Ndege ya Air Tanzania yapata ajali ikiwa na abiria 35 Kigoma, hakuna vifo

Air Tanzania iliokuwa inaondoka leo Kigoma nusura kuanguka wakati ikiruka na imejipiga chini ndani ya bwawa ila hakuna abiria aliyepoteza maisha.

attachment.php

si ilifungiwa hii kampuni ya ndege au waliifungia kisiasa zaidi.. poleni wote mliopatwa na shock ya bila kujitakia..
 
kudadadekiiii, aibu gani hiii , ndege zenyewe zipo mbili tu , then zinatushindwa kutunza,
IVI SISI TUNAWEZA NINI JAMANI?????
Juzi treni limezima njiani kisa WESE hakuna ...

sisi kama tumelogwa. nakumbuka ******- alikwenda kusaini mkataba wa anga huru nchini uturuki , sasa sijui hii MIKANGAFU yetu kama inaweza kupaa anga za KIMATAIFA

Poleni watanzania WENZANGU


Hivi si na ile boeing bado ipo pale mwanza baada ya kutembelea tumbo mwaka juzi?
 
tbc ndio wamechemsha . amina mollel karudia mara tatu kwamba ndege imeanguka.

Watangazaji wetu ni washamba kupita kiasi hawajui chochote, wanachojua wao ni kusemaga HALI YA SINTOFAHAMU sijui kiswahili cha wapi hiki, mambo ya msingi zero, reporting zero. teh he he he.
 
kama Mtanzania.....habari za Air Tanzania zinaniuma sana.......
hasa pale ninapoona Kenya Airways, Rwanda Airways na Air Uganda......
sijui ni nani ametuloga jamani.........

KQ wameweka order ya Dreamliners 3 wakati ATC yetu the best aircraft ni hiyo ya mapanga ya mwaka 1976
 
Kazi kweli kweli raha ya milele uipe ee bwana na mwanga wa milele uiangazie ipumzike kwa amani...
Jamani natoka kuongea na mtu wa tcaa yuko pale kwenye tukio anasema kuna dalili ya kuizika ile ndege pale ilipo else garama zake ni karibu kununua kandege kengine nimehuzunika sana sana kwa nini tuendelee kuzika ndege hivi tumezika mwanza ,leo tuzike kigoma,,,tumekosea wapi kwa mola wetu jamani
 
kudadadekiiii, aibu gani hiii , ndege zenyewe zipo mbili tu , then zinatushindwa kutunza,
IVI SISI TUNAWEZA NINI JAMANI?????
Juzi treni limezima njiani kisa WESE hakuna ...

sisi kama tumelogwa. nakumbuka ******- alikwenda kusaini mkataba wa anga huru nchini uturuki , sasa sijui hii MIKANGAFU yetu kama inaweza kupaa anga za KIMATAIFA

Poleni watanzania WENZANGU

Tumethubutu, tumeweza na tunazidi kusonga mbele!
 
Serikali ya ccm na sheria yake ya vifaa mbofu mbofu itatutoa roho siku si zetu.
 
NI siasa ya ujamaa na kujitegemea iliyotufikisha tulipo. Amini usiamini.

"Mali ya umma" ndio kiini cha kufa kila kitu katika Tanzania.
Siasa ya UJAMAA na KUJITEGEMEA: ni kweli UJAMAA umetulea shida lakini tumekosea pia kuacha KUJITEGEMEA, kila kitu tunahitaji wafadhili, matokeo yake tumekuwa ombaomba duniani, hata matengenezo ya ndege hii utasikia tumeomba fedha toka nje, we subiri tu.
 
Precision mbona haianguki ingawa mvua ikinyenyesha maji yanaingia ndani ya ndege kama chujio la Nazi?
 
Kazi kweli kweli raha ya milele uipe ee bwana na mwanga wa milele uiangazie ipumzike kwa amani...
Jamani natoka kuongea na mtu wa tcaa yuko pale kwenye tukio anasema kuna dalili ya kuizika ile ndege pale ilipo else garama zake ni karibu kununua kandege kengine nimehuzunika sana sana kwa nini tuendelee kuzika ndege hivi tumezika mwanza ,leo tuzike kigoma,,,tumekosea wapi kwa mola wetu jamani


Inauma sana kusoma habari hizi kuhusu Air Tz na inauma sana kusema kwa sasa ndege za Air Tz si salama. Ni sawa kuziita Flying coffin.

Hakuna matumaini tena. Labda mpaka hapo M4C itakapofika kwenye kilele.
 
Habari zilizofika hivi punde ndege ya atcl dash 8 imepata ajali na hakuna aliyekufa ila ndege imeumia vibaya
Poleni sana atcl mbuzi wa maskini hazai
 
kama Mtanzania.....habari za Air Tanzania zinaniuma sana.......
hasa pale ninapoona Kenya Airways, Rwanda Airways na Air Uganda......
sijui ni nani ametuloga jamani.........

Preta usimtafute mchawi, hatujalogwa na mtu yeyote, tumejiloga wenyewe!!! Uchumi tunao lakini tumeukalia, au tumeuachia unaibiwa!!!

