo iko namna, lazima kuna mkono wa serikali. Sidhani kama kuna DC au RC ambaye anaweza kukubali kupakwa matope na hata kutukanana na Mbunge au wananchi kwa ajili ya michango ya "hiari", lazima kuna kitu serikali imekificha ambacho wananchi hatukielewi. Ma RC/DC wanatekeleza maagizo ya serikali kwa kuwa wao ni wateuliwa wa Rais na hawawajibiki kwa wananchi moja kwa moja, na kama wakishindwa kufikia malengo maana yake ni kwamba wameshindwa kazi. Kama wamepewa lengo la shule kila kata na wananchi hawana hizo hela, unategemea wasitumie nguvu kukusanya hiyo michango? Maana akishindwa kufikia malengo inawezekana kibarua chake kikaota nyasi. Hizi news tunaziona ni kutoka kwenye wilaya ambazo watu wake hawana fedha ama ni wajuvi na hivyo hawataki kuonewa kwa kulazimishwa kuchanga michango ya hiari, ndiyo maana ma-DC wanatumia mabavu!!
 
Huyu Ole Sabaya hajui kwamba michango ya namna hiyo ilisha pitwa na wakati mbona analeta mfumo wa serikali za kikoloni tena. Migambo kutumika kuwasaka raia kama wahalifu lazima hatua walioichukua kwa kiasi fulani ni sahihi. LAZIMA WAACHIWE HURU, HAWANA KESI YA KUJIBU.
 
Unajua watanzania tumezidi uoga usiokuwa na maana. Kuna freedom of expression. Hii ni Article nyeti ambayo iko katika haki za binadamu. Msimtishe mtanzania mwenzetu mwenye uchungu na uozo wa serikali.

Kwa upande wangu;

Lowassa aliwahi kutamka kuwa uchumi umekua. I was shocked, manake uchumi kukua hali idadi ya wasomi haifiki 40,000. Uchumi umekua hali bado kuna watu wengi ambao hawajui kusoma na kuandika. Uchumi umekua hali kuna mfumuko wa bei (mfano mafuta). Nashangaa hizo inflation rates zao (yeye na viongozi wengine) ambazo hata hivyo zinapishana kila siku (pamoja na zile za Balali).

Mramba naye aliwahi kuropoka siku moja kuwa wataleta treni za umeme, sijui hizo treni zingeendeshwaje wakati kata kata ya umeme isiyo rasmi bado haijadhibitiwa, kama sio kupelekea watu kukwama njiani.

Huku ni kudhihirisha kuwa viongozi wetu wanakaa katika dunia tofauti huku rais wao akiwa anakaa kwenye sayari nyingine (probably Mars).

Waziri wa Fedha aliwahi kudhihirisha namna alivyokosa uelewa wa maswala ya fedha (ingawa aliwahi kumkashifu mheshimiwa Zitto ambaye ni mtaalamu wa Uchumi anayetambuliwa na baraza la maprofessa wa chuo kikuu), kuwa ana uelewa mdogo wa mambo ya senti; kwa kusema kuwa ukame, baa la njaa, na tatizo la umeme havijaathiri pato la taifa. Wataalamu wa fedha wanasema huku ni kudhihirisha ukilaza katika fani. Hajui kuwa pato la taifa linachangiwa na vitu vingi kwa mfano increased number of companies registered kwa mwaka n.k. The same madam aliwahi kudai kutetea unreasonably kupanda kwa kodi ya mafuta. Eti kodi itatengeneza barabara ambazo zitapunguza consumption ya mafuta. Sasa sijui na wakazi wa miji kama Dar watawekewa tiles au..?? Manake cost effect itakuwa pale pale. Inatisha..!!! Halafu mnasema uwaziri hausomewi. Kuna wizara nyeti ambazo lazima umweke mtaalamu, achana na wizara za jamii n.k.