Baada ya jumuia ya Africa Mashariki kuvunjika, Kenya Tanzania na Uganda ziliaanza mkakati wa kujijenga binafsi nje ya wigo wa jumuia, ikiwemo kila nchi kuwa na shirka lake la ndege. Kenya Airways ilianzishwa chini ya serikali hadi mwaka 1996 lilipoanza kuendeshwa kama kampuni binafsi chini ya usimamizi wa serikali (public-preivate ownership), Air Tanzania ilianzishwa chini ya serikali lakini ikiendeshwa kama shirika la umma, na Uganda Airways ilianzishwa chini ya serikali lakini ikiendeshwa kama shirika la umma. Miaka 35 baadaye Kenya Airways (The Pride of Africa) ina ndege 34 zinazoruka na zingine 24 zimeagizwa na ina route fupi za ndani na za nje maeneo / viwanja 56. Uganda Airways ilianza kusuasua na ilipofika mwaka 2001 ikafilisiwa, na badala yake mnamo mwaka 2007 ikaanzishwa Air Uganda (The Wings of East Africa) ikiwa ni private company chini ya Aga Khan Fund for Economic Development (AKFED) na sasa ina ndege 38. Air Tanzania (Wings of Kilimanjaro) iliyoanza kwa kishindo na ndege 2 za Boeng ilib737, Fokker Frienship mbili na Twin Otter nne ilibinafisishwa mwaka 2002 ikawa chini ya South Africa Airways na mkataba huu ukavunjwa mwaka 2006. Baada ya mkataba kuvunjika Air Tanzania majeruhi alibaki na ndege 2 aina ya Bombardier Dash 8 na sasa baada ya ajali ya ndege (5H-MWG) imebaki na ndege moja (5H-MWF) ambayo iko matengenezo, hivyo haina ndege hewani. Jukumu la kubeba abiria wa ndege nchini Tanzania limebaki mikononi mwa Precission Air ambayo ina ndege 11 na nyingine 5 ziko zimeagizwa na inatua viwanja 14. Tanzania, Tanzania, Tanzania, nchi yangu, nakupenda!!! Air Tanzania, ingawa sasa huna ndege inayoruka, nitaendelea kukupendaaa!!!!.
RIP ATC.JPG
 
Serikali haina nia madhubuti ya kulikwamua shrika la ATCL....Ndege ilyodondoka ni aina ya DH-8 inayofanya scheduling ya Tabora to Kgoma to Dar kila siku iendayo kwa Mungu!ni ndege moja tu ndo imebaki...ipo nyingine mpaka leo nasikia ipo Hangar ya ATC ikifanyiwa matengenezo makubwa(wenyewe wanaita check-3)...kwa safari hizi ni hakika ndege moja haitoshi..inachoka na ni hatari kwa usalama wa abiria na Taifa!Ni kwanini ATC?Leo shirika binafsi la Precision linamiliki ndege kadhaa aina ya ATR45,ATR75 na BOING-733 Mbili...zinafanya safari ndani na nje ya nchi...Comoro,Nairobi adi South Africa kwanin sio ATC?Leo kuna 540.COM...Lina DH-8,CRJ-CANADIAN Kwanini sio ATC?Kwanin watu binafsi waweze halafu serikali yenye dhamana na kila amana ishndwe?kuna mkono wa Mtu na tunahtaji mabadiliko ya kweli..ni AIBUUUUUUU na uku nje ya nchi tunaaibika sana!


Ndugu yangu umenena kwa uchungu kabisa na haki yako. Through your presentation umenikumbusha Injili ya Mateso ya Bwana Yesu tuliyoisoma juzi ambapo Bwana Yesu baada ya kuona wanawake waliokuwa wanamlilia akawageukia akwaambia" Nyie wanawake wa Yerusalemu msinililie mimi, jililie nyie na wananenu..." Tnapaswa kuililia Tanzania na tijililie sisi wenyewe maana haya yote yalivyohasisiwa na mzee Ruksa na yakaenziwa na serikali ya Watanzania ni wavuvi wa kufikiri na ikafuatiwa na serikali ya kutembeza kombe kana kwamba Watanzania ni viwete hapo ndipo tulipofikishwa. Lakini kibaya zaidi hata uwezo wetu wa kufikiri naona na wenyewe kama umeathiriwa maana kama Jenerari Ulimwengu anavyotanabaisha kwenye makala zake hatutaki kurudi nyuma na kuangalia ni wapi tulipojikwaa kama Taifa. Ukiona watu wanakaa kutafuta mchawi na kulidhika ujue ni hatari. Mwalimu aliondoka akatuachia mashirika hata kama yalikuwa hayafanyi vizuri lakini yalikuwa na assets. Air Tanzania ilikuwa na assets na moja ya assets zake ilikuwa ni ndege pamoja na wataalamu. Kilichotokea nini? Tukaanza kuuza moja baada ya nyingine na tukaanza biashara ya kukodisha assets-ndege tukaishia kukodisha Air Bus ambayo hatukuwa na wataalamu kwa maana ya pilots, engineers an technicians wa kuifanyia matengenezo ya lazima nayo na hatukwa miundo mbinu ya kutua ila uwanja wa ndege wa Dar. Safari nyingine za nje zilishachukuliwa na South Africa Airways kupitia makubaliano ya kiulaghai tuliokuwa tumeingia. Waliofanya hivyo bado wanaishi Mwinyi. Mkapa na Kikwete wanatakiwa waulizwe na wajibu. Hapa sio kumungunya maneno wanajua walichofanya na ndio wanaweza kulekebisha kilichotokea. Hakuna njia ya mkato. Shirika lina wafanyakazi wengi mno ndege moja. Wa nini? Wanafanya kazi gani? Huku ni starve the hen and expect bear golden eggs. Ndio maana kidege kinafanyishwa safari nyingi
 
kama Mtanzania.....habari za Air Tanzania zinaniuma sana.......
hasa pale ninapoona Kenya Airways, Rwanda Airways na Air Uganda......
sijui ni nani ametuloga jamani.........
Aliyetuloga ni Nyerere, na bahati mbaya ameshakufa.
Mkapa akaongeza zindiko na JK amepoteza tunguli.
 
Kwangu kama mdau bado ni breaking news wewe kalia ya kanumba wako .... Umeniuzi kweli
 
Back
Top Bottom