Ukija kwa waheshimiwa wengine ambao hunifanya nikisikiliza kipindi cha bunge huwa natamani hata kuvunja TV. Wamekuwa wakiweka siasa kwenye eneo nyeti la uchumi. Lowassa amekuwa akijigamba sana kuhusiana na kukua kwa uchumi, mi sijui kule umasaini kuna maendeleo ya Joberg (South Africa) au..?? Ukienda vijiji vingine kunatisha. Hali ya miji kama Dar kwao ni kama South Africa fulani. Sasa sijui hali ya huko ikoje..!!!
 
Jamani, Jamani!!!
hao Mgambo Wanatekeleza Agizo Kuu La Kulinda Amani Na Utulivu! Tena Kwa Maslahi Ya Taifa!

Hivo Ri Afande Lazima Riwashughurikie Hao Raia Walio Haribu Ofisi Ya Serikari Na Kukiuka Maagizo Ya Kiongozi Ya Kutotoa Mchango Na Kujichukua Sheria Mkononi

Kwasababu Hawakutii Amri Harari Ya Kutoa Elfu Kumi Tayari Ni Ri Muarifu! Likamatwe Tena Usiku Na Kuwekwa Jera!.... ( Lol!)only In Bongo!!! amani Na Utulivu Kwa Kwenda Mbele
 
AIBU AIBU, ndugu wana JF siku moja nilikuwa nimesafiri kwenda katika vijiji vya wilaya ya mpwapwa wakati kodi ya kichwa (maendeleo)haijafutwa nikawa niko nafanya mahojiano ya kiutafiti na wanakijiji mara nikawaona wote wamekosa raha ghafla na wengine wakawa wameanza kukimbia nikadhani kuna majambazi wametuvamia. mara nikaona ni wanamgambo na mtendaji wa kata akiwa na baadhi ya wazee wamewafunga kwenye kamba. Nikauliza kwa nini? nikajibiwa kuwa hawajalipa kodi ya sh 3,000. kuangalia wale wazee wa kigogo wamejifunga yale mashuka yao ambayo yalikuwa yanaonekana dhahili kuwa hayajafuliwa toka yatoke dukani. sasa nikamuuliza yule mtendaji kuwa ni kweli hawa wazee yeye anaamini kuwa wanakwepa kodi au hawana? akasema wanakwepa! nikamuuliza kweli kama wanazo pesa unadhani hata wasingenunua hata sabuni ya kufua nguo zao; akasema wanaweza uza ngombe ili kulipa kodi? wazee wakasema na hao ngombe tayari walishawalipia kodi. nikainama nikakumbuka kule mjini ambavyo tunakatiza mitaa na pochi zenye pesa na hakuna mtu anayetuuliza ila vijijini ambako watu hawana pesa ndio wanaolipishwa. nikalipia karibu wazee nane waliokuwa wamechoka kwa kukimbia na kuvutwa na kamba ila na listi tena mtendaji akawa hana. Baada ya ubishi mkubwa akawafungua wale wazee akaahidi kuniletea mimi polisi kwa kumuharibia kazi. Ninadhani hizi shule zikijengwa kwa matumizi ya nguvu watu watazichukia matokeo yake hata watoto wao hawatawapeleka kusoma.
 
Waliwachagua wenyewe. Kwanza nadhani hao wananchi wamepata kipigo na usumbufu usiotosha. Hizo ndizo sera walizozichagua, sasa wanamlilia nani?
Mwaka 2010 waamke. Kuna mbunge mmoja wa upinzani nasikia aliwaambia wapiga kura wake kuwa lipeni kodi kwani huo ni wajibu wenu, mkishafanya hivyo kazi yenu mmemaliza. Michango ni hiari na uwezo wako.
Tutataka watu wa namna hii.
 
Not to advocate disorder, but drastic times calls for drastic measures.

Saaaafi sanaaaaaa, hii inaitwa "extended Robin Hood Theory", kodi na michango kibao kwa GDP per capita gani tuliyonayo? Halafu kibaya zaidi hamna hata uhakika kuwa hiyo michango itatumika kwa hizo girini wanazotuambia.

The mgambo militia are harassing people in violation of the constitution in a style fit for apartheid era South Africa or colonial Tanzania.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom